Pundit.. tatizo la sisi tunaokaa nje au ambao tumekuwa exposed na affluence ya magharibi we have started to create this "instant mentality" where by one pushes a button na kitu hicho! unabonyeza namba mbili tatu, hela inachomoka, unaingiza hela hapa pale kopo la soda linatoka.
Hivyo tumefikia mahali hata kwenye kubadilisha oil ya gari huhitaji hata kutoka unaenda drive through wanakubadilisha oil na filter wewe unapiga soga unalipa unachomoka zako.
Sasa maisha haya ya nchi zilizoendelea ambazo ziko kwenye tier one zinatufanya na sisi kwa namna fulani tuamini kuwa Tanzania iko kwenye kundi hilo kwa sababu sisi Watanzania tunaoishi nchi za magharibi tunaenjoy maisha hayo.
Sasa leo ukitaka habari unaingia drudge report unaipata kabla haijafika CNN au FoxNews; ukitaka kujua maendeleo ya habari yoyote una "click" hapa na pale na habari inatokea and sometimes you can follow the news live as it is happening. Tunadhani Tanzania nako iko hivyo.
Tumesahau kuwa sisi tuko kwenye bottomo of the bottom tier! Sasa anapokuja mtu na gazeti au chombo chake habari na kuanza kuleta habari kwa haraka basi tunatarajia iwe kama au inakaribiana na "instant lifestyle" tuliyoizoea ambayo neno subira halipo. I wan't it, and I want it now!
Hivyo basi tunajikuta tunajiandaa kwa frustrations and disappointment. Kama ulivyosema, hivi haya magazeti yanapopokea matangazo ya intaneti ni kweli yanalipa kiasi cha kufanya wategemee matangazo hayo na si mauzo? NI makampuni mangapi ambayo yanatangaza kwenye intaneti Tanzania na ambayo yanaingiza biashara? Kutangaza kwenye intaneti kunapresume kuwa watu wengi (your target market) wana access ya hiyo intaneti. Vipi kama unatangaza lakini hilo tangazo halirudishi wateja?
NI kwa sababu hiyo basi magazeti kama Tanzania Daima na Raia Mwema na MwanaHalisi ambayo yanategemea zaidi mauzo kuliko matangazo ya biashara yanajikuta yanabadili mkakati wa kupata fedha na siyo suala la uzembe.
Hakuna kitu cha dezo na mambo ya ujamaa yalipita zamani. Tunaishi katika nchi ya kibepari na katika mfumo huu wa kibepari kinachopendwa na maximization of profit and individual success. Kama kuwahisha gazeti online kunapunguza mauzo ya magazeti mitaani what do you do? The answer is very clear.
Ndipo hapo tunaingia sisi wengine ambao tunajaribu kutengeneza mtandao wa habari kuweza kuleta habari za leo leo hii, na habari za sasa sasa. Guess what?
Do we get support? no.. watu wanataka dezo. Tunajaribu kuweka mtandao wa kutuletea habari kwa kadiri zinavyotokea lakini hao waleta habari wafanye kwa dezo kama kutoa sadaka kanisani? Linapotokea tukio mahali waende kwa nauli ya nani na watakapopata mahali pa kutumia intaneti cafe walipie kwa fedha zipi?
Hii ni changamoto kubwa kweli ya habari Tanzania na ndio maana kati ya vitu ambavyo kwa upande wangu ninajaribu kufanya ni kuunganisha nguvu za wale walioko nyumbani na sisi ambao tunaishi kwenye instant culture. Bado ni vigumu sana, so friends, cut them some slack otherwise.... anzisheni na nyie vyombo vyenu vitakavyoweza kufanya kazi kwa kujitolea kuleta habari 24 hours, no delay, no complains and see how easy it is.
M. M.