Tanzania & Corona - Biashara ya Mabilioni

wajibisha

Member
May 16, 2021
77
150
Habari za jioni Wakuu.

Kipyenga cha kuashiria mapambano dhidi ya Corona kimeshapigwa jana na ni suala la muda tu kabla ya hatua stahiki kuanza kuchukuliwa.

Wenzetu walishaanza mapambano haya mapema sana walianza na hatua za kufunga mipaka, watu wakalazimishwa kuvaa barakoa , social distance kwa wingi, lockdown za ndani ya nchi zikafuata na sasa wako kwenye hatua za mwisho za chanjo.

Cha ajabu tume yetu katika taarifa yake ya jana haikutoa mapendekezo tuanze na hatua ipi. Tufunge mipaka sasa hivi? Tuvae Barakoa? Ama tujikite moja kwa moja na kutoa chanjo? Na kama tunaenda na chanjo, tunaenda na ipi? Astrazaneca? Pfizer? Johnson & Johnson? Ama ile dawa ya kutoka kwa Mr. Putin?

Maono yangu yaninipeleka kuamini tulipofikia ni dhahiri shahiri hatua tunazoweza kuchukua ni kuhimiza uvaaji barakoa na chanjo ‘maana wenzetu washatoka kwenye lockdown na kufunga mipaka.

Chanjo ya COVID-19 imekua gumzo katika baadhi ya nchi za kiafrika kutokana na uchu wa baadhi ya viongozi kutaka kujineemesha kupitia janga hili.

Unaweza kujiuliza pesa ya haraka iko wapi hapa.

Taarifa zinaonyesha dozi moja ya kununua Astrazaneca inagharimu kati ya Tsh. 15,000 mpaka Tsh. 20,000. Hiyo ni bei ya kununua.

Hii inamaanisha dozi mbili itagharimu kama Tsh. 40,000 kwa bei ya juu.

Chukulia Kampuni X itapewa tenda ya kuleta hizi chanjo na tufanye hesabu za haraka haraka.

Idadi ya Dozi - 1,000,000
Bei ya manunuzi - Tsh. 40,000 kwa dozi
Jumla ya gharama za manunuzi - Tsh. 40,000,000,000 ama tusema Tsh. 40 Billion.
Ushuru- Zero Percent
Gharama za Kusafirisha - Weka asilimia 10% ya bei ya manunuzi- Tsh 4,000,000,000 as tuseme Tsh. 4 Billion
Jumla ya gharama za mzigo ( Cost of Sales) - Tsh. 44 Billion

Sasa mzigo umeshafika Dar, unafikiri bei ya Dozi inaweza kuwa kiasi gani?

Wakati unafikiria hilo kumbuka upimaji wa covid-19 hapa nchini ukitaka kusafiri ni USD 100 takribani Tsh. 230,000

Sasa tuseme bei ya full dozi itakua hiyo hiyo Tsh. 230,000.00 halafu turudi kwenye mahesabu.

Idadi ya Dozi - 1,000,000
Idadi ya watakopata chanjo - 500,000
Bei ya chanjo kwa mtu - Tsh. 230,000.00

Hesabu za Mauzo

500,000 X 230,000 = Tsh. 115,000,000,000 ama tuseme Tsh. Bilioni Mia Moja Kumi na Tano.

Hiyo hesabu ni kwa watu Laki Tano, Jiulize itakuaje kwa watu Milioni Moja, Tano, Kumi na n.k

Ushauri Serekali lazima iweke wazi taarifa za nani ataagiza hizi chanjo, ni Serekali yenyewe ama watu binafsi? Na vipi kuhusu usalama wa chanjo hizo kama makampuni yataruhusiwa kuagiza?

Kama nilivosema kipyenga ndio kwanza kimelia.
 

Elli M

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,112
2,000
Pinga hoja kwa hoja sheikh
Sheikh hapa hakuna hoja bali majungu! Kuna aina za uandishi unaona kabisa uelekeo wake sio wa kujenga bali kujimwambafai.

Recently kumekua na Wajuaji wengi sana ambao ni Anti-Samia wakija na maandiko marefuuuu yaliyojaa cheap propaganda including this one.

Hivi kweli kwenye Uhai wa mtu unaweza kusema ni biashara? Eti pesa itapatikana wapi? Halafu anataka mjadiliane
 

Kikiwo

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,776
2,000
Kweli hapo kuna pesa ya haraka shida very few pple will benefit labda kama una connection na kampuni itakayopewa tender ya kuagiza dozi za chanjo.
 

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,888
2,000
Sheikh hapa hakuna hoja bali majungu! Kuna aina za uandishi unaona kabisa uelekeo wake sio wa kujenga bali kujimwambafai.

Recently kumekua na Wajuaji wengi sana ambao ni Anti-Samia wakija na maandiko marefuuuu yaliyojaa cheap propaganda including this one.

Hivi kweli kwenye Uhai wa mtu unaweza kusema ni biashara? Eti pesa itapatikana wapi? Halafu anataka mjadiliane
Kama si biashara wagawe bure.
Alafu iwe Pfizer.!
 

wajibisha

Member
May 16, 2021
77
150
Sheikh hapa hakuna hoja bali majungu! Kuna aina za uandishi unaona kabisa uelekeo wake sio wa kujenga bali kujimwambafai.

Recently kumekua na Wajuaji wengi sana ambao ni Anti-Samia wakija na maandiko marefuuuu yaliyojaa cheap propaganda including this one.

Hivi kweli kwenye Uhai wa mtu unaweza kusema ni biashara? Eti pesa itapatikana wapi? Halafu anataka mjadiliane

Nitakujibu kama ni biashara ama sio biashara Pale tutakapopata chanjo bure.
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,387
2,000
Kenya mzigo waliopewa "Bure" umekata, ajabu kila aliyechanjwa alionjeshwa dozi moja ya pili ndio hivyo hakuna na ili angalau uwe na kinga kamili ni lazima update dozi mbili ..
Kuna mbinu wauza karanga huitumia Sana, anakulazimisha kukuonjesha, utanunua tu maana kuonja ni mara moja! Wakenya lazima wanunue tu, hatuwacheki ila ndipo na sisi tunapoelekea...ila Mimi chanjo labda wachome maiti yangu!
 

ikindo

Senior Member
Nov 29, 2011
109
225
Napata mashaka Sana na ripoti isiyokuwa na takwimu, sijui time imeweza vipi kuona hatari ya korona wakati kulikua hakuna takwimu Wala vipimo vya korona Hadi kuja na hayo mapendekezo, Tana inashangaza kuwa ni ripoti ya wasomi wetu na sio wanagenzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom