Mwanamalundi
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,125
- 1,432
Soma ukurasa wa 36
Kinga dhidi ya mashataka ya
na madai Sheria ya 1984
Na.15 ib.9 Sheria ya 1992
Na.20 ib
Kuna haja ya kuongeza kipengele kifuatacho
Kinga dhidi ya mashataka ya
na madai Sheria ya 1984
Na.15 ib.9 Sheria ya 1992
Na.20 ib
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.
Kuna haja ya kuongeza kipengele kifuatacho
(4) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), Raisi mstaafu atashtakiwa mahakamani itakapobainika kwamba alitumia madaraka kinyume na majukumu ya Uraisi, hususani katika maeneo yafuatayo:
(a) kwamba, alitumia madaraka yake kuhujumu utajiri wa Taifa
(b) kwamba, alitumia madaraka yake kuchochea aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,rushwa, uonevu au upendeleo
(c) kwamba, kwa kutumia madaraka yake, aliendesha shughuli za uchumi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache