Tanzania: Bei ya mafuta yapanda!

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Habari za usiku mabibi na mabwana.

Ninataarifa mbaya kwa watumiaji wa nishati ya mafuta hususan wale wenye magari na wafanyabiashara ya usafiri. Bei mpya elekezi inayotoka kila mwezi ipo tayari na inategemewa kuanzza kutumika kesho.

Bei hii mpya inasemekana itaongezeka kwa shilingi 300 kwa lita ya petrol na diesel sio shilingi 30 ni mia tatu kwa maneno. Kama unatia mafuta ya mjali hakikisha unapiga full tank!

Kupanda kwa mafuta ina maana moja tu! Nauli za mabasi na daladala zitapata! Usafirishaji wa bidhaa kwenyda masokoni nao. Utaongezeka bei hii itafanya bishaa kupanda bei pia.

Nawatakia usiku mmwema wadau.
 
Bei elekezi, mbona juu namna hiyo? miatatu 300 sio mchezo hata hiyo 30 ya diesel italeta matatizo. Ila shilingi nayo imetepweta jioni hii soko linafungwa $1:1,570/= hali si hali.
 
Bei elekezi, mbona juu namna hiyo? miatatu 300 sio mchezo hata hiyo 30 ya diesel italeta matatizo. Ila shilingi nayo imetepweta jioni hii soko linafungwa $1:1,570/= hali si hali.

hivi ulishawahi jiuliza kwa nini tz dola inapanda sana kuliko kushuka maana huu ni mwezi wa Sita tokea iwe 1500/$...

Je tatizo ni nini hasa na unataka nini kifanyike ili hii hali tuikwepe?

usiku mwema..
 
duh, hali mbaya.
Waweza kutujuza kwanini yamepanda kwa kiasi kikubwa hivyo?
Ni kwamba duniani kwa ujumla yamepanda au kuna uchakachuaji?
Kulikuwa na malalamiko ktk mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja, kama una data zaidi plz tunufaishe.
 
Baada ya bei ya mafuta kutulia kwa muda leo vyombo vya habari vimetangaza kuwa mafuta yamepanda bei. Ongezeko hili ni asilimia 14 ya bei ya jana. Je, kuna unafuu wowote unaotokana na kuwepo kwa EWURA na uagizaji wa mafuta kwa pamoja ulioanzishwa na serikali?
 
halafu mijitu ya Gas Stations huwa ikisikia tu bei imepanda, muda huo huo huwa inapandika bei mpya...ila ngoja mafuta yakishushwa bei, mpaka wakwaruzane na EWURA wee!
 
nauli na bei ya vyakula inaweza kupanda muda si mrefu.
Maisha magumu na ugumu unanngezeka zaidi.
 
Back
Top Bottom