Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 70,954
- 93,931
Maisha bora kwa kila mtz
mbona tutajuta
Maisha bora kwa kila mtz
Mkuu ndetichia, kapfo mangi, mbonyi tsa mfiri?hivi ulishawahi jiuliza kwa nini tz dola inapanda sana kuliko kushuka maana huu ni mwezi wa Sita tokea iwe 1500/$...
Je tatizo ni nini hasa na unataka nini kifanyike ili hii hali tuikwepe?
usiku mwema..
tusio na magari raha, labda ninywe ya buku tano tu.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepanda.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo jana bei mpya zitaanza kutumika kuanzia leo.
"Sambamba na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye Soko la Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012," ilieleza taarifa hiyo.
Kaguo katika taarifa hiyo alieleza kuwa bei za rejareja kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka, ambapo Petroli imepanda kwa Sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50; Dizeli Sh 199 kwa lita sawa na asilimia 10.26; na Mafuta ya Taa Sh 67 kwa sawa na asilimia 3.47.
"Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika kama ifuatavyo: Petroli imeongezeka kwa Sh 291.54 kwa lita sawa na asilimia 15.07; Dizeli Sh 199.57 kwa lita sawa na asilimia 10.68 na mafuta ya taa kwa Sh 67.29 kwa lita sawa na asilimia 3.63," aliseleza katika taarifa hiyo.
Alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni mpya iliyopitishwa na Ewura na kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la Desemba 23, 2011.
Kama huna gari utapanda bodaboda au daladala. Kwa bei hiyo expect nauli kupanda na. Ya chakula pia au unakula nyasi?
Wanabodi,
Najaribu kutafakari Hawa jamaa wa Ewura vigezo wanavytumia Kubadili Bei ya Mafuta Kila Mwezi.
Naomba ieleweke kuwa Mimi hapa silalamiki kwasababu Bei imepanda, Hata Pia ingeshuka kwa kiwango Cha Tshs 291 kwa lita kama ilivyopanda sasa lazima ningejiuliza maswali tena mengi.
Mwanzo Nilifikiri wazo la 'BULK BUYING' Lingepunguza gharama kwa waagizaji kwahiyo mafuta yangeshuka bei lakini mambo yamekua tofauti kabisa na matarajio yangu.
Hatuwezi kulinganisha ''INFALTION RATE'' na ''RATE'' ya kubadilika kwa bei ya mafuta. naona havina uwiano kabisa. hapa EWURA mnatuburuza.
Hivi kweli EWURA hakuna maslahi binafsi yanawapa msukumo katika upangaji wa hizi bei?
10,000/= you get four litres of petrol, with the current traffic jam in Dar? This is all Bullshit!!!!!!!!!!!
tusio na magari raha, labda ninywe ya buku tano tu.