FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,192
Tanzania hatukuanza kutetereka kiuchumi sababu ya Kagera.Faizafox, hakuna mtu anayemzuia Magufuli kufanya kazi na yeye asituzuie kutoa maoni yetu ailikuwepo Nyerere akatuacha wakaja wengine wakatuacha hata huyu ataiacha Tanzania kama alivyoikuta.
Nikutoe wasiwasi tu kuwa unaongea na mkongwe wa siasa aliyeshiriki vita vya Kagera.
Wewe ni kikongwe najua unajua Tanzania lini ilianza kuteteleka kiuchumi na sababu zake ikiwepo vita ya Kagera, pamoja na uchumi kuharibika Nyerere hakuruhusu mabeberu kuchimba dhahabu yetu, kuchimba gesi na mafuta yetu, aliwaambia wayaache hayaozi hadi tutakapopata uwezo na ujuzi wa kuyachimba, lkn walioachiwa kiti ndio hawa wanayagawa kama njugu kwa kisingizio cha uzalendo bubu, Nyerere kaiacha nchi na viwanda vingi tu, kwa hilo hatuwezi kumlaumu Nyerere.
Magufuli angemrithi Nyerere leo tusingekuwa na dhahabu wala gesi wala mafuta, hana uwezo wa kulinda maliasili kwa akili.
Umesahau Kennedy alileta msaada wa nini Tanganyika?
Tulikufa kiuchumi tulipoanza kutaifisha 1967.
Ungekuwa huruhusiwi kuongea ungekuwemo humu saa hizi?