Tanzania bado hatujapata Rais Mzalendo na Intellectual

Tanzania bado hatujapata Rais Mzalendo na Intellectual

Nakupinga magufuli siyo zalendo, huwezi nunua midege na kujenga uwanja wa ndege kijijini kwenu wakati wanakijiji wenzio wanakula mizizi

Hakuna mzalendo anatuma vikosi vya siri kuua na kuteka RAIA wake
Kijana una ushahidi juu ya hili la kuua???
 
Ukiwa mtu wa kulalamika lalamika bila hoja za msingi, hata uwezo wako wa kufikiri unakuwa mdogo.

Tuwaulize Chadema, Patriotic & Intellectuals wapo kwenye chama chao?

Mbona uko nje ya mada? Hivi umeelewa ulichoandika kweli? Hata kama umeamua kuwa Mjinga wakati mwingine ni bora kuficha ujinga wako. Pathetic
 
Yaaa mpaka tutakapompata mtetea mashoga Lisu

Mkuu Lisu alikufanyaga ni cha siri? Mana naona huwa unaumia sana juu yake, funguka tu unaweza pata ushauri wa kukutoa kwenye hiyo depression uliyonayo, kwani mficha maradhi kifo humuumbuwa. Humu kuna wajuvi mbalimbali so weka wazi swala lako utasaidikia.
Nb: Ushauri huu siyo wa lazima waweza endelea kuficha
 
Can ICT advancement be a factor in leading people? Uongozi wa miaka 60s,70s,80s,90s na wa sasa unaweza kuwa na changamoto Fulani ya ICT ama kukurahisishia kutawala au kufanya utawala ukawa mgumu zaidi.Magufuli,kwa mtazamo wangu, anafanya kazi nzuri kwa mazingira haya ya "kizazi kipya".

Kazi ipi inafanywa na jiwe? Nyie ndiyo mnampotosha jiwe kiasi cha kuonekana kachanganyikiwa. Mnasema kazi nzuri wakati huo huo hata yeye jiwe anajua hakuna alilolifanya na jamii inamchukia. Je wataka nikupe kauli nne za uongo kutoka kwa jiwe?
 
Sifa za raia yoyote ni mpaka awe marehemu,Nyerere angekua hai nyie ndio mngekua wa kwanza kumtukana ,ni mtazamo tu

So Kikwete na yeye ameshafariki siyo? Mbona wananchi wengi wanamkubali Kikwete compared na jiwe
 
Ni kweli aisee Tanzania kila mtu ni kocha.
Kwa mfano Mimi sijaelewa kwa nini Magufuli hayupo kwenye kundi la Intellectuals?
Kama research na planning zake hakuna mtu anayejua mbinu zake hadi leo.
Kwa mfano akiamua kutembelea wizara fulani anakuwa na data zote from A to Z.
Na Kama alikuwa na uwezo wa kujua mpaka idadi ya samaki,mifugo,barabara zote kwa nchi nzima na kujua bado ngapi zinaendelea na ujenzi pamoja na zitakazojengwa.
Kwa nini asiwe intellectual?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
We jamaa wewe !! Piga ua utakuwa ni msukuma, huwezi kuwa mjinga kiasi hiki, so kukariri nako ni mtu kuwa intellectual ?
Kweli TZ bado sana kama tuna watu wazima wanaoamini katika kukariri
 
Naona bwana vi audio umeamua kuandika porojo.. tulia na bora musomeshwe namba tu.

Umejaribu kuchokonoa mmebaki mataa.. sasa fahamu kwamba hata ikiwa 2025 tena kura tutampa JPM

Leo umeangalia ya Ikulu ukatamani mngekuwepo hapo kunywa kahawa huku mkiiba tu.. tulia ukalime acheni tamaaa

Endelea kulia na bado

Unatia huruma, pole sana lakini ndiyo maisha iko siku utatoboa tu
 
Sasa mbona Magufuli hvyo vyote anavyo coz ktk marais wote ni yeye tu ndio amethink beyond na kugundua kwamba tuna uwezo wa kujenga miundombinu ya kisasa bila mikopo ya nje.
Kwa Nini asiwe Intellectual.

“ Uwezo wa kujenga bila mikopo ya nje” hili unamaanisha kweli au just joking or you are uninformed
 
Mkuu Uzi nzuri,lakini kwa wanasiasa wetu wa hapo Tanzania unadhani nani kwasasa anasifa hizo zote mbili?
 
"Uzalendo" (patriotism) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unakaribiana sana na utaifa, ukizidi sana huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.

"Intellectual" (mtanisaidia kiswahili chake), is a person who engages in critical thinking, research, and reflection about society, proposes solutions, understand things especially complicated ideas.

Marais tuliowahi kuwa nao ni Nyerere tu aliyekuwa navyo angalau vyote.

Nyerere alikuwa Mzalendo na angalau alikuwa Intellectual.
Mwinyi hakuwa na Uzalendo wala hakuwa Intellectual. Tofautisha kuipenda nchi, kupenda watu wake na Uzalendo.
Mkapa alikuwa Intellectual lakini hakuwa Mzalendo.
Kikwete hakuwa Mzalendo lakini alikuwa mjanja half intellectual.
Magufuli ni Mzalendo lakini si Intellectual.

Nyerere alikuwa na uwezo wa kulinda maliasili za taifa alikuwa na uwezo wa kuwaambia wawekezaji wayaache madini hayaozi, alikuwa na mapenzi na nchi yake na watu wake alikuwa na uwezo kiakili na alikuwa haogopi challenges hata UN walitambua hilo.

Mwinyi hakuna na malengo yeyoye ya muda mrefu kwa nchi zaidi ya kusolve matatizo ya kipindi kifupi (biashara huria), hakuwa na uzalendo wala uwezo kiakili (critical thinking), alikuwa muoga wa challenges, alikuwa dhaifu kiuongozi.

Mkapa alikuwa na uwezo kiakili (critical thinker), hakuogopa challenges, lkn uwezo wake haukutumika kwa faida ya kulisaidia taifa (NBC case), alivunja misingi mingi ya kitaifa aliyoikuta, aligawa maliasili nyingi za taifa kwa wageni, hakuwa mzalendo.

Kikwete alipenda watu wake wa karibu (inner circle) lkn si nchi, half patriotism, hakupenda challenges ingawa hakuzikimbia (democracy case), hakujali sana maliasili za nchi kupotea iwe kwa kuibiwa au kwa mikataba feki, mengi alifanya kwa ajili yake na machache kwa ajili ya taifa (half intellectual).

Magufuli ni mzalendo halisi anaipenda nchi yake lakini siyo intellectual, anaogopa challenges, anataka kulinda maliasili za taifa lkn hana uwezo (hataki kujijengea uwezo) wa kugundua tricks za mabeberu, anatumia nguvu instead, (Acacia case), kwa kutambua hilo wajanja wanatumia uzalendo bubu kwa maslahi yao.

Tanzania tunataka Rais awe na vyote angalau Nyerere alionekana kuwa navyo, tunataka rais kama Putin, rais kama Kagame, Abiy Ahmed ambao ni patriotic na intellectuals.

Kwa utajiri tulionao siku Tanzania ikipata Rais mzalendo na intellectual hakuna nchi Afrika Mashariki na Kusini itakayotupata kwa maendeleo na uchumi, itakuwa nchi ya kulinganishwa na SA.
Ni MFUMO wa utawala chini ya CCM ambao unalea unafiki, dhuluma, udikteta nk. Nchi inajengwa kwa utawala wa Katiba na sheria ikiwa na "strong institutions" sio strong personalities kama unavyotaka.
 
Toa maoni kisomi , fanya ulinganishi kati ya hao uliotaja.

Usikurupuke
Yani mimi katika maraisi wote, namkubali Kikwete na mwinyi...

Kwanza nyerere ndio amesababisha haya yote

Nyerere ni overrated sana

..... Mfano mzee mwinyi ndio angekuwa raisi wetu wa kwanza, leo tungekuwa mbali sana
 
Yani mimi katika maraisi wote, namkubali Kikwete na mwinyi...

Kwanza nyerere ndio amesababisha haya yote

Nyerere ni overrated sana

..... Mfano mzee mwinyi ndio angekuwa raisi wetu wa kwanza, leo tungekuwa mbali sana
Baba yako kalifanyia nini taifa? Angepewa madaraka ya kusimamia watu mill 55 angeweza?

Familia ya watoto 3 inamshinda na kwenda kulala bar ,sembuse watu 55 mill???
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
We jamaa wewe !! Piga ua utakuwa ni msukuma, huwezi kuwa mjinga kiasi hiki, so kukariri nako ni mtu kuwa intellectual ?
Kweli TZ bado sana kama tuna watu wazima wanaoamini katika kukariri
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Mkuu Kama kukariri ni rahisi hebu kariri na wewe mifugo yote ya nchi nzima,lugha zote za kabila za Tanzania.
Au huko mbali sana lima hata shamba lako la mpunga au mahindi hekari 5 halaf ukariri idadi ya mahindi ili hata mwizi akiiba 5 uwe unajua.
 
Baba yako kalifanyia nini taifa? Angepewa madaraka ya kusimamia watu mill 55 angeweza?

Familia ya watoto 3 inamshinda na kwenda kulala bar ,sembuse watu 55 mill???
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Hapo umepigiria msumari aisee.
Utakuta mtu anamtukana raisi halaf yeye mwenyewe familia ya watoto watatu tu inayumba hadi watoto wake wanakosa nauli ya kwenda shule.
 
Back
Top Bottom