Tanzania bado hatujapata Rais Mzalendo na Intellectual

Tanzania bado hatujapata Rais Mzalendo na Intellectual

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,511
Reaction score
62,099
"Uzalendo" (patriotism) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unakaribiana sana na utaifa, ukizidi sana huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.

"Intellectual" (mtanisaidia kiswahili chake), is a person who engages in critical thinking, research, and reflection about society, proposes solutions, understand things especially complicated ideas.

Marais tuliowahi kuwa nao ni Nyerere tu aliyekuwa navyo angalau vyote.

Nyerere alikuwa Mzalendo na angalau alikuwa Intellectual. Mwinyi aliipenda nchi ila hakuwa mzalendo wala hakuwa Intellectual. Tofautisha kuipenda nchi, kupenda watu wake na Uzalendo. Mkapa alikuwa Intellectual lakini hakuwa Mzalendo. Kikwete hakuwa Mzalendo lakini alikuwa mjanja half intellectual. Magufuli ni Mzalendo lakini si Intellectual.

Nyerere alikuwa na uwezo wa kulinda maliasili za taifa alikuwa na uwezo wa kuwaambia wawekezaji wayaache madini hayaozi, alikuwa na mapenzi na nchi yake na watu wake alikuwa na uwezo kiakili na alikuwa haogopi challenges hata UN walitambua hilo.

Mwinyi hakuwa na malengo yeyoye ya muda mrefu kwa nchi zaidi ya kusolve matatizo ya kipindi kifupi (biashara huria), hakuwa na uzalendo wala uwezo kiakili (critical thinking), alikuwa muoga wa challenges, alikuwa dhaifu kiuongozi.

Mkapa alikuwa na uwezo kiakili (critical thinker), hakuogopa challenges, lkn uwezo wake haukutumika kwa faida ya kulisaidia taifa (NBC case), alivunja misingi mingi ya kitaifa aliyoikuta, aligawa maliasili nyingi za taifa kwa wageni, hakuwa mzalendo.

Kikwete alipenda watu wake wa karibu (inner circle) lkn si nchi, half patriotism, hakupenda challenges ingawa hakuzikimbia (democracy case), hakujali sana maliasili za nchi kupotea iwe kwa kuibiwa au kwa mikataba feki, mengi alifanya kwa ajili yake na machache kwa ajili ya taifa (half intellectual).

Magufuli ni mzalendo halisi anaipenda nchi yake lakini siyo intellectual, hana critical thinking yeyote anaogopa challenges, anataka kulinda maliasili za taifa lkn hana uwezo (hataki kujijengea uwezo) wa kugundua tricks za mabeberu, anatumia nguvu instead, (Acacia case), kwa kutambua hilo wajanja wanatumia uzalendo bubu kwa maslahi yao.

Ili tuendelee Tanzania tunataka Rais awe na vyote, angalau Nyerere alionekana kuwa navyo, tunataka rais kama Putin, rais kama Kagame, Abiy Ahmed ambao ni patriotic na intellectuals.

Kwa utajiri tulionao siku Tanzania ikipata Rais mzalendo na intellectual hakuna nchi Afrika Mashariki na Kusini itakayotupata kwa maendeleo na uchumi, itakuwa nchi ya kulinganishwa na SA.
 
Yani mimi katika maraisi wote, namkubali Kikwete na mwinyi...

Kwanza nyerere ndio amesababisha haya yote

Nyerere ni overrated sana

..... Mfano mzee mwinyi ndio angekuwa raisi wetu wa kwanza, leo tungekuwa mbali sana
 
Una msifu Nyerere kwa kuwa hukuishi kipindi chake, waliotusimulia hawana Hamu na Nyerere kwani wanadai alikuwa mbabe kupita kiasi na hakutaka kupingwa hata kwa hoja.

Kila mtu hafai kulingana na asili ya mwanadamu, Kama watu wanadiriki kumkosoa Mwenyezi Mungu, itakuwaje kwa mwanadamu tu?

Hakuna aliye mkamilifu na usidhani atapatikana kiongozi atakayependwa na kuwafurahisha watu wote, never!

Magufuli piga kazi mzee!
 
kwenye heading umesema bado hatujapata rais mzalendo na intellectual, kwenye content umesema Nyerere alikuwa na sifa hizo kama sio kuchanyikiwa huko ni nini?

Mazoea hujenga tabia , mazoea yenu ya kukosoa hovyo bila kufikiri ndio imepelekea ukashindwa kujua heading umeandika nini na content unatakiwa uandike nini.

Hakuna rais hata mmoja aliyekuwa haipendi Tanzania, walipigana kufa na kupona kwa ajili ya Tanzania, walifanya waliyotakiwa kufanya kwa uwezo wao na wengine wakaendeleza waliyofanya. Prof.Kabudi aliwahi kusema" ukitoka mahali fulani kwenda fulani usiangalie kwa jicho la sasa" na pia anapenda kusema" ukitaka kupima mafanikio angalia kina mtu alichokea na sio kimo alichofikia" .Tunasahau haraka msaada wa wazee wetu kwenye ujenzi wa nchi yetu kwa sababu ya unafiki
 
hao unaowasema walikuwa na roho ngumu na bado wengine ni wagumu haswa na ndo maana unaona maendeleo, tatizo leo hii mtu akifanya jambo kwa maslahi ya taifa tunakuwa na midomo sana na tunalia haswa, miaka ya nyuma watu walipotea sana na haikuwahi julikana walipotelea wapi na kutokana na uhaba wa vyombo vya porojo habari hazikuenea ka hivi leo, yani ni ka vile kupotea kwa alibino miaka ile,

Mtu ka kagame si mtu wa mchezo mchezo bana anafanya lolote ilimradi nchi yake iwe vizuri, je tuko tayari kuwapa ushirikiano iwapo watakuwa ka hao viongovi ulowataja?
 
Una msifu Nyerere kwa kuwa hukuishi kipindi chake, waliotusimulia hawana Hamu na Nyerere kwani wanadai alikuwa mbabe kupita kiasi na hakutaka kupingwa hata kwa hoja.

Kila mtu hafai kulingana na asili ya mwanadamu, Kama watu wanadiriki kumkosoa Mwenyezi Mungu, itakuwaje kwa mwanadamu tu?

Hakuna aliye mkamilifu na usidhani atapatikana kiongozi atakayependwa na kuwafurahisha watu wote, never!

Magufuli piga kazi mzee!
na alikuwa mbabe haswa tatizo sisi ni lawama tuu, ujamaa ulikuwa na madhara sana na baadhi ya maeneo haukuwezekana maana watu waliona kuacha vyao kwenda kujikusanya sehemu zisizo na maendeleo ni ujinga, alikuwa na mengi mazuri pia mabaya. mtu akisema Nyerere aliacha nchi baada ya kuona imemshinda najua wasiojua watakataa sana but ndo hivyo, kilakiongozi ni mbaya bana sema ubaya wake ni kwaajili ya taifa ama nani?
 
Una msifu Nyerere kwa kuwa hukuishi kipindi chake, waliotusimulia hawana Hamu na Nyerere kwani wanadai alikuwa mbabe kupita kiasi na hakutaka kupingwa hata kwa hoja.

Kila mtu hafai kulingana na asili ya mwanadamu, Kama watu wanadiriki kumkosoa Mwenyezi Mungu, itakuwaje kwa mwanadamu tu?

Hakuna aliye mkamilifu na usidhani atapatikana kiongozi atakayependwa na kuwafurahisha watu wote, never!

Magufuli piga kazi mzee!
Sasa umetoka kuipigania nchi, umezunguka sehemu mbalimbali mpaka mnakabidhiwa nchi.

Mara uhaini unatokea, mara tetesi za uhaini zinakufikia.

Utataka ushauri wa watu? Utataka kuamini watu? Lazima uwe mbabe, lazima uwe na circle ndogo ya watu unaowaamini.
 
Kwa upande wangu marais wote ni bora kwa kipindi chao Magufuli ni bora zaidi pia marais walio pita wana kili hilo
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Can ICT advancement be a factor in leading people? Uongozi wa miaka 60s,70s,80s,90s na wa sasa unaweza kuwa na changamoto Fulani ya ICT ama kukurahisishia kutawala au kufanya utawala ukawa mgumu zaidi.Magufuli,kwa mtazamo wangu, anafanya kazi nzuri kwa mazingira haya ya "kizazi kipya".
 
Una msifu Nyerere kwa kuwa hukuishi kipindi chake, waliotusimulia hawana Hamu na Nyerere kwani wanadai alikuwa mbabe kupita kiasi na hakutaka kupingwa hata kwa hoja.

Kila mtu hafai kulingana na asili ya mwanadamu, Kama watu wanadiriki kumkosoa Mwenyezi Mungu, itakuwaje kwa mwanadamu tu?

Hakuna aliye mkamilifu na usidhani atapatikana kiongozi atakayependwa na kuwafurahisha watu wote, never!

Magufuli piga kazi mzee!
Kama unakiri kuwa hata Mungu anakosolewa, kwann uyo Msukuma wenu yy hataki kukosolewa, na akikosolewa nyinyi msio na kazi mnawatusi wanaomkosoa, as if huyo ngosha ni mungu mkuu
 
Una msifu Nyerere kwa kuwa hukuishi kipindi chake, waliotusimulia hawana Hamu na Nyerere kwani wanadai alikuwa mbabe kupita kiasi na hakutaka kupingwa hata kwa hoja.

Kila mtu hafai kulingana na asili ya mwanadamu, Kama watu wanadiriki kumkosoa Mwenyezi Mungu, itakuwaje kwa mwanadamu tu?

Hakuna aliye mkamilifu na usidhani atapatikana kiongozi atakayependwa na kuwafurahisha watu wote, never!

Magufuli piga kazi mzee!
Huu ni uchambuzi binafsi haujamlenga mtu, wala sijamzuia Magufuli kupiga kazi.

Unasema wewe umesimuliwa ya Nyerere wengine tumefanya naye kazi, hata yeye alikuwa na mapungufu kwa maeneo mengine lkn si kwa haya niliyohoji ukilinganisha na marais wengine.
 
Back
Top Bottom