"Uzalendo" (patriotism) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unakaribiana sana na utaifa, ukizidi sana huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.
"Intellectual" (mtanisaidia kiswahili chake), is a person who engages in critical thinking, research, and reflection about society, proposes solutions, understand things especially complicated ideas.
Marais tuliowahi kuwa nao ni Nyerere tu aliyekuwa navyo angalau vyote.
Nyerere alikuwa Mzalendo na angalau alikuwa Intellectual.
Mwinyi hakuwa na Uzalendo wala hakuwa Intellectual.
Mkapa alikuwa Intellectual lakini hakuwa Mzalendo.
Kikwete hakuwa Mzalendo lakini alikuwa mjanja half intellectual.
Magufuli ni Mzalendo lakini si Intellectual.
Nyerere alikuwa na uwezo wa kulinda maliasili za taifa alikuwa na uwezo wa kuwaambia wawekezaji wayaache madini hayaozi, alikuwa na mapenzi na nchi yake na watu wake alikuwa na uwezo kiakili na alikuwa haogopi challenges hata UN walitambua hilo.
Mwinyi hakuna na malengo yeyoye ya muda mrefu kwa nchi zaidi ya kusolve matatizo ya kipindi kifupi (biashara huria), hakuwa na uzalendo wala uwezo kiakili (critical thinking), alikuwa muoga wa challenges, alikuwa dhaifu kiuongozi.
Mkapa alikuwa na uwezo kiakili (critical thinker), hakuogopa challenges, lkn uwezo wake haukutumika kwa faida ya kulisaidia taifa (NBC case), alivunja misingi mingi ya kitaifa aliyoikuta, aligawa maliasili nyingi za taifa kwa wageni, hakuwa mzalendo.
Kikwete alipenda watu wake wa karibu lkn si nchi half patriotism, hakupenda challenges ingawa hakuzikimbia (democracy case), hakujali sana maliasili za nchi kupotea iwe kwa kuibiwa au kwa mikataba feki, mengi alifanya kwa ajili yake na machache kwa ajili ya taifa (half intellectual).
Magufuli ni mzalendo halisi anaipenda nchi yake lakini siyo intellectual, anaogopa challenges, anataka kulinda maliasili za taifa lkn hana uwezo anatumia nguvu badala ya akili, (Acacia case), kwa kutambua hilo wajanja wanatumia uzalendo bubu kwa maslahi yao.
Tanzania tunataka Rais awe na vyote angalau Nyerere alionekana kuwa navyo, tunataka rais kama Putin, rais kama Kagame ambao ni patriotic na intellectuals.