Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,484
- 2,892
Mtanzania,"Uzalendo" (patriotism) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake. Uzalendo unakaribiana sana na utaifa, ukizidi sana huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.
"Intellectual" (mtanisaidia kiswahili chake), is a person who engages in critical thinking, research, and reflection about society, proposes solutions, understand things especially complicated ideas.
Marais tuliowahi kuwa nao ni Nyerere tu aliyekuwa navyo angalau vyote.
Nyerere alikuwa Mzalendo na angalau alikuwa Intellectual.
Mwinyi hakuwa na Uzalendo wala hakuwa Intellectual. Tofautisha kuipenda nchi, kupenda watu wake na Uzalendo.
Mkapa alikuwa Intellectual lakini hakuwa Mzalendo.
Kikwete hakuwa Mzalendo lakini alikuwa mjanja half intellectual.
Magufuli ni Mzalendo lakini si Intellectual.
Nyerere alikuwa na uwezo wa kulinda maliasili za taifa alikuwa na uwezo wa kuwaambia wawekezaji wayaache madini hayaozi, alikuwa na mapenzi na nchi yake na watu wake alikuwa na uwezo kiakili na alikuwa haogopi challenges hata UN walitambua hilo.
Mwinyi hakuna na malengo yeyoye ya muda mrefu kwa nchi zaidi ya kusolve matatizo ya kipindi kifupi (biashara huria), hakuwa na uzalendo wala uwezo kiakili (critical thinking), alikuwa muoga wa challenges, alikuwa dhaifu kiuongozi.
Mkapa alikuwa na uwezo kiakili (critical thinker), hakuogopa challenges, lkn uwezo wake haukutumika kwa faida ya kulisaidia taifa (NBC case), alivunja misingi mingi ya kitaifa aliyoikuta, aligawa maliasili nyingi za taifa kwa wageni, hakuwa mzalendo.
Kikwete alipenda watu wake wa karibu (inner circle) lkn si nchi, half patriotism, hakupenda challenges ingawa hakuzikimbia (democracy case), hakujali sana maliasili za nchi kupotea iwe kwa kuibiwa au kwa mikataba feki, mengi alifanya kwa ajili yake na machache kwa ajili ya taifa (half intellectual).
Magufuli ni mzalendo halisi anaipenda nchi yake lakini siyo intellectual, anaogopa challenges, anataka kulinda maliasili za taifa lkn hana uwezo (hataki kujijengea uwezo) wa kugundua tricks za mabeberu, anatumia nguvu instead, (Acacia case), kwa kutambua hilo wajanja wanatumia uzalendo bubu kwa maslahi yao.
Tanzania tunataka Rais awe na vyote angalau Nyerere alionekana kuwa navyo, tunataka rais kama Putin, rais kama Kagame, Abiy Ahmed ambao ni patriotic na intellectuals.
Kwa utajiri tulionao siku Tanzania ikipata Rais mzalendo na intellectual hakuna nchi Afrika Mashariki na Kusini itakayotupata kwa maendeleo na uchumi, itakuwa nchi ya kulinganishwa na SA.
Mshua amekaa mezani na Prof. Thornton toka Canada wamekata issue kwa facts. Pale haikuwa nguvu ni akili na hoja. Mpaka Barick wakatuma team nyingine kwa ajili ya majadilino; eventually jamaa walikuba wameingia chaka.
JPM amekaa chini na Airtel ambao kwa miaka 19 walikuwa hawalipi dividend na baada ya mjadala wa kutosha, jamaa wamekubali kutoa 1 bil kwa miaka 6 pamoja na kifuta jasho cha kuomba radhi 5 bil ikijumuisha Tanzania kurejea katika managerial post na kuwa na wajumbe wa bodi
Bharti Airtel to hand over Sh5.27bn today
Dar es Salaam. India-based Bharti Airtel International is to hand over Sh5.27 billion to Tanzania’s government today in part implementation of their agreement over ownership of Airtel Tanzania.
JPM aliwaondoa middle men kwenye
JPM amepunguza matumizi yasioyo ya lazima serikalini ya vikao na safari ambazo hazikua na tija. Hapo napo watu hawaoni. Walau akanunua national airline ku-facilitate travels za ndani.
Ni sisi hawa hawa tulikuwa tumechoshwa na fastjet kwa kuwa na gharama kubwa na ikiwa airline ambayo hawabadilishi ticket.
Hili nalo watu hawaoni.
Pengine, mseme mlitaka JPM atumie akili kiasi gani?
Au kuna nani ambae kama angekalia nafasi ile kama ingetokea akawa mzalendo, ilitakiwa afanye maajabu gani?
JPM kajenga PR na jirani na mtani wa jadi Kenya. Mpaka wanakamata mzigo wa dhahabu na kurejesha.
Huko nyuma Kenya iliwahi kuwa na kashfa na Goldenberg. Zote zilikuwa dhahabu zimepigwa toka Tanzania zikaingia katika mifumo rasmi ya reserve ya Kenya then zikayeyuka.
Ipo siku muda wa huyu mzee uliisha watu tutamkubuka. Muda huwa ni mwl. mzuri
La mwisho, toka zama za kale, Mungu huwa anaweka solution za matatizo/changamoto kwenye kila taifa ili na wengine tawala ziwaone. Yusuf aliwahi kutoa economic solution kwa Taifa la Misri kwa kujenga warehouse za kuhifadhi chakula kwa miaka zaidi ya14 ikijumuisha kuwa na akiba kwa mataifa jirani. Sio suala la Imani, lilikuwa suala la kimkakati kwa Misri na mpaka sasa Pyramids ambazo ni tourist destion iko on record ilijengwa na wayahudi ambao walikwenda kutafuta msosi wakasahau kurudi kwao.
Kwa kile kinachopwaya, wewe umetafuta avenue ya kushauri kimkakati nini kifanyike kwa maslahi ya Taifa au tunalaumu tu na kuwa-rate watu based on own bench mark.
Mungu wa Mbinguni tunaemwombaga kwenye nyumba za ibada na atusaidie kushukuru na kushauri kwa staha inapobidi. Kukandia na kujiona tuko intellectual yet hatujaomba japo avenue ya kutoa sulution kwa mambo ambayo ni undone, nadhani sio sawa.