Tanzania 2nd Poorest country in the world....?

sasa nini kilitokea mpaka viwanda hivyo vikatoweka?
1. Gharama kubwa za uzalishaji kwa unit moja, kwani kila kilicho zalisha lazima kilipia wachezaji wa timu za mipira wa miguu, netball, wacheza ngoma nk.
2. Ziara za viongozi kwenye viwanda, memo za zawadi
3. wafanyakazi wengi kuliko walio hitajika nk
"POOR MANAGEMENTS"
Hakuna kiwanda kilicho kuwa kikitoa faida bali viliendeshwa kwa ruzuku ya wakulima na wafanyakazi. Je unataka turudie zama HIZO
uwekezaji unafanyakazi eastern Europe bila shida, south africa nk why not Tanzania?

UBINAFSI WA VIONGOZI WA CCM
 
1. Vasco da Gama alipopitia Bagamoyo alishangazwa sana na utajiri na majengo makali ... akipita leo ataona nini? hatuna mentality ya continuity. Ulaya, Marekani, Uchina, India, nk - leo ni nchi za maendeleo hata ka vile zinaficha wamaskini wao. Mawazoni mwangu - sababu ni mzee alianza kujenga 'nyumba' ya miti, mtoto wake alianza kufyatua matofari, mjukuu wake alijenga gorofa akitumia matofari... sisi huku watoto na wajukuu wanaishi ndani ya nyumba ya udongo ilojengwa na baba/babu afu ikibomoka - tunahama na kujenga nyumba nyingine ya udongo. Sijui ni uvivu ama kutokuwa na mentality ya ku-invest kwa generation ijayo. Kwa mfano, ka viongozi wetu wangekazana kujenga mabarabara baada ya kupata uhuru - hata ka majenzi yangemalizika baada ya miaka kumi, leo tungekuwa mbali. Mazao ya mkulima yakisafirishwa kirahisi kwenda mjini ama viwandani, basi wamjini na mkulima watatajirika.

2. Tunategemea kuendelezwa na wa-nje ambao wanatuogopa tukiendelea, na pia watapoteza soko na mazao ... kwa nini watatusaidia? Mbona hatustuswi na wakina IMF ambao masharti yao watupayo tukiwa na njaa ni ya kuendeleza nchi zao badala ya zetu????? Wakati viwanda vyetu, masipitali, mashule, nk yanabomoka, wanatupa mkopo wenye masharti ya kulima mazao ya biashara...

3. Labda hewa joto inatufanya tuwe wavivu kujenga... Ulaya, kibanda kitakuwa baridi nusu ya mwaka, kwa hiyo kila generation inataka kujenga jumba zuri la kuzuia baridi... again, plan za viongozi hazionyeshi kuwa lengo urgent la ku-invest in future. Seemingly, viongozi na sisi wengi tuna mentality ya kutojali kesho ka tumbo lajazwa leo. Hatujiulizi maisha ya mjukuu yatakuwaje na tuanze kujenga nini ili wafaidike...

4. Sirikali zatufanya wananchi tuwe vipofu wakati viongozi wakiiuza nchi yetu bila sisi kunufaika. Wananchi tunahitaji kuamka na kuanza kuwauliza viongozi 'mliitumiaje?'

5. Hatuna effective tax collecting system... matajiri wanaficha pesa kirahisi tu, na wengi hawana lengo la kunufaisha ama kutajirisha nchi ... back to that mentality ya 'leo' tu, fvck 'kesho'.

6. Kuna wengi wenye mentality ya 'maintaining caste system' ... hawataki kumuendeleza mtumishi wao kwa sababu hawataki kumlipa vizuri ama kumpoteza - kwa hiyo wanamnyima... viongozi pia wana mentality hii. Mtajiri mmoja atamponda mwingine ili awe yeye tu tajiri ... hata ka kuna mali nyingi tu.

7. Rome haikujengwa kwa 'siku moja'. Sisi wengi tunataka jengo liibuke baada ya 'siku moja' ama si maendeleo afu hatuanzi kujenga... sadly, tunapima maendeleo na nchi ambazo zimekuwa na uhuru wa miaka 200, na tunataka hayo maendeleo yaibuke 'leo' bila jasho lingi. Juzi niliiona picha ya gari la zamani la jeshi la USA... lilikuwa la mbao na bila madirisha. Walianzia mbali...

8. Najua nchi yetu ni maskini... lakini kwani si dola moja yanunua vingi kwetu kuliko Marekani? Sasa hivi vipimo vya waUlaya vina-equate kwetu? $500 itanunua mengi Tz kuliko Ulaya ... ama? Tunahitaji vipimo vya maendeleo tofauti na hivi vya UN... kwa mfano, nani ana barabara nzuri, masipitali bora, nk badala ya wangapi walipwa dola 1000. Just a thought.
 
Jinchi haliendelei viongozi aka watawala na wanaofungamana nao ndio wanaoendelea, heri yangu mimi maskini akaunti zangu hazizidi milioni 25
 
CCM inastahili lawama zote!

Mkuu Pape heshima mbele,

Nadhani lawama zisipelekwe kwa Wanasiasa pekee, jee wachumi wetu wako na wanazuoni wako wapi, wanaplay vipi katika hili janga...mbali na hapo hata waandishi wa habari wako wapi....habari zote zinazopewa attention ni habari za siasa...angalia front page za magazeti yote mkuu....

Kwa nini tu masikini kiasi hiki wakati nchi yetu imesheheni vitu vya kututoa umaskinini.

Wasalaam

MJ
 
Ndio maana Pinda aliiona hii aibu ya watu kuvaa suti na kutembelea magari ya bei mbaya wakati nchi yao ni maskini wa mwisho duniani. Kama ccm haitaondolewa madarakani basi umasikini utakuwa kitambulisho cha utaifa wetu milele. Ni chama cha viongozi wavivu kufikiri na wanaiongoza nchi kwa kutumia uzoefu. Ee Mungu utukumbuke kwa kumleta mkombozi wa taifa letu.
 
Pamoja na hiyo update unayotupa haibadilishi kitu - sisi ni maskini tu na sijui tunaweza nini - maana umaskini huu niuite wakurithi, wakujitakia au wa kulaaniwa?

Mi nafikiri ni wajitakia kwa sababu ya uvivu wa kufikiria.


then tuongelee umaskini kwa kiwango tulichonacho na sio kutoa information zilizo biased ili tu ku'support 'kujisema' kwetu..
 
These statistics can be misleading and let us not be taken aback by them. I have travelled a lot and have compared Tanzania with some of the countries that are said to be better than us. Believe me Tanzania is not that worse off. And as one user has put it The data and source used by the original poster is outdated. Please check further for more recent data on poorest countries in the world by going to google.com. Zimbabwe is now said to be the poorest by the criteria of GDP. There are also a lot of politics in these categorization. do not believe in all the statistics being given....Tanzanians we can do better and let us work harder and get rid of Mafisadi...
 
Yours is outdated information. Check the link below, Tanzania ranks 152 out 182 countries in the World. Our GPP per capital is now USD 1,208.

Source: http://hdr.undp.org/en/statistics/
YOu are right, si kweli kwamba Tanzania ni ya pili kwa umaskini huo ni uongo. Tusikimbilie tu kulaum. Miaka mitatu iliyopita ilikuwa ni ya saba kwa umasikini. Mimi nafikiri imepanda sana. though hairidhishi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom