Tanzania 2nd Poorest country in the world....?

MamboJambo,

Ungefanya homework yako kwanza kabla ya kupost hii kitu!! Inaeleweka kuwa Tanzania ni maskini lakini si kwa kiwango hicho!!! Hizi data zako ni za per capita ya mwaka 2000!! Hebu nenda kwenye website ua UNDP tafuta the latest HDR uone si km unavyopotosha hapa....

Kwa kukusaidia tu angalia hapa... http://hdr.undp.org/en/media/HDR_2009_EN_Complete.pdf

Japo hizo data zinaweza kuwa outdated,cha muhimu hapa ni kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini kabisa duniani,na cha muhimu zaidi ni kwamba hatustahili kuwa katika nafasi hiyo.Hizo latest data unazotaka tuzitumie kwenye reference zinabadili ukweli gani kuhusu umasikini wetu?Kama pato la wastani mwaka 2000 lilikuwa dola 900 na sasa dola 1208 je hudhani kuwa sasa tuko katika hali mbaya zaidi kuliko tulivyokuwa mwaka 2000 (ukitilia maanani kushuka thamani kwa shilingi na vigezo vingine vya kifedha)?
 
swali kwa watanzania mnaokwenda china kutuletea takataka.KWA NINI MSIENDE KULETA MASHINE WANAZOZITUMIA????

mfano:kuna haja gani kwa mtu mzima kupanda ndege kufuata vifurushi vya suti feki wakati zinashonwa na vyerehani vya kawaida tu!na vitambaa urafiki vipo?!

si mngeenda once kuchukua hivo vyerehani then ushonaji ufanyike hapa nchini?

Ndugu hawa wanaoenda China hawana kosa lolote kwa upande wao ni mafanikio, ukiangalia profile za hawa wafnayabiashara wengi hawana elimu na wametoka mbali kweli, wengine naowafahamu walikuwa wanauza mifuko ya plastic aka rambo,kuna moja namfahamu kabsaa hata darasa la saba hajamaliza yeye kaenda mbali zaidi sasa hivi anakiwanda chake kidogo cha kutengeneza nguo china, sera za huko zinatoa fursa hiyo

Tukirudi hapa kwetu mfumo mzima ni kama haupo hata kidogo, kama watoa maamuzi wamehamua nchi iwe ya uchuuzi ufanyeje sasa, ikumbukwe multiplier effects ya viwanda kama vya nguo inaweza ikawa kubwa saana kwa uchumi wa tanzania, nani analijua hilo utasema ni waziri wa viwanda? na shaka, uwezo wa kuendelea tunao cha msingi tunatakiwa tupate viongozi vichaa kama HUGO CHAVEZ, tupelekwe mchakamchaka mpaka kieleweke, serekali inawezesha wahindi tu wanachuma na kwenda kulia India, Canada na kwingineko, wanasiasa wanalijua hilo na hata wamelibariki kabisa

Tatizo kubwa hapa ni mfumo mzima wa nchi
 
Ngoja nikupe connection yake.........! Fedha za Mafisadi, tu haziwezi kuwa na impact kny GDP kama wakizitumia hukohuko nje ya TZ......lakini wakiagiza ma VOGUE, BENZ, HUMMER & Other machinery....zikipita bandarini wanlipia kodi karibia 60% ya CIF......!

Pili, wale mafisadi wanaozidungua hapa hapa TZ, wanajenga majumba huko masaki, O/bay etc au wanafanya masherehe, au wanatanua kny viwanja vikali au wanafanya shopping za nguvu.....huko kote kuna tax implication ambayo inapitia kny vifaa vya ujenzi, mafuta, vyakula, nguo etc etc!

So kwa vyovyote vile, pesa za ufisadi zina impact kny GDP mkuu!
ameipata bila kuzalisha kodi anayotoa si zaidi ya ufisadi. anaitumia na kuishindanisha na waliozalisha kwaiyo inapandisha bei pia. akileta bidha tena inakuwa ni chini ya kiwango kwa sababu atatoa rushwa sasa mkuu hapo kuna positive impact au negative
 
MamboJambo,

Ungefanya homework yako kwanza kabla ya kupost hii kitu!! Inaeleweka kuwa Tanzania ni maskini lakini si kwa kiwango hicho!!! Hizi data zako ni za per capita ya mwaka 2000!! Hebu nenda kwenye website ua UNDP tafuta the latest HDR uone si km unavyopotosha hapa....

Kwa kukusaidia tu angalia hapa... http://hdr.undp.org/en/media/HDR_2009_EN_Complete.pdf

Does it make any difference hata kama angechukuwa data za 2020? gorrrrrrrrrrrsh.
 
With CCM in power nothing will prevail. Hii nchi inaharibiwa na CCM kwa kudharau wataalamu na kuendekeza WB na IMF, hawa ndo wanaua uchumi wa nchi nyingi maskini.

Cha msingi ni kwamba tujitahidi tufufue viwanda vyetu na kujenga vipya, bado hatuja chelewa.

Ukishakuwa na kiongozi anayeamini kuwa ili nchi yake iendelee inampasa kusafiri kila siku kwenda ng'ambo kutafuta "wawekezaji uchwara" na kuomba mikopo forget about development. Hata sijuhi rahisi huwa anaenda kuwambia nini hao wawekezaji anaowatafuta kwani hizo data zote kuhusu Tanzania tayari huwa wanazo. mfano UNDP, CIA na agency zingine nyingi zina database kibao ambazo mwekezaji anazihitaji kuhusu kuamua ni sehemu gani akawekeze mtaji wake bila hata kumsikiliza na kumuona Kikwete!! Kwetu kila kukicha raisi anaruka tu, aangalie asigeuke ndege.
 
Sishangai kabisa kwa maana kazi za production hatufanyi - viwanda tumeviua - mashamba ya mkonge, kahawa etc hakuna kitu.

Sekta ya madini ndiyo haichangii chochote tumewapa wa sauzi wanajichimbia wanabeba midhahabu makwao, hata kuvua samaki hatuwezi tumewapa wahindi wahindi wako na viwanda wanategeneza mabillion ya mihela wanapeleka makwao.

Sasa tumeamua kuwa wachuuzi - kwenda China, Dubai kuleta makolokolo na kuuziana - utaendelea vipi as a nation kama na sisi hatuwauzii wenzetu vya kwetu?

Pia tumefungua milango yote - hapo ina maana chochote kiingie thats good lakini ni hatari sana kama wewe hufanyi exportation kwa wenzako, business inakuwa one way traffic - wapi na wapi?

Taifa la wachuuzi.... ni sawa na kusign contract ya kuwa maskini milele.

Rudisheni viwanda, Fanyeni mapinduzi ya kilimo / siyo udanganyana na kilimo kwanza - aibu.

Tunaugonjwa wa "copy and paste" bila kuangalia madhara yake. Kama ulivyoiweka vizuri hatufanyi production yoyote tunakaria kukusannya vijikodi kutoka kwa wanchi wale wale waliojichokea na kuwaacha mafisadi na wale waliogenishwa (wawekezaji) wakijichotea kwa nafasi yao bila kulipa kodi.

Falsa yetu ni kuuza viwanda vyetu na kubinafisha miundombinu yote muhimu kwa visingizio vya serikali haitakiwi kujishughulisha na biashara. Cha ajabu, nenda ktk nchi nyingi zilizoendelea hadi leo serikali inamiliki viwanda na miundombinu muhimu! kuna serikali zinatoa social service kama education na healthcare free. Serikali zilizo nyingi bado zinasupport kilimo including EU ambayo inatoa karibia 50% ya matumiza yake kwenye farm subsidies. Kwetu tunaimba "kilimo kwanza" ili kuwanufaisha mafisadi wa wadoshi wao.
Nenda China uone ukiritimba uliopo na ndo maana wanaendelea, falsa yao ni iba technologia yoyote nzuri kwa maslahi ya China, lakini kwao mtu hurusiwi kutoa technolojia nzuri ya China nje ya China.
Nenda Japani, kama nchi wana agency kwa ajili ya kusaidia viwanda na makampuni yao kupata biashara nje. Agency kama METI http://www.meti.go.jp/english/ . mifano ni mingi kwa UK, USA, Korea nk.
Serikali na viongozi wetu wanaangalia wao watapata nini ni si nchi itafaidika vipi?
Naamini kwa viongozi na policy tulizonazo kama zipo kina Kikwete , Karamagi, Ngereja, Kawambwa, Marsha, Mkuro, tusahau maendeleo kwa Tanzania
 
hata vyerehani vinahitaji sayansi ambayo watanzania hatuna?!!mashine zipo simple na complicated..,tatizo mayakkhe sie hatutazami hilo.
kuna viwanda vingi sana vilikuwepo kabla ya kuuliwa na management mbovu,si chini ya 500.Tuanza na hivi kwanza..,

kwa nini General tyre ife?!wakati idadi ya magari TZ inazishinda manispaa ku-control traffic?

kwa nini kiwanda cha smenti kishindwe kushindana wakati nchi ina uhaba wa zahanati,makazi bora na huduma lukuki za afya?

kwa nini tusiwe hata na viwanda vya ku-assemble simu za mkononi wakati tunaongoza kwa matumizi yake barani africa?!

we do not play to our advantages!!

Kimweri,

The devil is in details. Kuna Magari mengi sana kwa nini general tyre ife watanzania tuishie ku-ride on second hand tyres? Ni swali zuri sana. Watanzania wanavaa nguo wote million arobaini kwa nini Mwatex ife? Kwa nini Mutex, Kiltex iwe historia?

Tatizo ni nani anamiliki General Tyre? Ni nani anaendesha General Tyre? General tyre inahitaji nini kufanikiwa? Ni nani atahakikisha vitu hivyo vinapatikana? Umeme wa kutosha, Raw materials, technology, etc....!!!! Viwanda vyetu tuliviendesha kama vya wakoloni. Tukawa tunaiba at every opportunity na serikali ikawa inatusaidia kuiba zaidi kwa kuweka management miungu ambao hawahojiwi na yeyote. Kiwanda kikifa wanasema tumekosa masoko ...... full stop .... Wanahamishiwa kiwanda kingine!!!!
 
Viwanda kumilikiwa na serikali kwa hatua tuliyofikia Tanzania itakuwa kama mchezo wa kuigiza. Yanakufa mashirika yenye ukiritimba ambayo hayashindani na yeyote (Angalia hali ya Tanesco, TRL, Bandari, n.k.) vyote ni vijiwe vya wezi waliokubuhu. Kusema tufanye attempt nyingine ya kuanzisha viwanda ni kuota ndoto za mchana. Hatuwezi chochote tuko dhofu hohe hahe. Hata mashirika kama NSSF, PPF, PSPF, ambayo kazi yake kukusanya tu fedha kinachoendelea huko ni kizungumkuti. Kwa kifupi hatuwezi kuendesha kitu chochote efficiently angalia benki kuu ilivyo kijiwe cha warafi!!!

Haki yetu itakuwa ni kufugwa kama Twiga wa Serengeti alisema mwalimu. Haya maresources tunayoyazungumzia kila siku wenyewe walishayachukua. Sisi itabbaki kuimba tuu; kuna dhahabu, Mbuga za wanyama, Mabonde, Bahari, n.k. Ukweli hivyo vitu si vyetu ni mali ya viongozi wanaoongoza nchi na mabwana zao waliowaweka madarakani. Kwani tunaweza kuchagua? Subutu, hiyo kura yako ataihesabu nani?

Tusubiri nchi zetu zilizochoka zitakuwa zinawekwa chini ya ulinzi tena yakitokea majanga. Haiti sasa hivi hadi ikulu imetwaliwa na wamarekani. Niambie hali ya baadaye ... kutakuwa na nchi inayoitwa Haiti tena? Labda kijiographia itabaki kwenye ramani.

Hiyo ndo fate ya maskini wote. Maskini wenye resources kama sisi ndo usiseme.
 
Sishangai kabisa kwa maana kazi za production hatufanyi - viwanda tumeviua - mashamba ya mkonge, kahawa etc hakuna kitu.

Sekta ya madini ndiyo haichangii chochote tumewapa wa sauzi wanajichimbia wanabeba midhahabu makwao, hata kuvua samaki hatuwezi tumewapa wahindi wahindi wako na viwanda wanategeneza mabillion ya mihela wanapeleka makwao.

Sasa tumeamua kuwa wachuuzi - kwenda China, Dubai kuleta makolokolo na kuuziana - utaendelea vipi as a nation kama na sisi hatuwauzii wenzetu vya kwetu?

Pia tumefungua milango yote - hapo ina maana chochote kiingie thats good lakini ni hatari sana kama wewe hufanyi exportation kwa wenzako, business inakuwa one way traffic - wapi na wapi?

Taifa la wachuuzi.... ni sawa na kusign contract ya kuwa maskini milele.

Rudisheni viwanda, Fanyeni mapinduzi ya kilimo / siyo udanganyana na kilimo kwanza - aibu.

This is great idea to industrialize our nation, sio dhahabu itoke tz halafu final product , import from china, we need to make our own. One day I talked with my friend claims that our economy has grown because previous president proud that Hazina is now full of money from collections, I told him to me I see it in a negative way, that supporse if all hawa baberu weupe wakiondoka will we able to bring collections given that we have killed all the industries and we dont have capable skill persons to run factories that will produce competative product in the market, can we survive? Jamaa aliniona mimi si mpendi Rais wetu, but fact is how much is contributaed by foreners and locals, bear is owned by makaburu, migodi makaburu, canadians, which then wanaleta hata mchicha kutoka kwao, ukiangalia proposal za project zao utakuta wanasema itasaidia ukuaji wa kipato cha locals, how ? Inauma, vijana tulio nje turudini tukafanya mabadiliko kwa exposure tulizo nazo, tuache maneno kama tunaipenda nchi yetu.

Sifa ya kijana si kulalamika ni kutenda, ukiona kijana ni mlalamikaji jua anakasoro. Wake up vijana wazungu wanatucheka wakisikia tunakimbilia ulaya wakati wao wanaona kunavitu vingi vyakufanya TZ!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wabeba maboksi wengi have nothing to come home to. They work like donkeys, too many bills and little to no savings. They can't afford to come back home.
 
Yawezekana sielewi;

a. Ni kitu gani tunazalisha sana na kuuza nje?
b. Ukiondoa mchango wa Madini kwenye exports yetu, madini yanasaidia vipi watanzania wengine (ambao hawako karibu na maeneo ya madini)?
c. NI vitu gani tunavyozalisha ndani ambavyo sisi wenyewe ni walaji wake wakubwa?
d. Corruption inaathiri vipi GDP na GNP ya nchi yetu?
 
Yawezekana sielewi;

a. Ni kitu gani tunazalisha sana na kuuza nje?

Labda nione kama nipo sahihi.

Ktk uelewa wangu finyu wa mambo ya uchumi, inalaazim kuweka uwiano kati ya import na export. Kama tuna-import sana hiyo ni hasara kwetu kwa sababu ya mambo ya thamani ya fedha, kuuwa manufactors na processors wa ndani etc. ambayo inayo taathira hadi kwenye ajira.

Suala la lingine ni shurti kuongeza thamani ya kile unachouza nje. Bila hivyo watu wako wanakosa ajira, fursa za kibiashara zinapotea na return inayopatikana inakuwa finyu kutokana na unit price yenyewe ya kitu kilicho raw kuwa chini.

BTW, sijasoma statistics za karibuni, lakini najua mazao ya miti, mazao kama chai, utalii na madini ndio vinara kwa kuingiza foreign curency.
 
Umeeleza vizuri sana mkuu. Ila bado hatujajua tatizo liko wapi? Tatizo kubwa ni ''mindset'' za Watanzania wote, wasomi na wasiosoma, viongozi na raia wake. Yaani utandawazi umeliangamiza kabisa taifa. Uko wapi utamaduni wetu?

Mfano; wenye mashindano ya Miss Tanzania ya mwaka jana kauli mbiu ilikuwa ni kukuza utalii wa ndani! Cha ajabu hakuna kikundi chochote cha ngoma za kienyeji kilipewa nafasi ya kutoa burudani pale. Walijaa wasanii wa Bongo Flava. Hivi mtalii anahitaji kusikiliza ''hip hop'' ya Tanzania? Halafu eti kukawa na show ya Michael Jackson. Double standards everywhere, utalii wa ndani na show za Michael Jackson, nyimbo za hip hop wapi na wapi?

Tujadili kiini cha tatizo! Tatizo liko kwenye fikra zetu! Tubadilike!

Fikra za kitanzania zimejengwa na ulezi wa CCM. CCM ibadilike, ikabadilika tu na ndipo wataanza kujiwajibisha na kampeni za kubadili watu. Kila kitu kinahitaji uongozi, hata kubadilika kwa tabia ya jumuia. Tukisema tu 'TUBADILIKE' bila ya kumwajibisha yeyote inaashiria kua tuna power vacuum.
 
Yawezekana sielewi;

b. Ukiondoa mchango wa Madini kwenye exports yetu, madini yanasaidia vipi watanzania wengine (ambao hawako karibu na maeneo ya madini)?
Pato lake linaingizwa kwenye kapu la Taifa.
c. NI vitu gani tunavyozalisha ndani ambavyo sisi wenyewe ni walaji wake wakubwa?
Maji ya Azam na Beer za TBL na Serengeti B.L
d. Corruption inaathiri vipi GDP na GNP ya nchi yetu?
Fedha ambazo zinastahili kutumiwa na wananchi kuboresha maendeleo yao inaishia kwa watu wachache, na mbaya zaidi kama itawekwa kwenye bank za nje ya Tanzania, Swali zuri mkuu linamfaa Beno Ndulu.
 
Back
Top Bottom