Tanroads Lindi yarejesha mawasiliano barabara ya Kilwa Masoko-Nangurukuru-Liwale

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
710
861
TANROADS LINDI YAREJESHA MAWASILIANO BARABARA YA KILWA MASOKO-NANGURUKURU-LIWALE

Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Lindi umefanikiwa kurejesha mawasiliano yaliyokuwa yamekatika kati ya Kilwa Masoko-Nangurukulu wilaya ya Kilwa na wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Mawasiliano hayo yamereshwa ndani ya saa 24 kupitia kazi iliyofanyika usiku na mchana hadi kuhakikisha daraja la muda katika mto Zinga ambao unatenganisha kijiji cha Zinga na Miguruwe linatengamaa ili shughuli za usafirishaji wa abiria na mazao ya chakula na biashara ziweze kuendelea.

Daraja hilo lilisombwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo uliosababishwa na kimbunga Hidaya kilichotokea Mei 3 na 4, 2024 katika mkoa wa Lindi na Mtwara.

Kurejea kwa mawasiliano hayo ni kama kurudisha matumaini ambayo watu walikuwa wameyapoteza kwani hiyo ndiyo njia pekee waliyokuwa wakiitegemea kufikisha mazao yao sokoni na hata bidhaa za kutumia majumbani.

Meneja wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Emil Zengo amesema kimbunga hidaya kilipopita maji yaliongezeka wingi na kasi kiasi cha kupita juu ya daraja hilo.

“Daraja hili liliweza kusukumwa kabisa, kusogea pembeni na kuta zake kubomolewa, kimbunga hiki ndiyo pia kilisababisha athari katika maeneo mengine pia ya barabara zetu ambayo ni barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kuja Lindi hadi Mtwara,” amekaririwa Mhandisi Zengo

Kwa sasa eneo hilo limekamilika na barabara ya kutoka Liwale hadi Nangurukulu inapitika huku matengenezo madogo madogo katika baadhi ya maeneo yakiendelea kufanyika ili wananchi waweze kupita na kufurahia uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita.

Mbali na daraja hilo, kimbunga Hidaya kilipopita nchini, pia kilisababisha zaidi
ya madaraja manne kukatika yakiwamo ya Somanga, Songas, Mikereng'ende, na la Mto Matandu, huku baadhi ya vijiji vikizingirwa na maji.

Baadhi ya wananchi wameeleza furaha yao juu ya kurejea kwa mawasiliano huku wakielezea adha waliyokuwa wakiipata awali ikiwemo kukosa mahitaji muhimu.

Kwa nyakati tofauti walipotoa maoni yao waliishurukuru Serikali kwa kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

Mary Mwela mkazi wa Miguruwe, Mwajuma Kassim Kibweku mkazi wa Miguruwe na Mjumbe wa Serikali ya kijiji, Fadhil Hemed Ngulile mkazi wa Miguruwe, Nurdin Maiki diwani wa kata ya Njinjo, Abdul Sadick dereva wa basi, Hemed Kingwande mwenyekiti kijiji cha Miguruwe wametoa shukrani zao kwa Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za dharula kwa ajili ya kurejesha mawasiliano ya barabara.

Kwa upande wake Msimamizi wa barabara ya Kilwa Masoko-Nangurukuru-Liwale Mhandisi Anna Nnko amesema Mbali na daraja hilo pia ipo sehemu ya barabara hiyo ilimegwa na maji yaliyosababishwa na mvua kubwa za El-Nino zilizokuwa zikinyesha jambo ambalo lilifanya TANROADS kulazimika kuihamishia upande mwingine ili shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea.

MWISHO.

IMG-20240522-WA0017(1).jpg
IMG-20240522-WA0007(1).jpg
 
Namna ile ndio kurudisha mawasiliano..? Ikinyesha lisaa moja ni balaa zaidi ya ile..pia barabara zina mahandaki makubwa sana pembezoni.
 
Hiyo picha ya kwanza mwanaume kapiga rangi kucha, huyo wa pili sijui hana mke,,,mpaka kazini kitu hakijalegea
 
Namna ile ndio kurudisha mawasiliano..? Ikinyesha lisaa moja ni balaa zaidi ya ile..pia barabara zina mahandaki makubwa sana pembezoni.
Wanaita emergency plan maana lazima mawasiliano yawepo hata kama kwa muda ndio maana unaona kuna Culvets zimefukiwa hapo chini kuruhusu maji kupiła japo kurejesha mawasiliano wakati wakijipanga kujenga daraja (structure) la kudumu eneo husika.
 
TOKA MAKTABA:
05 May 2024

TANROADS RUVUMA YAFANYA UKARABATI MKUBWA MIUNDOMBINU KATIKA DARAJA LA MUHUWESI WILAYANI TUNDURU

1716382020546.png

Na Mwandishi Maalum Ruvuma

WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Ruvuma, imekamilisha kazi ya kuimarisha daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru ambalo liliathirika na mvua za masika na kusababisha taaruki kwa watumiaji wa daraja hilo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=FEgteyhTaMQ
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Saleh Juma alisema, kwa sasa daraja hilo ni salama na haliwezi kusogea tena kama ilivyotokea hapo awali, na amewatoa hofu watumiaji hasa wenye magari kuhusu uimara wa daraja hilo linalounganisha mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.

1716381943651.png


Aidha alitaja kazi nyingine zilizofanyika, ni kuziba mashimo makubwa kwenye barabara inayoingia katika daraja hilo yaliyosababishwa na maji ya mvua kupita chini ya barabara na kukatika kwa sehemu ya lami

Daraja jipya la Muhuwesi lenye uzito wa zaidi ya tani 1,000 lilivyosukumwa na kuhamishwa na nguvu ya mto Muhuwesi


View: https://m.youtube.com/watch?v=QKPSCVAeD04

Serikali yatoa zaidi ya Bilioni 1 kufanya Marekebisho Daraja la Muhuwesi Tunduru likosegezwa na nguvu ya maji ya mto Muhuwesi mnamo mwezi February 2022 lina urefu wa mita 40 na kusifika kuwa mojawapo ya madaraja imara hadi hapo 2022 lilopopata changamoto ni njia muhimu kuunganisha mikoa ya Lindi Mtwara, Ruvuma, Njombe kuelekea Iringa hadi mikoa ya Pwani na Dar es Salaam

2016 DARAJA LA ZAMANI KATIKA MTO MUHUWESI TUNDURU LILILOBOMOLEWA NA TANROADS

1716381910128.png
 
Hiyo picha ya kwanza mwanaume kapiga rangi kucha, huyo wa pili sijui hana mke,,,mpaka kazini kitu hakijalegea
Watu mna eagle eyes. Mngekuwa weledi hivi kuchunguza wapi fursa halali za kiuchumi zinapatikana na pia kufanya kazi kwa kujituma tungekuwa
 
Back
Top Bottom