TANROADS: Barabara ya njia nne (Bukoba) yenye urefu wa Kilometa 1.6 iliyoanza kujengwa 2023 kukamilika Novemba 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Ntuli amesema kwamba ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara njia Nne Bukoba kutoka Rwamishenye hadi Makutano ya barabara ya stendi ya mabasi Mkoani Kagera unatarajiwa kukamilika Mwezi November 15/2025.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya, amesema kuwa ujenzi huo ulikwama kwa muda hali iliyozua maswali mengi kutoka kwa wananchi.

“Wananchi wamekuwa na maswali pengine ya sintofahamu ni lini Barabara hii itakuwa tayari kwa matumizi ila sisi kama Tanroad) hatujalala kazi inaendelea na hapa tunaendelea ukarabati wa daraja Letu la kanoni ili turahisishe kazi,amesema Mwaikokesya "

Ujenzi huo wa barabara Rwamishenye hadi Makutano ya barabara ya stendi ya mabasi una urefu wa kilomita 1.6.
photo_2025-05-01_13-05-46.jpg
Akiwa kwenye ziara ya kikazi Machi 28, 2024 kukagua ujenzi wa miundombinu ya barabara Mkoani humo Kagera, Waziri wa Ujenzi alisema kuwa Serikali ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.64 kuanza ujenzi wa wa barabara hiyo kwa kipande cha kilometa 1 ambacho kinaanzia Rwamishenye hadi eneo la Mitaga ambapo kwa wakati huo utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 25.

Aliongeza kuwa Serikali iliongeza kiasi cha shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kipande cha mita 600 kuanzia eneo la Mitaga hadi stendi na ujenzi wa daraja kubwa mto Kanoni.

Hata hivyo kwa mujibu wa TANROADS - Kagera awali ilieleza kwamba mkataba wa ujenzi wa kipande cha kilometa 1 ambacho kinaanzia Rwamishenye hadi Mitaga, chini ya Mkandarasi M/s Abemulo Contractors Ltd utakuwa wa miezi 12 kuanzia Oktoba 9, 2023.

Kutokana na kipande hicho kutokamilika hadi sasa Mei 2025, kumekuwepo na malalamiko ya wananchi na wadau kuhoji sababu ambazo zimepelekea kipande hicho kuchelewa kukamilika kwa wakati hali ambayo inadaiwa kupelekea usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo.

Sanjari na hayo, kuhusu uwezekano wa kujenga daraja mbadala kwa ajili dharura eneo la mto kanoni ambako ujenzi unaendelea kwa sasa, Mhandisi Mwaikokesya ameeleza kuwa hilo halipo katika mkataba wa ujenzi hivyo kwa sasa, wananchi wataendelea kutumia njia ya kuzunguka kupitia Nyakanyasi, Kashura pamoja na Kashozi Road ili kuingia eneo la Mji.

Pia soma ~ Ujenzi wa Njia Nne Bukoba unasuasua, Mamlaka hazifahamu barabara hiyo ndio mlango wa uchumi wa Mji?
 
1.6km au 16km au 160km? Embu mtoa mada clarify?
 
Huo mkoa tangu wamshangilie Idd Amin kwamba bora kaja kuwachukua, una laana, wanajenga kilometa nne miaka miwili, soko walipewa fedha miaka kumi iliyopita hawajajenga, stendi walipewa fedha kabla hata ya Ubungo na Nyegezi na Morogoro, mpaka leo bado
 
chichiemu
 
Mkandarasi kalipwa fedha..... Amepaki malori yake tu kule katoma
nani anasimamia? --- unamaanisha serikali kazi yake ni kutoa hela alafu haifatilii?
 
takataka tupu
 
Huo mkoa tangu wamshangilie Idd Amin kwamba bora kaja kuwachukua, una laana, wanajenga kilometa nne miaka miwili, soko walipewa fedha miaka kumi iliyopita hawajajenga, stendi walipewa fedha kabla hata ya Ubungo na Nyegezi na Morogoro, mpaka leo bado
Mkuu, sisi CCM tunakubaliana katika utofauti wa mawazo ili mradi tu iwe katika kujenga. Mimi ni Mhaya. Hivi ni kweli kuna Mhaya yeyote aliwahi kusema ni afadhali awe chini ya Idd Amin kuliko kuwa chini ya Mwl. Nyerere? Ushahidi please!
 
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Ntuli amesema kwamba ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara njia Nne Bukoba kutoka Rwamishenye hadi Makutano ya barabara ya stendi ya mabasi Mkoani Kagera unatarajiwa kukamilika Mwezi November 15/2025.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya, amesema kuwa ujenzi huo ulikwama kwa muda hali iliyozua maswali mengi kutoka kwa wananchi.

“Wananchi wamekuwa na maswali pengine ya sintofahamu ni lini Barabara hii itakuwa tayari kwa matumizi ila sisi kama Tanroad) hatujalala kazi inaendelea na hapa tunaendelea ukarabati wa daraja Letu la kanoni ili turahisishe kazi,amesema Mwaikokesya "

Ujenzi huo wa barabara Rwamishenye hadi Makutano ya barabara ya stendi ya mabasi una urefu wa kilomita 1.6.
Akiwa kwenye ziara ya kikazi Machi 28, 2024 kukagua ujenzi wa miundombinu ya barabara Mkoani humo Kagera, Waziri wa Ujenzi alisema kuwa Serikali ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 4.64 kuanza ujenzi wa wa barabara hiyo kwa kipande cha kilometa 1 ambacho kinaanzia Rwamishenye hadi eneo la Mitaga ambapo kwa wakati huo utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 25.

Aliongeza kuwa Serikali iliongeza kiasi cha shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kipande cha mita 600 kuanzia eneo la Mitaga hadi stendi na ujenzi wa daraja kubwa mto Kanoni.

Hata hivyo kwa mujibu wa TANROADS - Kagera awali ilieleza kwamba mkataba wa ujenzi wa kipande cha kilometa 1 ambacho kinaanzia Rwamishenye hadi Mitaga, chini ya Mkandarasi M/s Abemulo Contractors Ltd utakuwa wa miezi 12 kuanzia Oktoba 9, 2023.

Kutokana na kipande hicho kutokamilika hadi sasa Mei 2025, kumekuwepo na malalamiko ya wananchi na wadau kuhoji sababu ambazo zimepelekea kipande hicho kuchelewa kukamilika kwa wakati hali ambayo inadaiwa kupelekea usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo.

Sanjari na hayo, kuhusu uwezekano wa kujenga daraja mbadala kwa ajili dharura eneo la mto kanoni ambako ujenzi unaendelea kwa sasa, Mhandisi Mwaikokesya ameeleza kuwa hilo halipo katika mkataba wa ujenzi hivyo kwa sasa, wananchi wataendelea kutumia njia ya kuzunguka kupitia Nyakanyasi, Kashura pamoja na Kashozi Road ili kuingia eneo la Mji.

Pia soma ~ Ujenzi wa Njia Nne Bukoba unasuasua, Mamlaka hazifahamu barabara hiyo ndio mlango wa uchumi wa Mji?
Mtoa mada, hivi huna habari kuwa serikali haipeleki fedha TANROADS?
 
Back
Top Bottom