imepita wiki sasa tangu aniombe namba ya simu. Ni kijana mnadhifu sana, tulikutana kwenye gari nikiwa natoka kazini na kwa bahati mbaya tulikaa siti moja. Aliniongelesha sana mpaka nikatoa namba yangu ya simu. Tangu hapo amekuwa msumbufu kila wakati anapiga simu mpaka saa8 za usiku. Kwa kweli nimetokea kumchukia sana japo hataki kuelewa kuwa simtaki. Imefika stage nimeblock namba yake ila ameamua kutumia lain nyingine. Naombeni ushauri nimfanyeje huyu mwanaume?