Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,508
- 113,629
Wanabodi,
Hiki ni kisa cha kufikirika tuu lakini ni kisa cha kweli na ni cha ajabu kweli, ila ndio ukweli wenyewe kwa kitakachotokea kwenye ndoa ya wawili hawa!.
Kwa hapa Tanzania, kwa kawaida tuna aina mbili kuu za ndoa, yaani type ya ndoa, ni tuna ndoa ya mke mmoja, na ndoa za wake wengi, halafu kwenye form ya ndoa, tuna aina 4, ndoa za kidini, ndoa za kisekali, ndoa za kimila, na ndoa za dhana ya ndoa, yaani presumption of marriage, hii ni ndoa ambayo watu wamechukuana tuu na kuishi pamoja bila kufunga rasmi ndoa.
Ndoa yetu ninayoizungumza kwenye muktadha huu, ni ndoa ya watu wawili wamependana wenyewe na ridhaa zao wenyewe wakaamua kuingia kwenye mahusiano rasmi ya ndoa ya mke mmoja mume mmoja, ambao walipaswa kuishi nyumba moja, nyumba ya ndoa.
Lakini wawili hawa waliamua kufunga ndoa ya ajabu kidogo!. Walifunga ndoa ya mke mmoja mume mmoja na kuishi nyumba moja kwa mwanamume. Mke au mume utaachana na wazazi wako, utaandamana na mumeo/mkeo, mtakuwa mwili mmoja!.
Kwa ndoa hii wakaamua ni ndoa ya mke mmoja ila nyumba mbili, ndani ya nyumba ya mume, ni ndoa ya mke mmoja, mume mmoja nyumba moja. Lakini mke akapewa uhuru, kule kwao, akawa ana nyumba yake na ana uhuru wa kujiamulia mambo yake madogo madogo ya kule ndani kwake. Hivyo ndoa yetu hii ni ndoa ya mke mmoja nyumba mbili!, nyumba moja ni ndoa ya mke mbili, nyumba moja ni ndoa ya mke mmoja halafu kule upande pili ni ndoa ya mitala!.
Wakati ndoa hiyo ikiendelea mke mke akiwa nyumba kuu ni mke mwema, mke mmoka mume mmoja, nyumba moja, ila akiwa kule kwao kwenye nyumba ya pili, kwa vile kule mke anao uhuru wake, kule akaanza kuutumia vibaya uhuru huo kwa kutoka nje ndoa hiyo, mume akagundua, mkewe akiwa kwao, huwa anatoka nje ya ndoa!, lakini kwa vile anampenda sana mkewe sio tuu hata kumkanya alishindwa hata kumuuliza tuu alishindwa kwa kwa kuhofia asije akamuuliza mke akakasirika na akadai talaka yake!, mume akaona kuliko kumuuliza na kuhatarisha ndoa ni bora ajikalie kimya avumilie!.
Licha ya mume kumtimizia mkewe mahitaji yake yote ya huku na kule, ikiwemo kumpa kila kitu alichokitaka, sasa mke anataka uhuru zaidi!, ile kujiiba na kutembea nje ya ndoa bila kuulizwa, sasa anataka ihalalishwe, mke apewe uhuru rasmi wa kutembea na yeyote anayemtaka zile siku akiwa kule kwake sio kwa kujiiba iba, iwe wazi kihalali!.
Ndoa hii ni muungano wetu, ndani ya muungano kimataifa ni muungano wa union wa nchi moja ya JMT, yenye serikali moja (nyumba) ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT. Wanandoa Tanganyika na Zanzibar, kila mmoja amawaacha baba yake na mama yake, na kuandamana na mwenzake kuunda JMT ambayo ni nchi moja.
Lakini kitaifa, nje ya muungano, muungano wetu ni federation, wenye nchi mbili, Tanzania bara na Tanzania wisiwani, au Tanzania Zanzibar, zenye serikali mbili ya JMT na SMZ, zenye marais 2, Rais wa JMT na rais wa Zanzibar!.
Mwaka 2010 Zanzibar ilibadili katiba yake na kutoka nje ya ndoa ya JMT, ina bendera yake, wimbo wake wa taifa, sasa inataka uhuru zaidi wa kujifanyia mambo ya kimataifa kama kujiunga OIC!.
Mshenga wa mgogoro huu wa ndoa, hiii Jaji Joseph Warioba, ameshauri uhuru huu kwa mke, utolewe!, badala ya kuendeleza ndoa ya mke mmoja, mume mmoja nyumba moja, ameshauri, kufuatia mke kuamua kwa dhati, kutaka uhuru zaidi hadi wa kutembea nje ya ndoa!, njia pekee ya kuinusuru ndoa hii, ni kumpa huyo mke uhuru zaidi, kwa kumruhusu aishi kwa uhuru zaidi, badala ya ndoa ya mke mmoja mume mmoja, nyumba moja, ndoo hii ikubaliwe kuwa ni ndoa ya mke mmoja, mume mmoja nyumba tatu!, ila kila mtu kuishi kwenye nyumba yake kwa uhuru, ila pia iwepo nyumba ya tatu ya ndoa ambayo mke na mume, watakutania hamu, ile siku watakapo hitaji kutimiza hitaji la ndoa!.
Jee ungekuwa wewe, ungekubali?!.
Kama unaamini kwenye ndoa ya mke mmoja mume mmoja nyumba moja!, pigania serikali moja!.
Kama unaamini kwenye ndoa ya mke mmoja mume mmoja nyumba mbili kama hivyi ilivyo sasa kwa kila mtu na haki zake kwa nyumba ya watu wawili, pigania serikali mbili!.
Lakini kama unakubali na ndoa ya mke mmoja, mume mmoja nyumba tatu ili kila mmoja awe huru, na mke awe na uhuru wa kutembea nje ya ndoa!, unga mkono serikali tatu!.
Baada ya kumsikia Jaji Warioba leo, akitoa sababu za Tume yake kupendekeza serikali tatu!, kumbe nia ni ili kumpa uhuru zaidi mke, afanye anachotaka, hadi kutembea nje, bila kuivunja ndoa!.
Mungu Ibariki Tanzania!.
Muungano Milele na utalindwa kwa gharama yoyote!.
Paskali