Tangazo la ''tuko wangapi?''

NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
863
407
Wadau,
Kuna hili tangazo la 'tuko wangapi' ambalo linarushwa kwenye vituo vya Radio na Tv sasa. Nataka kulizungumzia hili ambalo linarushwa kwenye Tv. Kwa kweli kwa maadili ninaona si sawa kwa namna ya jinsi lilivyo,hususani ukilitazama lile ambalo linaonesha watu wapo chumbani. Na linarushwa wakati ambao watu wengi wanakuwa na familia zao na wanatazama television. Yaani wakati ambao watoto wanajumuika na wazazi. Ukitazama hata ubora wa tangazo sijauona,kwa sababu ni tangazo ambalo dhumuni lake ni zuri lakini kwa namna ilivyotumika kufikisha ujumbe ni mbovu sana. Jaribu kutazama pale linapoonesha watu wakishikana miili(wanawake kwa wanaume),je mnaona ni sawa? Najua wengine watadai kuwa kizazi cha sasa kinajua kila kitu,lakini hata kama watoto wa sasa wanajua kila kitu tusiruhusu kila jambo kuwa wazi.
Ninatoa sifa ya wale waliotengeneza tangazo linaloruka kwenye Radio,kwani ujumbe wake upo wazi kabisa.
 
Mh! Mi naona we ni Kati ya wale ambao neno "tupo wangapi" linawakera sana!
 
Acha kuficha mambo, watoto wa siku hizi sio ksma wa zamani ambao walikua wakiambiwa mama yko alikununua.
Watoto wa siku izi wakimuona mama mjamzito wanajua amepataje.

Na muache kuwaambia ukikojolea kolani unageuka mjusi.
 
Ukilisema hilo je ambalo linawaonyesha wasichana na vitu vyao vya kutumia kila mwezi

Maana ile hadi jinsi ya kuvaa unaonyeshwa.

Kwahyo kwa siku hizi ni kawaida tu
 
wakati sisi huku tunahangaika kuboresha maadili yetu watu huko ulaya wanahangaika kutawala dunia!! Tutaweza kweli kuwafikia wazungu maendeleo yao kamatukizidi kupoteza muda wetu kuangalia na kuchunguza upuuzi huo!! shida wengine wanawaza tu ngono kilawakati, kilamuda!!
 
hamna ubaya wowote,
tena habari za tupo wangapi na zaidi ya hizo zinazohusu ngono salama, ngono zembe, magonjwa ya zinaa, mapenzi na ngono, inabidi zielezwe wazi wazi kwa watoto kutoka kwa wazazi wao ili wapate taarifa sahihi kuliko kujifanya unajua maadili af wanao wanaenda kuelezwa taarifa zihusuzo ngono/mapenzi zisizo za kweli vijiweni..
 
Huwa nabadilisha channel linapoanza tu!! Yaani siwaelewi hawa waliolitengeneza, tangazo lenyewe ni nadharia tu!! Hivi kweli yanaweza kutokea hayo kiuhalisia? Mtu hata kama ana wapenzi wengi huwa anaficha si kama lilivyo hilo tangazo. Aliyelitengeneza sijui aliwaza nini!!! Labda anataka kuwafundisha vijana wafanye hivyo!!
 
Mnabisha bure. Tangazo hilo ni baya hata kama kizazi cha sasa kinajua kila kitu sio kila kitu kinawekwa wazi kiasi hicho bana
 
Tuache ushabiki wa kijinga, achilia mbali watoto je ndo umekaa na Mkweo au mtu unayemuheshimu mnasubiri taarifa ya habari halafu kanakuja hako kakitu cha watu kutomasana kitandani utajisikiaje kama sio kutamani kutoka sitingroom? Hili ni zuri endapo Mr and Mrs mna Tv ya Bedroom ili muambizane Vizuri "TULIZANA". Bora lile la Gari kubomoka na lile la hotelini.
 
Back
Top Bottom