Tangazo: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943




UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

Academic Staff Assembly



JUMUIYA YA WANATAALUMA CHUO KIKUU CHA
DAR ES SALAAM (UDASA)
inawaletea:
KONGAMANO LA KATIBA


MADA KUU: MCHAKATO NA MAUDHUI YA KATIBA MPYA


WAZUNGUMZAJI WAKUU:
1. PROFESA ISSA SHIVJI
2. NDG JENERALI ULIMWENGU

TAREHE: JUMAMOSI, 15 JANUARI 2011
UKUMBI: NKRUMAH, CHUO KIKUU CHA DSM
MUDA: SAA 4:00 ASUBUHI HADI SAA 8:00 MCHANA


WOTE MNAKARIBISHWA
 
Nitafika bila kukosa...Mada ni nzuri na wato mada nao wako safi..Tuje na Nakala za Katiba zetu au tutapewa kwenye Kongamano hilo?
 
kwa sisi tuliombali na dar es salaam, tunaomba kongamano hilo lirushwe na Mlimani TV. Asante.
 
Mimi sio mwanataaluma nimfanya biashara tu hapa kariakoo, vipi naweza hudhuria?
 
Dk. Tunashukuru kwa taarifa, watu wanamwamko wa kutosha na wasiwasi wangu ni Ukumbi wa Mkurumah hautatosha maana wanachuo watakuwa wengi na raia wa kawaida na watakuwepo, Je makadirio ya watu yakoje?
 
Huu ni mwanzo mzuri; natumaini taasisi nyingine za kijamii nazo zitaaanza kuzungumzia suala hili la Kikatiba.
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Katiba: Jumamosi, 15 Januari 2011 Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha DSM

Jumuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) imeandaa Kongamano la Katiba litakalofanyika katika ukumbi wa Nkrumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku ya Jumamosi, tarehe 15 Januari 2011 kuanzia saa 4 asubuhi. Mada kuu katika kongamano hili ni: Haja, Maudhui na Mchakato wa Katiba Mpya.
Katika siku za karibuni wadau wengi wa demokrasia na maendeleo katika nchi yetu wamekuwa wakitoa wito wa kuandikwa upya kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, kumekuwa na kusigana juu ya mchakato unaofaa kufuatwa katika kufikia katiba mpya. Vilevile, wananchi wengi wamekuwa wakihoji nini hasa matatizo ya katiba iliyopo na maudhui gani yawekwe katika katiba mpya. Hivyo basi, lengo kuu la kongamano hili ni kutoa fursa kwa wananchi kuelewa misingi mikuu ya Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutafakari kwa kina haja, maudhui na mchakato wa kupata katiba mpya.
Katika kufikia lengo hili, UDASA imewaomba na wamekubali wananchi wawili waliobobea na wenye uzoefu wa muda wa kupigania demokrasia ili wawe wazungamzaji wakuu. Wananchi hawa ni Profesa Issa Shivji wa Kigoda cha Mwalimu cha Taaluma za Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ndugu Jenerali Ulimwengu wa Raia Mwema. Wote hawa wanafanana kwa jambo moja nalo ni ukweli kwamba wametumia zaidi ya nusu ya maisha yao katika kupigania haki za wanyonge Tanzania na katika bara la Afrika kupitia maandishi, machapisho na mihadhara inayoibua hisia, matumaini na wakati mwingine hasira. Zaidi ya yote, ni miongoni mwa Watanzania wachache wanaoielewa historia ya mapambano ya kidemokrasia na ya kijamii ya watanzania na Bara la Afrika kwa ujumla. Ni kwa sababu hii UDASA iliamua kuwachagua kuwa wazungumzaji wakuu katika kongamano hili muhimu.
Tunarajia kuwa kongamano hili litatoa mwongozo kuhusu maudhui na mchakato mwafaka katika kufikia Katiba Mpya yenye kubeba matakwa na utashi wa Watanzania wote.
Wananchi wote wanaalikwa kuhudhuria kongamano hili.

Dk Kitila Mkumbo
Makamu Mwenyekiti na Mratibu wa Makongamano, UDASA
0754 301908 kitilam@udsm.ac.tz
 
Tatizo ni wazungumzaji- tumeshawasikia sana kuhusu hilo, hakuna na wengine? kama Profesa safari, Zitto Kabwe, Dr Mwakyembe etc- ni wazo tu
 
Dr. Kitila tuko pamoja.

In fact nilisoma Raia Mwema last week jumatano waliandika Kongamano litakuwa "Jumamosi ijayo" nilipofika last Saturday nikakuta Nkurumah pako kimya!!! Nikarudi home na "Nondo" zangu nilizoziandaa.

Tutafika bila shaka ingawa nina wasiwasi muda unaweza usitoshe. Bora tumalize saa 10 jioni. Maana binafsi kama nikipewa fursa bila time limit, nahitaji kama saa moja kuwakilisha hoja zangu.
 
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

Academic Staff Assembly



JUMUIYA YA WANATAALUMA CHUO KIKUU CHA
DAR ES SALAAM (UDASA)
inawaletea:
KONGAMANO LA KATIBA


MADA KUU: MCHAKATO NA MAUDHUI YA KATIBA MPYA


WAZUNGUMZAJI WAKUU:
1. PROFESA ISSA SHIVJI
2. NDG JENERALI ULIMWENGU

TAREHE: JUMAMOSI, 15 JANUARI 2011
UKUMBI: NKRUMAH, CHUO KIKUU CHA DSM
MUDA: SAA 4:00 ASUBUHI HADI SAA 8:00 MCHANA


WOTE MNAKARIBISHWA

kitu kitakuwa kimetulia saana
 
jamani mliokaribu msikose fulsa hiyo, nasi tulio mikoani tutaendelea kufuatilia kupitia vyombo vya habari. na ikiwezekana tunaomba watoa mada wasisaha mikoani ambako ndio kuna idadi kubwa ya watu tusiojua hata rangi ya katiba iliyopo sasa!
 
ha ha ha nadhani polis wameanza kujuta kwa matendo waliofanyia wananchi arusha nadhani kwa dar patakuwa shwari kabisa

hoja tupu hureeeeeeeeeeeeeee
 
Dr. Kitila tuko pamoja.

In fact nilisoma Raia Mwema last week jumatano waliandika Kongamano litakuwa "Jumamosi ijayo" nilipofika last Saturday nikakuta Nkurumah pako kimya!!! Nikarudi home na "Nondo" zangu nilizoziandaa.

Tutafika bila shaka ingawa nina wasiwasi muda unaweza usitoshe. Bora tumalize saa 10 jioni. Maana binafsi kama nikipewa fursa bila time limit, nahitaji kama saa moja kuwakilisha hoja zangu.
Upewe saa nzima kwani umekuwa mtoa hoja inabidi uandae kongamano lingine kwa kawaida mass wanapewa 5-10min.
 
Back
Top Bottom