Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 44,190
- 129,599
Kuna wakati huwa ninajiona nina akili sana. Mimi ni kati ya watu wachache humu jukwaani niliyekuwa nina upinga muungano wa changu changu, chako changu hata kabla ya huyu Mzanzibari kuokota embe dodo chini ya mti wa mwarobaini. Na sijawahi kuwakubali Wazanzibari kwa sababu ninatofautiana nao kila kitu.John Heche anena mazito juu kalia zinazotolewa toka Zanzibar ;
Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara..
Maneno muhimu kutoka kwako:
Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari?
Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika.
Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika.
Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko?
1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar?
2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu,
Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika?
Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara?
Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar?
Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya….
Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu?
Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao.
Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?
Lakini nashukuru pia mimi ni mmoja wa wananchi ambao tulipiga kura ya maoni ya kuunga mkono uwepo wa serikali 3, badala ya hii takataka tuliyoirithi tokea 1964.
Kiufupi huu muungano ni wa kipumbavu.