Tanganyika nje ya Muungano Inawezekana?

Tanganyika nje ya Muungano Inawezekana?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,253
Reaction score
44,595
1239052_10151707297686156_54493065_n.jpg
 
Kwa nini tusikutane SADC au EAC mpaka iwe Umoja wa mataifa. Au ndio yaleyale ya Kaunda the Arab republic of Zanzibar? In reference to the Arab republic of Egypt.
 
Mzee madoshi,

Kwani ikiwa hivyo weewe utapoteza nini so far.....??

Au how much will it costs you.....???
 
Kinacho tumaliza tuna ishi kwa hisia zaidi, kwaanini ulazimishe kitu ambcho muhusika mwingine hajisikii, Si halali muungano wa lazima, Zanzibar inaweza kuwa shirikisho na maisha yakaindelea mbela kwa raha zaidi!
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Kwanza uliadimika sana hapa jamvini. Naona umerejea na hii imekurudisha kwa kasi mkuu wangu.
 
Last edited by a moderator:
Kweli WaTanganyika na WaZanzibari wamechokana sasa.
 
Kakke;7222818]Zanzibar. Kamati ya Maridhiano imetoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba ya JMT kwa kutaka Zanzibar ijitegemee karibu kwa kila kitu.Maeneo inayotaka yaondolewe kwenye Muungano ni uraia na uhamiaji, sarafu na Benki Kuu, mambo ya nje na usajili wa vyama vya siasa.
Hapa wanataka kila kitu isipokuwa Ulinzin na usalama. Kama ni hivyo kuna haja gani ya kuwa na muungano?Si wameshasema wanataka kujitegemea kila jambo, sasa muungano wa nini?
Kamati hiyo inayounga mkono muundo wa muungano wa Serikali tatu inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo, iliwasilisha mapendekezo hayo juzi katika Ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema kuwa maoni hayo ndiyo mawazo ya Wazanzibari wengi.
Huu ni uganga wa kienyeji. Wao wamefanya tafiti gani au wana data zipi za kuonyesha kuwa huo ndio msimamo wa wazanzibar wengi? Kwanini wasifikirie kura ya maoni ambayo itatoa takwimu za uhakika wanataka tuamini mawazo ya watu sita kama mawazo yao.
Na je wanaweza kutuambia msimamo wa Watanganyika ni upi kwanini wadhani maoni yao ndio muhimu katika katiba na si ya Watanganyika wapatao milioni 40. Huwezi kuongelea muungano kama huna data za kila mahali na kile unachokongelea
Msimamo wa kamati hiyo unaelezwa kuwa chanzo cha mmoja wa wajumbe wake, Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uanachama wa CCM, Agosti 26 mwaka huu
Huu kama si wendawazimu sjui ni kitu gani. Yaani wanatengeneza katiba ya kumfurahisha Mansour!!!Halafu ndio maoni ya wazanzibar wengi. Kama kamati ni ya kupuuzwa
Akisoma mapendekezo hayo, Jussa alisema kwa kuwa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar uliziunganisha nchi zilizokuwa huru, unatakiwa kuitwa Muungano wa Jamhuri za Tanzania, kusisitiza kuwa rasimu hiyo inatakiwa kueleza wazi kwamba nchi nyingine zinaweza kuingia kwenye muungano huo
Kama wanataka kila kitu kiondolewe sasa wanataka muungano wa nini? Halafu wanasema eti katiba iseme nchi yoyote inaruhusiwa kujiunga! To hell! tuna EAC tuna SADC, AU wao wanataka nchi gani tena. Huu ni mkataba aliobaki nao Maalim pale chumbe.
Ni ima mkubali muungano au muondoke. Mnababaika baika nini?
Alisema kamati hiyo imependekeza kuwa mambo ya nje yasiwe suala la muungano na badala yake nchi washirika zisimamie zenyewe eneo hilo
Tanganyika tunasema ulinzi na usalama usiwe wa ushirika kila nchi isimamie ulinzi na usalama wake. Period
"Kila nchi mshirika (Zanzibar na Tanganyika), ibakie na uraia wake na mtu kuwa na uraia wa nchi mshirika ndiko kumpe uhalali wa kuwa raia wa shirikisho," alisema
Wanogopa kuwa nje ya muungano I mean bila jina Tanzania wataumia.
Sasa wanashauri kuwe na passport za Tanzania-Tanganyika, Tanzania-zanzibar ili waendelee kujibanza katika mambo ya ulinzi na usalama, soko, ajira na ardhi. Tanganyika inasema ukishakuwa na passport yako wewe utakuwa raia wa kigeni tu hakuna ujanja wa kujificha nyuma ya mgongo wa Tanganyika. Maoni hayo mwisho chumbe
Pia kamati imependekeza Rais wa muungano ambaye atakuwa na madaraka ya juu katika shirikisho lote kwa mambo yote ya Muungano, hivyo nchi washirika zinapaswa kuwa na haki sawa katika kutoa watu wa kushikilia Baraza la Mawaziri la Muungano, Bunge na Mahakama.
Utamaduni wa mzanzibar ni kudai haki asiyojua inapatikana kwa gharama gani.
Wao akili zao zipo katika vyeo. Hiyo kamati haielezi serikali ya muungano itagharamiwa kwa usawa gani.

Akili ya mzanzibar ni kutaka vyeo gharama wamtupie Mtanganyika. Wekeni mezani gharama zinalipwa vipi na kwa utaratibu gani. Usawa wa vyeo mwisho chumbe, ukivuka chumbe uje na kitu mezani si maneno maneno tu.
Alisema rasimu inatakiwa itamke wazi kwamba urais wa Muungano utashikwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya nchi washirika yaani Tanganyika na Zanzibar na kwamba Rais atangazwe mshindi baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 50 kutoka Tanganyika na Zanzibar
Utamaduni ule ule wa kudai vyeo bila kujua gharama. Utamaduni huu tumewajengea kwa miaka 50 na sasa wanadhani ni hali yao kubebwa katika mbeleko kila siku. Kamati tunawaambia mwisho wa mbeleko, ukija Tanganyika uje na kitu si maneno na bla bla
Alisema badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa Makamu wa Rais kupatikana kutokana na mgombea mwenza, marais wa nchi washirika (Zanzibar na Tanganyika) moja kwa moja wawe makamu wa kwanza na makamu wa pili wa Rais wa Muungano
Akili ya mzanzibar ni cheo tu basi hafikiri zaidi ya hapo. Hii ndio kamati ya watu wenye weledi! real! phwee, kamati imekaa miezi miwili hawana data za iana yoyote za kiuchumi au kijamii.
Walichokuwa wanafikiri ni namna ya kugawana vyeo bila kujua gharama za kuendesha serikali hiyo


Kama znz inataka usawa basi usawa huo uwe katika kila jambo.
Huu utamaduni wa kudai veyo na gharama kumtupia Mtanganyika sasa basi.
Mtanganyika amelipa sana na hana sababu za kuendelea kulipa.

Sijui wanachoogopa kusema vunja muungano ni kitu gani. Ukishakubali kuitwa Tanzania basi ujueu kuna gharama zinaambata na jina hilo siyo veyo.

Wazanzibar utamaduni wa kudai vyeo bila kujua gharama zake ni utoto jaribuni kuona mbali zaidi. T
umechoka jamani kujadiliana na watu kama hii kamati.

Muda waote hawana data za kiuchumi wamejifungia wakiangalia nafasi za vyeo! It's rubish the least to say.
I am sorry , I couldn't find a better word.


JokaKuu Jasusi GHIBUU Mchambuzi Zitto
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wa aina mbili, wale wanaopenda na kuacha, na wale wanaopenda jumla!.
Huyu mke nimependa kwa moyo wangu wote na simwachi ng'o!.
Kuna makuwadi, wanamjaza utambi adai talaka ili wamuozeshe kwa bwana mwingine!.
Hili silikubali hata kidogo!.
Ameshawishiwa kutembea nje ya ndoa (mabadiliko ya katiba), akidhani sasa ndio nitataliki, simtaki ng'o!.
Sasa ameomba ruhusa kuhama chumba eti atakuja siku tuu za chakula, ile zile nyingine agawe kungine!, sikubali ng'o!.
Ndoa yetu ni ya mume mmoja, mke mmoja! 1+1=2!. Kwa vile napenda, pamoja na visa vyake hivi na vile, nitamvumilia mpaka mwisho na simwachi ng'o!.
P.
 
Back
Top Bottom