Tanga; Mkoa uliokufa


You aren't serious at all [emoji15] heading inazungumzia Mkoa alafu content Jiji [emoji848] huwezi kuona mazuri ya tanga in two weeks jipe muda usiwe na papara. Vigodoro ndio tamaduni yetu tunakula bhata Kwa gharama nafuu, kuoa na kuachika maarufu kama chuo/vyuo ni matumizi sahihi ya uhuru wa mtu kumbuka mke/mume siyo baba wala mama yako kama unabisha rejea mahusiano ya wazungu.
Tanga ya leo;
1. Kampuni 3 za ndege zinazofanya safari zake kila siku.
2. Meli kubwa ya abiria na mizigo tanga-pemba hadi unguja
3. Treni ya mizigo inapiga kazi
4. Mabasi ya maana kibao
5. Uzalishaji wa mkonge umeongezeka 50 times as compared to 1999
6. Uzalishaji wa Korosho, iliki, mdalasini, karafuu umeongezeka 100 times
7. Viwanda vipya na vikubwa kibao
8. Hoteli za kisasa kibao
9. Bomba la gesi na mafuta on the way
10. Sekta ya nyumba na makazi ndio usiseme
 
Acha kutetea upuuzii..mkoa wenu unazid kudidimia wakat kuna mikoa Kama...... Iringa.. singida... morogoro....NK.... wadigo.. wabondei... Tanga sio jiji CCM wamewadanganya Sana Kimapato Tanga mnazidiwa na Mafinga....

Let's talk with figures
 
Umekaa wiki mbili tena umeishia huko uswahili a.k.a barabara za namba, halafu unakuja na jibu lako kama hilo? Acha kuwadanganya watu.

Mji umekufa lakini watu wanaishi na idadi yao inaongezeka kila siku.

Usafiri umeongezeka, mabasi yanaongeza ruti na ndege zimeongezeka pamoja na meli halafu unasema mji unakufa.

Viwanda vipya vya saruji (Sungura na Rhino) vimefunguliwa huku wachina wakitarajia kujenga kiwanda kikubwa cha saruji kuliko vyote ukanda wa Afrika Mashariki halafu unasema mji umekufa?

Site mpya za Mwahako, Neema, Kange, Kasera, Pongwe mpaka Machui umezitembelea? Kama huko ni mbali shuka kidogo na Karume road ukianzia Duga mwembeni mpaka Tanga Beach Resort uone makao mapya.

Nyumba chache za makuti zilizobakia hapo utakuta wengi wa wamiliki walishakufa na walioachiwa urithi wana migogoro nazo. Hata hvyo ujenzi wa makuti ni utamaduni lakini sio kiashiria cha umaskini.

Watu kukaa barazani kwenye mikeka wakicheza bao na kunywa kahawa sio kama hawana kazi, hapo wamebarizi baada ya kazi au wakisubiri waingie kazini jioni au usiku kwa wale wavuvi.

Ukumbuke wengi wa wanamji ni waislamu hivyo huwezi kuwakuta baa au vilabuni wao hukaa vibarazani mwao.

Fanya utafiti wako kisomi kisha uje tena.
 
Mkuu lengo la mleta mada ni kututaarifu tu kua alikua masomoni Nairobi for 18 yrs,analeta malalamiko ya kufa kwa mji wa Tanga bila kua na figure au fact za kufanyia comparison ya 1999 na 2017,hawa ndio wale wakibahatika kutoka kidogo tu huanza kudharau kwao,

Sasa Nairobi tu imemtoa akili je akienda nchi zilizoendelea si ndio atadharau kila kitu huko kwao?
 
Wewe mambo mengi Inaonyesha umeambiwa.Huijui Tanga vizuri,,,nakushauri kaa fanya utafiti vizuri mwenyewe utajua ukweli.
 
Mwamvie huyo
 
Acha kutetea upuuzii..mkoa wenu unazid kudidimia wakat kuna mikoa Kama...... Iringa.. singida... morogoro....NK.... wadigo.. wabondei... Tanga sio jiji CCM wamewadanganya Sana Kimapato Tanga mnazidiwa na Mafinga....
Wewe naona umejitune kuiweka tanga katika kundi unalotaka. Hii ni dhahiri kuwa uelewa ni mdogo hivyo hata ukipewa viashiria ambavyo hukuvijua bado utabisha tu
 
Mji wa amani mnataka kutuletea balaa tu. Ukipita barabarani vitafunwa teleee, bagia, maandazi, kaimati, vibibi, mikate ya kumimina, kachori. Alafu useme watu wake masikini, duuuu huu ni ujinga sasa.
Aliyeleta mada ni mwepesi sana kichwani haina haja ya kutumia nguvu.
 
Mkuu aliyeleta hoja ni mwepesi sana kichwani hivyo watu kama nyie kumjibu inabidi kuwa mvumilivu sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…