Tanga kwetu raha

Tanga kwetu raha

Pande za Bombo hapa weekend kama hii ni kujiachia tu Raskazone beach na watoto wa kitanga
 
Uzi maalumu kwa wana JF walio zaliwa Mkoa wa Tanga hata kama haupo Tanga ila Tanga ndio Nyumbani basi husika Hapa,Dhumuni ni kufahamiana.

Tanga ndio mji unaoendelea kwa kasi Tanzania akiachana Dar, na Arusha,Tanga ndio inafata.

Tanga tumejaaliwa kuletewa mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuja Tanga katika kijiji cha Chongoleani.

Uchumi: uchumi wa Tanga katika miaka ya 2000 ulishuka kutokana na Viwanda vingi kufa lakini ujio wa Bomba la mafuta utapelekea JIJI letu kuendelea kuku-kwa kasi.

Viwanda: Viwanda Unga wa ngano pembe Viwanda vya cement,simba ,rhino Viwanda vya mafuta sabuni na lotion Viwanda vya soda healtho na anjari Kiwanda,cha majani ya chai ya amani Kiwanda cha nondo Ambon plastic,Maji ya kunywa. Tanga fres tunazalisha maziwa ya kuuza Nchi nzima. VIWANDA vipo vingi naomba niishie hapo.

Licha ya kuwa ndio umepangika kuliko mikoa yote Tanzania,
Lakini mkoa,wa Tanga ndio mkoa uliokamilika sana kiasi kwamba wakisema kila mkoa ujitegemee nahisi utakuwa mbali sana.

Utalii Kuna pwani ya pangani Mbuga ya saadani
Shamba la vipepeo lushoto Mapango ya Amboni nk

Michezo: Uwanja,wa mkwakwani Timu,3 kubwa coastal union african,sports na mgambo jkt Coastal waliwa kuchukua ubigwa wa ligi kuu. Japo kwa sasa timu zetu hazipo kwenye ligi kuu lakini tunapambana turudi tena.

Matunda Maembe kule handeni dr idrs rashid ana heka 100 za miembe na ndio muuzaji mkubwa kwa bakhresa,Machungwa,Mananasi,apple Mafenesi nk.

Social: media: Tanga Tv, Redio mwambao, Tanga raha fm nk.

Elimu: zipo shule kubwa kama Tanga take. Usagala nk

Mimi kama mkaazi wa Tanga, Nawatambulisha kwenu Matajiri- Mabilionea wawili tu wa Jiji la Tanga Bw Gulam ambaye ana kituo cha mafuta mkabala na kituo cha polisi cha kati hapa Tanga, huyu ni mfanyabiashara wa mafuta na Bw Kifaranga ambaye ndie mmiliki wa RATCO ( kampuni ya usafirishaji ) na mwingine ni Mzee Simba mtoto ( kampuni ya usafirishaji )pia !
Kwa Jiji la Tanga ukiwataja hao kwanza unakuwa unazungumzia Wakwasi wa mkoa wa Tanga ijapokuwa wapo wengi sana na wanazidiana tu kwa nukta chache !

Tanga tumejaaliwa kuwa na hotels za nyota tatu kama Tanga beach resort, Nyumbani hotel, Mkonge hotel,Kwetu hotel, Dolphin holel,nk.

Naomba niishie hapo: TANGA NDIO HOME
Shehoza kashafilisika? na Badru Issa yule mhaya
 
Madame s unakaa wapi nije nikutembelee jumapili?
Au kwenu mlango upo juu ya bati?
 
tanga ndio inaaibisha kanda ya kaskaxini
mnatakiwa muwe kanda ya pwani kwa wavivu wenzenu
ktk kaskaxini,tanga ndio ya mwisho kila kitu

Huo Ndiyo ukweli japokuwa wengi huwa hawapendi kuambiwa ukweli!
Asili, jadi na chimbuko la wazazi wangu ni Tanga ijapokuwa nilizaliwa Muhimbili !
Unakuta Mtu ana familia hana kazi yeyote lakini mapori kibao Ila hataki kushika jembe alime japo hata kuazima shamba la Mtu kwa kumuazima!
Walau wazigua wa Handeni, pande Za Kilindi na Ushoto huko ndo wanajitahidi kulima ingawa ukiwakuta wamechoka!
 
Siyo wote Ila kusema ule ukweli walio wengi ni "wabwa" Kama wakwele
 
n kweli mkuu
hawa watu wao n kucheza baikoko tu,wanaaibisha kanda ya kaskazn wahamishiwe pwan kama vp
 
Back
Top Bottom