Tanga fresh mko serious kweli?

Tanga fresh mko serious kweli?

hii post ni ya muda ila imenivutia kwasababu mm kila siku usiku lazima ninywe Tanga fresh pakti moja na nimefanya hivyo zaidi ya mwaka sasa sijawahi kukutana na ladha tofauti ladha ni ileile tena yenye ubora wa hali ya juu.
 
yatakua yamekweisha muda wake wa matumizi hayo, pole sana.
 
Binafsi huwa sipendi harufu na ladha yake pia
 
Yalikuwa hayaja expire.., na hii ni mara ya pili.., hata mara ya kwanza yalikuwa hivi hivi.., nikafikiri watakuwa wame improve..lakini wapi.., em' kunyweni brooklyn afu ndio mje kuongea hapa..

Hao brooklyn wanakulipa kiasi gani kwa hili promo unalowapigia.

Sijawahi ona tatizo lolote kwa maziwa ya Tanga Fresh.
 
Hii ni promo kwa maziwa kutoka Kenya. Hakuna mada hapa. Maziwa ya Tanga Fresh yapo vizuri na wameshika soko la maziwa kwa Tanzania hususan Dsm. Inafahamika Brookside inafanya kila njia kuiondoa Tanga Fresh kwenye soko.
 
Excorcist ni mbwa kutoka kenya anaipigia debe brookside. Nitakunywa Tanga fresh hata yatiwe sumu ya panya. Rudi kwenu kenya kama unaona vya kenya ni bora. Narudia tena wewe ni taxi bubu tu.
 
tatzo huwa mnakurupuka bila hata kuangalia expire date
 
yale maziwa hayafai hata mimi juzi nimenunua,moro super market nilishangazwa na radha yake kama tui la nazi:A S confused:
 
Naungana na wewe mleta mada! Inshort hawa wa Tanga fresh hawako kiushindani kabisa. Wameralax tu wanaangalia watu wakinunua maziwa toka Kenya na South Africa. Packaging yake mbovu na sidhani hata kama ni salama kwa afya! Wenzao wameanza ku grade maziwa kulingana na fat % nk ila wao wala hawana time. Watanzania hebu tuamke tuwe creative jamani!
Juzi nilinunua maziwa ya Tanga fresh ya pakti.., nilipoyaonja nilishtuka mno..!! Yaani ladha yake ni kama maji ya kisima.., hayana taste kabisaaaa!! Na hakika kwa waliowahi kununua najua mnaelewa ninachosema. Hivi huko kiwandani hakuna watu wanao yaonja kabla ya kuingiza sokoni??! Matokeo yake tunaishia kununua maziwa toka kenya, uchumi wetu utakuwa kwa staili hii?!!
 
yale maziwa hayafai hata mimi juzi nimenunua,moro super market nilishangazwa na radha yake kama tui la nazi:A S confused:
Hiyo ladha ya tui la nazi ndio inanikera kabisa.., nimejaribu kumpa paka wangu ndio akanywa kwa shida sana. Mimi sio nafagilia mtu hapa.., ila tanga fresh mjifunze kutoka kwa wenzenzenu na mboreshe ladha ya maziwa.
 
Hiyo ladha ya tui la nazi ndio inanikera kabisa.., nimejaribu kumpa paka wangu ndio akanywa kwa shida sana. Mimi sio nafagilia mtu hapa.., ila tanga fresh mjifunze kutoka kwa wenzenzenu na mboreshe ladha ya maziwa.

Kama kuna tatizo tueleweshane na tuelimishane taratibu. sio kulivalia njuga kama tumeua mtu. Tumekusikieni na swala hili linafanyiwa kazi.....UTAWALA
 
Back
Top Bottom