Tanesco yatangaza mgawo; kuanza mara moja!

Mzalendohalisi,

Hiyo miradi mikubwa mikubwa ya Wachina iangalie sana mkuu, itakuja itokea Afrika puani. Hawa jamaa hii miradi mikubwa mikubwa hata kule kwao inawaletea matatzo sasa ndio iwe kwetu Afrika? Tuwe waangalifu sana.

Kama inawezekana tuwe na miradi midogo midogo ili hata kukiwa na matatizo sehemu moja basi effect yake haiwi kubwa sana.

Kwa nchi maskini kama za kwetu ni hatari sana kutegemea hii miradi mikubwa mikubwa. Kama ule mradi wa Singida utafanikiwa itakuwa nzuri, changanya na umeme wa maji, imarisha Kiwira na ule mgodi mwingine wa makaa ya mawe, ongezea technology ya solar kwenye miji midogo midogo, nafikiri ndio strategy nzuri.

BTW: Nilikuwa najua IMF wanatuonea Afrika, nimeona walivyowabana Ukraine, Slovakia na Iceland, kumbe Mwarobaini ni ule ule.

Mtanzania,

A you serious?? Mtanzania miradi midogo midogo??? Kama dowans, upepo singida, wa megawats 50, 100, 200 n.k?? Hiyo mirandi midogo2 ndo imetufikisha Tz hapo mgao kila siku na Ufisadi mbele! Miradi midogo poa ila just to compliment miradi mikubwa!

Kumbuka only 10% ya watz wana umeme sasa hivi!

Maendeleo ya viwanda, infrustructure ni energy..sasa tuendelee kusuasua hadi lini?

Let us be ambitious kuwa na miradi ya kuzalisha hata 5,000 megawats..then tuachane na kufikiria dowans n.k we can export ziada kwa nchi zingine!

Mkopo utoke, mbinguni, China, US.. I dont care! We need reliable source of energy!

Kama tungaliinvest pesa nyingi ktk Energy leo tungekuwa mbali kiasi!
 
Last edited:
Hivi nyinyi pale bungeni huwa mnafanya nini zaidi ya mchezo wa kuigiza? IPTL mnakubali inunuliwe, Dowans mnakataa, matatizo mnayaona kila siku, lakini kila kitu afanye Rais, hata kutatuwa matatizo ya umeme ni kazi ya Rais? nyinyi mshaona tatizo, mnaishia tumetowa pendekezo, hilo pendekezo lenu litasaidia nini? mapendekezo mangapi mmeshatowa ambayo hayana tija yoyote?

Kazi yenu kuongea na kujijengea umaarufu na wengine toka bunge lianze kurushwa live tumeona kuwa ni ma-actor wazuri. Ni wakati wabunge ma-actor wa Tanzania mujiingize kwenye kucheza filamu, mtasaidia sana katika kukuza soko la filamu za Tanzania.

Hamna lolote zaidi ya kupayuka na kuigiza.

Hivi ni lini mtaacha fikra za kulaumu na kutaka kufanyiwa, kufanyiwa, kufanyiwa na kusema, kusema, kusema? Sijawaona mkijitapa kuwa tumefanya, tumefanya, tumefanya! afadhali hata ya Mwakyembe alipoona kuna tatizo la umeme akajitafutia ulaji wa kutafuta makampuni ya kuzalisha umeme wa upepo.

Mkuu utakuwa unakosea sana uki-generalise hawa wabunge. Kwa kweli kuna wengine wanajitahidi sana ila support ndo hawapati wapo wachache. So being specific kwenye hoja yako ukawataja ingekuwa na nguvu zaidi.
 
Ethiopia wanajenga Dam la USD 1.7 Billion by 2011 litakamilika na watazalisha over 2500 Megawats na ingine wataexport to Kenya! Wamekataa katakata kuwasikiliza WB na IMF inaonekana wamepata mkopo toka China!

Sudan nao pia wamefungua Bwawa kubwa sasa juzi kwa mkopo toka China!

Yet sisi bado tunazungumzia kununua Dowans ya Magawats sijui 50!!!!

Hivi Watanzania tutaamka lini???

Mradi Mkubwa wa Umeme utaanza lini?

....sisi tutaanza wa kwetu tukishatoka, Kenya, Comoro, Madagasca, Afrika ya kati, Zimbabwe, Malawi,etc. Kwani tuna haraka gani mh!
 
Mzee Mwanakijiji nilshakuambia sikio la kufa halisikii dawa. Kwa hali ilivyo hata ikiwashwa mitambo ya Dowans tatizo liko pale pale. Mitambo ya SONGAS iliyoharibika inalisha kiana ambako kwa mtandao mbovu ulivyo hatuwezi kuepuka mgao. Hata mabwawa yamwagike maji mwenye hisa ameziba masiko kuhusu kuwekeza ili kufanya upanuzi wa miundo mbinu ya kusambaza umeme Bongo inayokuwa Haraka kuliko akili fupi za watawala. Dr.Idris asijidanganye kwa sababu hadidu rejea za ajira yake ni ya miaka mitatu tu hata akilala ofisini asiote kwamba ufumbuzi ni kununua Dowans. YALISEMWA mdharau chake hudhamini cha mwenzake. TANESCO wakiendelea kuachia makampuni uchwara kama SONGAS waandike maumivu. Migawo itaendelea mpaka kiama kwa TZ kama maswala nyeti yataachwa mikononi mwa wasanii ambao hawadhamini wataalam waliobobea na waachiwe waendeshe Shirika. Tatizo ni serikali kuweka mashabiki wa kisiasa kama Ngeleja na Malima kwenye wizara nyeti ambao upeo wao ni mdogo. Biashara ya majenereta na kelele mitaani Ruksa!!!!! mbonde angalia mkono huoo!Kelbu!!!!!Kama mitambo ya AGGREKO bado ipo iwashwe ipunguze makali. sijafika Bongo muda wa mwezi mmoja sijui kama imeondolewa au wanangojea walipwe pesa za kodi ya TRA na TANESCO kwani mkataba si unasema hivyo!!!!!! Mkulo, WIZARA na Bodi ya wakurugenzi minyeni kidogo akishalipwa ndio iundwe tume ya kuchunguza!!!!
 
Ama ndo technical knowhow ya Songas kutaka kununua mitambo ya dowans kama dharura. Manake viongozi wanatuburuza kwa kuingia deal feki kiola kukicha, bila aibu. Wanachofanya ni kutumia kiburi, ubabe na dharau ilimradi tu wanafikia malengo yao ya kuchota vijicent. Watambue ya kuwa watanzania wengi sasa si malimbukeni kiasi hicho wanachofikiria, Hakika muda umefika, watajutia uovu wao.
 
..............Mmh!!!!!!!! Maumivu ya kichwa huanza pole pole...............
 
Mnanikumbusha zile kelele za majenereta Samora na Kariakoo. Kumbe mpaka tutazeeka tunazisikia tu. Kweli maendeleo TZ ni ndoto ya mwendawazimu???????
 
Hivi nyinyi pale bungeni huwa mnafanya nini zaidi ya mchezo wa kuigiza? IPTL mnakubali inunuliwe, Dowans mnakataa, matatizo mnayaona kila siku, lakini kila kitu afanye Rais, hata kutatuwa matatizo ya umeme ni kazi ya Rais? nyinyi mshaona tatizo, mnaishia tumetowa pendekezo, hilo pendekezo lenu litasaidia nini? mapendekezo mangapi mmeshatowa ambayo hayana tija yoyote?

Kazi yenu kuongea na kujijengea umaarufu na wengine toka bunge lianze kurushwa live tumeona kuwa ni ma-actor wazuri. Ni wakati wabunge ma-actor wa Tanzania mujiingize kwenye kucheza filamu, mtasaidia sana katika kukuza soko la filamu za Tanzania.

Hamna lolote zaidi ya kupayuka na kuigiza.

Hivi ni lini mtaacha fikra za kulaumu na kutaka kufanyiwa, kufanyiwa, kufanyiwa na kusema, kusema, kusema? Sijawaona mkijitapa kuwa tumefanya, tumefanya, tumefanya! afadhali hata ya Mwakyembe alipoona kuna tatizo la umeme akajitafutia ulaji wa kutafuta makampuni ya kuzalisha umeme wa upepo.

Mkuu sahamani kama nitakuudhi, by the way fani yako ni nini?

Maana sipati picha unaposema bunge ama wabunge waingie kwenye utendaji.
Kazi yao ni kutunga sheria na kusimamia serikali kutekeleza majuku yake.

Rais ndio anateua watendaji wote kwa case hii Dr. Idrisa kachaguliwa na Rais na Idrisa hawajibiki bungeni. Ni wajibu wa rais kuwaeleza wananchi tatizo linaloikumba nchi kwa wakati uliopo (by then ilikua umeme) na akasema ni njia zipi zitakazotumika kutatua tatizo once and for all. Je, kama ilishindikana alirudi kuja kuwaambia wananchi????

Kama priority haikuwa umeme labda ilikua ni kutatua njaa ambayo by then ilikua tatizo je kwa anini aliwapa wananchi hiyo taarifa /ahadi???????

Je bunge/wabunge including Dr, lilitimiza wajibu wake??? sihitaji kukuambia na kwanini mtu anatetea Dowans tu?????


Kuhusu suala la IPTL serikali hainunui mitambo bali serikali inanunua (buy-out) Company inayoizalisha umeme inayoitwa Independent Power (T) Limited (IPTL) pamoja na assets zake, hivyo gharama za kuinunua ni pamoja good will, staffs, n.k. Na kama itaona vema kubadilisha mitambo baada ya kuinunua then itafanya hivyo tofauti na Dowans tunanunua mitambo na sio Company ya Dowans. Hivyo huwezi kucompare tembo na swala

Dar es Salaam, kiongozi asiye na mpango ni sawa na kondoo asiye na mchungaji akija mbwa mwitu.........


WAZEE WA KUCHOMA NDIZI
 
Ndio maana kuna mihimili mitatu ya dola .....Executive, Legislative na Judiciary ....sasa kama kila mtu akitakiwa afanye la mwenzako kuna lolote kweli litafanyika....kwa maana ya kukosa coordination.

Nchi hii ina matatizo mengi tu na wala sio umeme, inachotakiwa ni Rais na serikali yake kuwa na vision ya kujua tatizo lipi au matatizo yapi yaanze kutatuliwa kabla ya mengine ambalo/ambayo litakuwa/yatakuwa na multiplying effect ya kusababisha matatizo mengine yatatulike kwa urahisi. Badala yake tunaona ni miaka inakwenda mbele lakini hamna kitu cha maana kinafanyika

Mkuu heshima mbele,

Umeme kwa taarifa yako ni driving engine of the economy. Moja umeme ukiwa ghali production costs inakuwa juu hivyo bei ya bidhaa kwa mlaji nayo inakuwa juu. Pili ukikosekana umeme production inasimama so unaemployment,
kodi itokanayo na hizo biashara zinakosekana, mkiimport kama substittion mnadrain Forex thamani ya Sh inapotea, ...... the list of problem is endless na ni vicious. So angalia nchi nyingi Duniani Umeme unazalishwa na mashirika ya serikali ama serikali ina share kubwa why???? usiniulize kwa sasa

So serikali inalojukumu la kufanya umeme ndio priority, na ni aibu kubwa kwa shirika kubwa lenye monopoly power linakosa short, medium and long term plans. shake up kidogo 53MW (less than 10%) of its total production imeshake imediately unaanza mgao KWANINI TUSIFIKIRIE HUU NI UFISADI AMA NI HUJUMA?????

WAZEE WA KUCHOMA NDIZI
 
Du, siamini kama linatoka kwako mkuu,

Kama mtu hafai si mnamuondoa weka wenye uwezo sasa wewe unawaza kuuuza majenereta tu mkuu

..usimshangae sana huyo mheshimiwa wetu maana mtu akishiba sana huwa anacheua tu bila kujali kama anachafua au la...
 
Nyie hamtaki.. nilisema Mwezi wa nne watu wakaja juu utadhani nini! Nimesema majenereta yatanunuliwa mtake msitake kwani kuna watu wanadaiwa na lazima walipe milioni 60 si mchezo.. watu hawataki. Na mkigoma mtanyimwa umeme masaa 12 hadi mpige magoti na kukubali kuvunjwa!

Msiwe na shaka.. kesho na Ijumaa nadhani moto wa mapambano unazidi kuwashwa! Maneno ya Mzee Malecela leo yatakuwa yameangukia kwenye sikio lisilosikia! Kama mnataka ile kongwa ya mafisadi ivunjwe ni kuendelea kusimama imara kuipinga Dowans; Kama mmewahi kusikia kuwa nchi imetekwa nyara.. basi ndiyo hivyo.. je mtafanya nini kuigomboa?

Leo wanataka mnunue Dowans.. ili wawape umeme kesho watataka mfanye nini? !!

NO DOWANS, NOT BOWING DOWN!

Mkuu uyasemayo ni kweli. Maana mimi kwa upande wangu najaribu kuangalia hivi sasa mvua zipo za kumwaga maeneo kibao sasa huo mgao unatokea wapi? Inamaana huo umeme wa maji ndiyo haupo? Na kama upo hausaidii chochote? Nafikiri wamefanya purposely ili watu wakose umeme wapige kelele waseme tulisema tununue Dowans mkagoma. Jamaa wamelala tu hawana vision nothing.

Hakuna kukubali tukae hata kwenye giza lakini Dowans no. Moto umewaka uendelee kuwaka mpaka kieleweke maana hawa jamaa wao wanajiona ndiyo kila kitu. Maana watu wa kawaida watasuffer lakini na wao watasuffer vilivyo though wana uweza wa majenereta lakini nao watakiona cha moto. Hakuna kurudi nyuma mwendo mbele..
 
Mkuu heshima mbele,

Umeme kwa taarifa yako ni driving engine of the economy. Moja umeme ukiwa ghali production costs inakuwa juu hivyo bei ya bidhaa kwa mlaji nayo inakuwa juu. Pili ukikosekana umeme production inasimama so unaemployment,
kodi itokanayo na hizo biashara zinakosekana, mkiimport kama substittion mnadrain Forex thamani ya Sh inapotea, ...... the list of problem is endless na ni vicious. So angalia nchi nyingi Duniani Umeme unazalishwa na mashirika ya serikali ama serikali ina share kubwa why???? usiniulize kwa sasa

So serikali inalojukumu la kufanya umeme ndio priority, na ni aibu kubwa kwa shirika kubwa lenye monopoly power linakosa short, medium and long term plans. shake up kidogo 53MW (less than 10%) of its total production imeshake imediately unaanza mgao KWANINI TUSIFIKIRIE HUU NI UFISADI AMA NI HUJUMA?????

WAZEE WA KUCHOMA NDIZI

Hii itakuwa ni ujuma kwani hata kipindi kile wakati khali iko mbaya kabisa walikuwa wanakata umeme masaa 8 mpaka 12. Sasa leo hii huo upungufu kidogo mgawo. Mimi nafikiri hata kwenye kuchagua hawa watu kuna maslahi fulani maana haiwezekani mtu zaidi ya miaka 2 huna alternative huna emergency au back incase tatizo likitokea. Hii ni aibu hivi hii TZ watu wenye vichwa hakuna mpaka wang'ang'anie Dr. Idrissa?

HII NI HUJUMA INABIDI MAPAMBANO YAENDELEE HAKUNA KULALA NA NO DOWANS HATA WAKATE SIKU NZIMA
 
Hapana, ni dar es Salaam tu. Mitambo ya Songas iliyoleta matatizo inatumika kuzalisha umeme kwa ajili ya Dar na Zanzibar, hivyo sehemu nyingine za nchi hazitaathirika. Hata hivyo, tanesco hawajasema iwapo Zanzibar nayo itaathirika. Kwa kawaida dar na Zenji zinatumia kama megawati 370 hivi, zilizokosekana kutokana na kuharibika kwa mashine hizo ni megawati 53.

Zanzibar haina haja ya kusemwa huyo ni mwathirika nambari one hakuna mjadala ,alafu niliwambia watu kuwa Dar na Zenji kiza totoro ,wakaruka wajuvi na kusema eti Sinza umeme kama mchana labda huko mitaa ya uswazi ,
Walishindwa kuelewa ishala ya indicator.
 
Sasa nikiingia katika siasa nasema ,unao onekana ni uoza wa Serikali ya Sultani CCM,Uongozi ni sifuri ,na maadili ni chini ya zero ,na ukosefu huu wa uwajibikaji kumesababishwa na kulindana ,hawezi kufukuzwa mtu,hawezi kuwajibishwa mtu na wote ,unasikia wamejiuzulu kwa riza zao, kwa maana kama mtu angeendelea kung'ang'ania basi asingekuwepo wa kumwambia ondoka ,au kazi basi ila kifo. hivyo imebakiza zamu ya Mheshimiwa Kikwete nae kuweka ngumu ,just aseme wazee wa busara wamemtaka aendelee kuongoza nchi hii kwani jitihada zake hazijapata kuonekana kwa kiongozi yeyote yule ,afu apo Mkwere anazikubali busara za wazee na kusema ametii maneno yao ,huku kichwa kikimuuma sana kwa kuyakubali mashauri mazito ya wazee wenye busara. Nae atakuwa amemaliza kazi na hakuna wa kumpigia makelele ,kwani hata ukipiga makelele anaelewa wazi kuwa kelele za mlango tu.
 
Typical.... Lakini tumeshazoea kama kukaa na giza tumeshazoea sanaa tu. Hata tusiponunua Dowans, utashangaa wakiweka mkakati mwingine wa kununua umeme wa dharura, na kwa vile wanajua pakugusa tusishangae mambo yakajipa, tena!!

Hivi, walianzaga kutuambia Stiegler's Gorge etc etc etc, lakini hivi kweli kuna any long term plan ya umeme Tanzania?? tukiwa kwenye long term sustainabkle solutions, vipi maji, mafuta, chakula etc??

Mkuu NN alisema, MiAfrika ndivyo............., although natamani kukubaliana naye, still am in denial!!
 
Mgawo wa umeme kuanza leo Dar

2009-03-26 12:26:41
Na Mashaka Mgeta

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), limetangaza mgawo wa umeme unaoanza leo jijini Dar es Salaam kutokana na kuharibika kwa mtambo wa kuzalisha nishati hiyo.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa jana ilisema tatizo hilo linatarajiwa kudumu kwa muda usiojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtambo huo na mwingine unaofanyiwa matengenzo, inamilikiwa na kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas.

Mitambo hiyo ina uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 53, wakati kiwango cha umeme kitakachohusika katika mgawo huo wa dharura ni wastani wa megawati 50.

Taarifa ilisema kiwango cha kawaida cha mahitaji ya umeme jijini Dar es Salaam ni megawati 355, na hivyo umeme utakaokuwa unapatikana ni Megawati 302.

Tanesco ilisema kutochukua hatua ya kugawa umeme kutasababisha kukatika kwa nishati hiyo kwenye gridi ya Taifa katika majira ya asubuhi na jioni kutokana na kuzidiwa kwa transfoma za Ubungo.

``Hivyo basi mgawo huu utafanyika katika mji wa Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana na saa 12 jioni hadi saa 4:00 usiku,`` ilifafanua taarifa hiyo.

Aidha, taarifa ilisema Tanesco ipo kwenye mchakato wa kununua transfoma ya tatu yenye uwezo wa MVA 150 ili kuzuia tatizo kama hilo kujirudia.
 
Mchakato wa kununua Transforma unaendelea....
Mchakato wa michakato unaendelea.....
michakato wa mchakato inaendelea.....
kaaazi kweli kweli
hata kutuua ni mchakato unaoendelea......
 
Back
Top Bottom