Tanesco yafilisika!!!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Kuna habari za ndani kuwa TANESCO imefilisika wala haikopesheki tena.source katibu mkuu wa wizara!kama kuna mwana jf aliye na data zaidi amwage hapa. Tukumbuke 8% only ya watanzania ndio wapatao umeme wa tanesco
 
Yale mabilloni aliyokopa Rashid toka kwenye consortium ya mabenki zilikwenda wapi? Rashid alijulikana kuwa ni fisadi toka akiwa BOT and yet mkamchagua kwenda kuwa CEO Tanesco mlitegemea nini?
 
Zamani ilikuwa ni Chukua Chako Mapema, sera hii sasa imeboreshwa zaidi.
hivi sasa ni NYAKUWA NYAKUWA. kila anayepewa nafasi sehemu kama tanesco, kazi ya kwana nikuhakikisha kuwa amenyakuwa kila kinachowezekana. Hivyo kufirisika kwa shirika kama hilo si jambo geni sana bali ni jambo ambalo inatarajiwa na wengi hasa kwa kuzingatia udhaifu uliopo katika mamlaka za juu zinazosimamia utendaji wa menejiment katika mashirika.
 
bora ifilisike wachukue wawekezaji... tuweke deal na lowassa achukue tanesco na aache u-PM utaona tanesco itakavyopanda na kuweza kufikia 50% ya watanzania

Mhando wa tanesco tayari, bado mhando wa TBC
 
Nini kufilisika bora ife kabisa tuanze moja maana Hili Litanesco sioni hata faida yake umeme wenyewe mgao kila kukicha..aaggrrrr
 
Km TANESCO haikopesheki inamaana serikali haipokesheki maana ni Taasisi ya Serikali. Otherwise ni blah blah. Tuwe makini na hoja zetu.
 
Km TANESCO haikopesheki inamaana serikali haipokesheki maana ni Taasisi ya Serikali. Otherwise ni blah blah. Tuwe makini na hoja zetu.
TANESCO haijafilisika. Imefilisiwa. Imekuwa shamba la bibi tangu enzi za EPTL. Akina Mwinyi, Kikwete, Kolimba wote walijichotea. Ikaja awamu ya Mkapa akawaweka shemeji zake pale na wapwa na net solutions. Awamu ya Kikwete wakaendeleza libeneke na Richmond Dowans. Akaingizwa fisadi Rashid naye akajichotea pamoja na nyumba ya bure.
 
Mtamwita Fisadi Idriss Rashid, Mtamwita mwizi wa kesi ya Rada but we are responsible for the collapse of Tanesco. Alipotaka kupandisha bei ya umeme alipingwa vikali eti watanzania hawawezi kumbe kuna watu walikuwa hawampendi tu na alikuwa akiwabania maslahi yao. Haya sasa shirika linawafia mikononi mwenu na Engineer mnayemtaka (new CEO) sijui mna mawazo gani. Tujifunzeni kuheshimu fani za watu sio kila kitu siasa.
 
Mie bwana kwa huyu jamaa (Idriss Rashid) nitapingana na watu hapa JF kwa nguvu zote kwasababu sikubaliani na nyie mnyonge mnyongeni haki yake mpeni they guy is a good CEO na Tanesco wengi wanamlilia.
 
Mie bwana kwa huyu jamaa (Idriss Rashid) nitapingana na watu hapa JF kwa nguvu zote kwasababu sikubaliani na nyie mnyonge mnyongeni haki yake mpeni they guy is a good CEO na Tanesco wengi wanamlilia.

Haya mkuu tupe data! Kwa nini walimlilia? Lazima kuna sababu ambazo ziliwafanya wamlilie si bure, tujuze mkuu.
 
Mtamwita Fisadi Idriss Rashid, Mtamwita mwizi wa kesi ya Rada but we are responsible for the collapse of Tanesco. Alipotaka kupandisha bei ya umeme alipingwa vikali eti watanzania hawawezi kumbe kuna watu walikuwa hawampendi tu na alikuwa akiwabania maslahi yao. Haya sasa shirika linawafia mikononi mwenu na Engineer mnayemtaka (new CEO) sijui mna mawazo gani. Tujifunzeni kuheshimu fani za watu sio kila kitu siasa.

Kama unaamini kuwa Idrissa ni CEO mzuri unapaswa kuelewa pia kuwa CEO mzuri anaweka strategy nzuri, kwa maana hiyo hiyo kama Idrissa aliweka stragety nzuri na board of directors wapo palepale ni miujiza tu ingemfanya Eng Mhando afanye Tanesco ifilisike ndani ya kipindi kifupi tu tangu aingie madarakani. Ni vyema tuangalie tatizo la Tanesco nje ya Mhando/Idrissa au CEO Mhandisi vs CEO asiye mhandisi. Tuangalie nini role ya share holders, board of directors na management kwa upana wake. Pia ni vyema kuelewa matatizo ya utendaji katika Tanesco ni mwangwi wa matatizo jumla ya utendaji katika taasisi zetu nyingine. Kama mfumo wa elimu haufanyi kazi, mfumo wa afya haufanyi kazi na mifumo yetu mingine pia haifanyi kazi basi kwangu ningeshangaa kama Tanesco ingeweza kuwa taasisi ya kufanya kazi kwa ufanisi. Suluhisho ni ku-overhaul system nzima ya utendaji kazi katika nchi yetu. Yes I said it (If it is broken why not fix it?)
 
Kuna habari za ndani kuwa TANESCO imefilisika wala haikopesheki tena.source katibu mkuu wa wizara!kama kuna mwana jf aliye na data zaidi amwage hapa. Tukumbuke 8% only ya watanzania ndio wapatao umeme wa tanesco
TANESCO haijafilisika kama unavyosema! Inahitaji tu mwendeshaji aliye na uchungu na chi yake! Kwasasa 'connection' ni 14%. The sector is still booming!
 
Mtamwita Fisadi Idriss Rashid, Mtamwita mwizi wa kesi ya Rada but we are responsible for the collapse of Tanesco. Alipotaka kupandisha bei ya umeme alipingwa vikali eti watanzania hawawezi kumbe kuna watu walikuwa hawampendi tu na alikuwa akiwabania maslahi yao. Haya sasa shirika linawafia mikononi mwenu na Engineer mnayemtaka (new CEO) sijui mna mawazo gani. Tujifunzeni kuheshimu fani za watu sio kila kitu siasa.

Mkuu nakuunga mkono, siku kila kitu tunaingiza siasa jamani Dr. Rashid alitaka kujiuzulu kabla mkataba wake haujakwisha lakini Mhe.Rais alikataa ombi lake.

Ninachotaka kusema Dr. Rashid aliwabania wengi alipokuwa CEO ndio maana akaanza kusambaziwa habari eti naye fisadi mara sijui nyumba ili mradi tu wamchafue. But all in all he was the right person to be Tanesco CEO.

Tukiendelea hivi hata nchi itafilisika utasikia Tanzania haikopesheki tena!!! Wabongo..............nimenyayua mikono...............
 
Haya mkuu tupe data! Kwa nini walimlilia? Lazima kuna sababu ambazo ziliwafanya wamlilie si bure, tujuze mkuu.

Na ni wajinsia gani?maana kuna jinsia haitakiwi kulialia hata msibani unakaza roho...ukilialia tu unakuwa jinsia ya katikati ambayo bado haitambuliki Tanzania...sasa mtujuve
 
Likifa ili shirika itakuwa jambo la mbolea sana tuanze upyaaaaaaaa/
Lazima iwe halikopesheki kuanzia dowans,ricmond,IPTL
 
Haya mkuu tupe data! Kwa nini walimlilia? Lazima kuna sababu ambazo ziliwafanya wamlilie si bure, tujuze mkuu.

For the first in many years wakati wa uongozi wa Idrissa Rashid waliweza kubreak even katizame katika vitabu vyao vya pesa. Huo ulikuwa ni mwanzo mzuri wa shirika kujiendesha kifaida. Lakini aliweza vp kufikia hivyo ni kwasababu aliziba mianya ya kifisadi iliyokuwa ikiendelea pale Tanesco hadi kuelekea wizarani. akachukiwa na wengi mpaka vigogo ndio zikaanza fitna za kumtoa kwani alikuwa anaharibu maslahi ya wateule fulani. Wafanyakazi wengi wa Tanesco wanamlilia kwasababu aliwaboreshea mazingira ya kazi akaweka uwiano wa maslahi kutokana na utendaji na cheo cha mtu. Kuna watu Tanesco walikuwa hawajapandishwa mshahara muda mrefu (especially watu wa chini jamaa alikuja akawalipa malimbikizo yao na kuwapandisha mshahara) wakati watu wa juu kila baada ya miezi fulani walikuwa wanapandishwa mishahara. Kiufupi jamaa aliweka kila kitu mswano pale Tanesco jambo ambalo baadhi ya watu hawakupenda ndio zikaanza fitna.

Kuhusu maswala ya je kwani zile strategy alizoweka yeye si zipo mpaka leo hivyo na yeye amechangia katika kuanguka kwa Tanesco. Nakuomba usome vizuri maswala ya utawala bora board ndio inaweka misingi ya uendeshaji lakini kama umeangalia ndani Board inapropose na kuaprove maswala ya shirika ila ni kazi ya CEO kuweka long term strategy anapoingia katika shirika fulani. CEO yeye ndie behewa la train akiwa mbovu basi shirika linakuwa bovu akiwa mzuri na shirika linakuwa nzuri hivyo sikubaliani na wewe kabisa kuwa Idrissa amechangia kufilisika ila huyo wa sasa na board yake ndio wa kublame na sio Idrissa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom