Tanesco wasababisha hasara kubwa kiwanda cha Mwatex

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,753
15,227
Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha MWATEX amewachana viongozi wa Tanesco mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza bwana Amos Makala kwa kukisababishia hasara ya millioni 100 kwa siku kiwanda hicho kutokana na mgao wa umeme unaoendelea mkoani humo bila kufuata utaratibu!.

Mkurugenzi huyo amesema Tanesco wamekuwa wakikata umeme kwa zaidi ya mara tano kwa siku na kupelekea baadhi ya mashine kuungua.

View: https://youtu.be/QnZmd8l8P8s?si=BUtgKaZ5-dyr9xUB
 
Umeme wao una tabia za kuogopa viongozi wa Aina Fulani pia huwa haukatiki ukiwa unalinda ugali wa mtu mkubwa kwenye shirika.
 
Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha MWATEX amewachana viongozi wa Tanesco mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza bwana Amos Makala kwa kukisababishia hasara ya millioni 100 kwa siku kiwanda hicho kutokana na mgao wa umeme unaoendelea mkoani humo bila kufuata utaratibu!.
Huyo Makala mwenyewe hata kumeneji kibatari nyumbani kwake hawezi sembuse dude kubwa kama Tanesco
 
Umeme wao una tabia za kuogopa viongozi wa Aina Fulani pia huwa haukatiki ukiwa unalinda ugali wa mtu mkubwa kwenye shirika.
Kwanini wananchi tusiandamane kwenye hili mbona tupo kama misukule wabongo...Tulikuwa tukimsakama Makamba kaondoka kaingia kipenzi cha wasukuma yaleyale vitu vyetu vinaungua hii washa kata washa kata Uwanja wa ndege hawazimi viwanda vitupu Mvafala na kambi ya jeshi juu ila kila siku zima kata
 
Inaweza kuwa urithi na kuharibiana.
Ukifanya wanayofanya wao utaenda nyuma ya nondo.
 
RC anamfundisha mfanyabiashara namna ya kurun biashara yake huku akifanya biashara hiyo kwa miaka zaidi ya kumi..
 
Back
Top Bottom