TANESCO: Uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni

Huyu kalishwa matango pori tu maskini ya Mungu,kunguru wanakuraje nyaya za umeme?hakuna uwezekqno wa kunguru kupigisha short circuit ya nyaya za 33KV,sema Kama ataamua kupiga msamba!

Uwezekano wa kunguru kupigisha short ni mdogo sana,
Chief hsbari mbona iko wazi sana ? Siyo kunguru kwa dhati yake bali kwa vile anavyo okototeza na kuruka navyo kwa ajili ya shughuli zake.

Kunguru wanasabaisha sana mizinga mijini huko mpaka watu wasio jua masuala ya umeme hili jambo wanalijua, utawasikia tu wakisikia mzinga wanasema "Kunguru huyo kashapigwa".

Pili, vifaa vinavyofungwa siku hizi kwa ajili ya kutambua "fault" viko fasta sana kutambua fault, ndiyo maana unakuta ikitokea tu mzinga kidogo, umeme unakata, kisha ndani ya sekunde kadhaa unarudi, ukikatika zaidi ya mara mbili, kifaa kinakata umeme mazima na kina toa taarifa ya kuwataka wahusika waende ku clear fault.
 
Bado haileti maana..ili hizo nyaya zinazoletwa na kunguru kuweza kupigisha shoti ni ama ziweze kuungunisha waya mmoja na mwingine au zindondokee ndani ya transfoma na huko ndani ndizo zikasababishe short circuit....vinginevyo ni ngumu kunguru katua kwenye waya mmoja tu wa umeme na kipande kingine kidogo cha waya mdomoni mwake anasababishaje shoti ya umeme? haiingii akilini? na kwa tabia za kunguru hawajengi kiota kwenye waya labda transforma na hapo kwenye transforma kuna insulator ya kutosha kuzuia viwaya vidogo kuingia ndani yake na kweza sababisha ajali hiyo....atafute tu maelezo mengine ya kitaalam lakini sio kuwasingizia ndege hawa... daah kweli mbaazi akikosa maua...
Ni matukio ambayo nimeshuhudia. Siwatetei Tanesco. Sijasema kuwa hutokea kila siku, nimefafanua baada ya watu kubisha kuwa kunguru hawezi kusababisha shoti.
Kunguru anabeba waya mdogo lakini unaweza kuwa mrefu hata zaidi ya mita moja. Huwa wanabeba hata kwa kutumia miguu yao (mdomo hutumia kubeba mzigo mwepesi)
Nyanya wanazobeba kunguru sio hizi za line ya Tanesco, ni zile nyanya ndogo za kusukia mota za feni, pamoja na nyanya ambazo hutokana na kuunguzwa kwa matairi ya gari. Hizi ndio hugusanisha waya mmoja na mwingine na kusababisha shoti.
Hawajengi kwenye waya au transfoma, bali hutua kwa ajili ya kupumzika na mzigo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom