TANESCO: Uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,399
2,000
Meneja Uhusiano wa TANESCO Johari Kachwamba, amesema kuwa uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwani Kunguru hao wanachangia kuharibu miundombinu hususani nyaya za umeme.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 5, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, hii ni baada ya East Africa Radio kupokea malalamiko ya wananchi wengi kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yao hapa nchini.

"Kinondoni tuna tatizo la Kunguru kuathiri sana miundombinu yetu, tunatumia nyaya zenye magamba ya 'silver' ambazo zinaathirika sana na katika kutatua hili tumeanza kubadilisha nyaya, tunazoziweka sasa hivi hazitakuwa zinaathirika kiurahisi na Kunguru, ni tatizo linalotokea mara kwa mara na si sehemu ya tatizo kubwa ambalo tunaweza kusema watu wa Kinondoni wanashindwa kufanya kazi zao", amesema Johari

Aidha Johari ameongeza pia, "Uwepo wa Kunguru wengi wanaonyanyua nyaya kwenye madampo ya taka na kwenye viwanda vya nyaya vilivyoko maeneo mengi ya Kinondoni ikiwepo machinjio, inafanya Kunguru kutua kwenye nyaya za umeme wa msongo mkubwa (33KV na 11KV) na kusababisha milipuko kati ya waya na waya, pia wakitutua kwenye 'Transformer' husababisha milipuko na hizo nyaya wanazobeba kwa ajili ya kutengeneza viota vyao".

Akizungumzia kuhusu suala la gharama ya kuwekewa nguzo, Johari amesema kuwa, mwananchi hatakiwi kulipa gharama ya nguzo yoyote ya umeme, huku akiwasisitiza Watanzania kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya umeme ili kutoiathiri.

Kunguru.jpg
 

Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,413
2,000
Kuna siku nilikutana na fuso la chadema limejaa matrei ya mayai madogo madogo nikauliza ni mayai ya nini yale, wakaniambia ni ya kungulu yametoka ubeligiji wanayapeleka kwenye incubator la mbowe kutotolesha. Leo nimepata majibu
 

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,631
2,000
Meneja Uhusiano wa TANESCO Johari Kachwamba, amesema kuwa uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwani Kunguru hao wanachangia kuharibu miundombinu hususani nyaya za umeme...
Aiseeeee.

Semeni koma 🤓🤓🤓🤓
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,292
2,000
Tanesco imesema ndege aina ya Kunguru ndio chanzo cha umeme kukatikakatika katika wilaya ya Kinondoni.

Kunguru hao hula maganda ya nyaya na kwa wakati huu matengenezo ya ubadilishaji nyaya unaendelea.

Maendeleo hayana vyama!

cc: Mrangi Ova
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
8,059
2,000
Tanesco imesema ndege aina ya Kunguru ndio chanzo cha umeme kukatikakatika katika wilaya ya Kinondoni.

Kunguru hao hula maganda ya nyaya na kwa wakati huu matengenezo ya ubadilishaji nyaya unaendelea.

Maendeleo hayana vyama!

cc: Mrangi Ova


Huo ni uongo uliopitiliza, toka lini Kunguru akala maganda ya nyaya??
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,703
2,000
Meneja Uhusiano wa TANESCO Johari Kachwamba, amesema kuwa uwepo wa Kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwani Kunguru hao wanachangia kuharibu miundombinu hususani nyaya za umeme....
Huyu kalishwa matango pori tu maskini ya Mungu,kunguru wanakuraje nyaya za umeme?hakuna uwezekqno wa kunguru kupigisha short circuit ya nyaya za 33KV,sema Kama ataamua kupiga msamba!

Uwezekano wa kunguru kupigisha short ni mdogo sana,
 

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
3,811
2,000
Nimeambia niongee au kuandika nikikosea watanirekebisha, haya nirekebishe ili nisikosee tena sasa
😂😂😂😂 Nimekukubali aisee. Utajifunza ukiwa hivi.
Ulitakiwa useme ARE THEY SERIOUS?
kama ni kitendo mfano kuuumia yani ku GET INJURED ndio unapachika seriously.
Mfano...
HE WAS SERIOUSLY INJURED IN THE ACCIDENT.

DO YOU SERIOUSLY TRUST HIM?...sababu hapa trust ni kitendo aka verb.


Achana na wale ma slayqueen wanaosemaga SERIOUSLY?!!! Hua wanachapia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom