TANESCO: SGR haitokosa umeme, ratiba kutovurugwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema reli ya kisasa (SGR) haitokosa umeme wala kukwama kufanya kazi kwa sababu ya kukatika au kutokea hitilafu katika miundombinu ya umeme.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mhandisi wa Idara ya Mipango ya TANESCO, Lucas Magero, alipozungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Wiki ya Nishati yanayofanyika Viwania wa Bunge jijini hapo.

Alisema umeme utakaotumika kuendesha reli ya SGR utakuwa unajitegemea ukitoka kwenye gridi ya taifa wa kujitosheleza na kwa namna miundombinu yake ilivyowekwa hakutokuwa na uwezekano wa kushindwa kujiendesha au kukwama kutokana na kukatika umeme au hitilafu.

"Umeme utakaotumika kwa ajili ya reli ya SGR utatumia laini yake ambayo haitohusiana na matumizi mengine yoyote na namna laini hiyo ilivyotengenezwa, siyo rahisi kukatika umeme wala kupata hitilafu: Kwa hiyo, niwatoe wasiwasi wananchi," alisema Magero.

Aliongeza: "SGR haitokosa umeme baada ya kuanza kwa sababu miradi iliyowekezwa katika uzalishaji wa umeme ni mikubwa sana na tunakwenda kuzalisha zaidi ya kile kinachohitajika.

"Na ikumbukwe kuwa kila baada ya kilomita 50 katika mradi huu wa SGR kutakuwa na kituo cha kupozea umeme chenye uwezo wa kutumia megawati 16.

Kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora tuna vituo 11 ambavyo tunakadiria kwamba vitatumia megawati 176.

"Makutupora hadi Tabora tuna vituo vitano vya kupozea umeme, Tabora hadi Isaka vituo vitano, Isaka hadi Mwanza vituo vitano ambavyo makadirio yake ya kutumia umeme ni Megawati 416."

Alisema SGR ikikamilika itatumia umeme wa Megawati 1,000. Alisema tayari maandalizi ya miundombinu ya umeme katika mradi huo wa reli ya SGR yamefikia asilimia 100 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na kwa Morogoro hadi Makutupora ni asilimia 99.

Kwa upande wa Isaka hadi Mwanza alisema mkandarasi anatarajia kuanza kazi Juni mwaka huu wakati Makutupora hadi Tabora bado wako katika hatua ya upembuzi yakinifu.
 
Vizuri ila kama Uwanja Wa taifa Dunia nzima inatazama Mechi hagu umeme unakata then anything is possible .
 
Back
Top Bottom