SGR Isaka-Mwanza Yafikia Asilimia 44.25

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Isaka mkoani Shinyanga hadi Mkoa wa Mwanza urefu wa kilometa 341 ukijumuisha njia kuu na njia ya kupishana kwenye stesheni unazidi kushika kasi na hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 44.25.

Meneja mradi kipande cha tano cha SGR, Christopher Kalisti alisema wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Alisema kuwa kazi kubwa ya msingi katika mradi huo ni ujenzi wa tuta na kuwa hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 80 wakati mifumo mingine inayofuata juu ya tuta ikiendelea vizuri ikiwemo kutandika reli na kazi hiyo ime-fanywa kwa kilometa 24. Kalisti alisema kuwa wanaendelea kusimika nguzo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme pamoja na kupanda majani kwa ajili ya ulinzi wa matuta.

"Ujenzi wa madaraja kiujumla unaendelea vizuri, tuna mada-raja zaidi ya 600 yanayojumuisha madaraja kwa ajili ya kupitisha mifumo ya umeme, kupitisha mawasiliano, kupitisha wanyama, kupitisha binadamu, kupitisha magari, kupitisha treni ya zamani kiujumla inaendelea vizuri na tumefikia zaidi ya asilimia 60;" alisema.

Naye Waziri wa Uchukuzi, Profesa Mbarawa alisema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo na alitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa kwake kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mdeme alisema kuwa kutokana na mkoa huo kupitiwa na mradi huo wa SGR kama mkoa wamejipanga kuzalisha zaidi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na mifugo.
 
Afadhari imesogea maana hii Sgr imechelewa sana
 
Isaka hata mwaka ni km 341 umepima kutumia hatua za miguu ....mwanza shy km 168m,shy tu isaka hakuna km 100
 
Thibitisha humu hakuna wehu wenzenu

..Sgr imegawanywa mapande toka Dar mpaka Mwanza, na Kigoma.

..Na serikali ilieleza kipande cha Dar Moro kitaanza na kufuatiliwa na kipande kingine kuelekea Mwanza na Kigoma.

..Hakuna mantiki ya kujenga kipande cha mwisho wa reli, Isaka kwenda Mwanza, kabla ya kumaliza kipande cha kwanza, na vya katikati.

..Haileti mantiki kuanza ujenzi Isaka Mwanza wakati kipande cha Morogoro to Dodoma / Makutopora hakijaisha. Au Makutopora Tabora Nzega hakijaanza.
 
Kipande cha Dar hadi Dodoma kimefikia asilimia ngapi?
Lini kinafunguliwa kianze kitumike?
EHEHEHE!
Huko Dodoma umekwenda mbali mno. Anzia Dar - Moro!

Ujenzi wowote wa miradi wa aina hii mara nyingi huleta hasara tu badala ya faida.
Ndiyo maana waChina hawapendi kazi za namna hii. Rejea ujenzi wa SGR ya Mombasa Nairobi; au ile Expressway ya Mlolongo. Kazi inakwenda mbio na hukumbuki kuwa kulikuwepo na ujenzi. Hata mchango wa ujenzi wa miradi hiyo katika uchumi inakuwa na maana zaidi.
 
Isaka hata mwaka ni km 341 umepima kutumia hatua za miguu ....mwanza shy km 168m,shy tu isaka hakuna km 100
Acha ujuaji wa kijinga, soma vizuri na elewa vizuri bila kukurupuka, na hili ni tatizo kubwa la watanzania wengi wapumbavu.

341km ukijumuisha njia kuu na njia ya kupishana kwenye stesheni, ujenzi wa railway umbali unaesabika mpka zile kilometa 92 za kupishana sio kama barabara.
 
..Sgr imegawanywa mapande toka Dar mpaka Mwanza, na Kigoma.

..Na serikali ilieleza kipande cha Dar Moro kitaanza na kufuatiliwa na kipande kingine kuelekea Mwanza na Kigoma.

..Hakuna mantiki ya kujenga kipande cha mwisho wa reli, Isaka kwenda Mwanza, kabla ya kumaliza kipande cha kwanza, na vya katikati.

..Haileti mantiki kuanza ujenzi Isaka Mwanza wakati kipande cha Morogoro to Dodoma / Makutopora hakijaisha. Au Makutopora Tabora Nzega hakijaanza.
Wakubwa wakale wapi?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Acha ujuaji wa kijinga, soma vizuri na elewa vizuri bila kukurupuka, na hili ni tatizo kubwa la watanzania wengi wapumbavu.

341km ukijumuisha njia kuu na njia ya kupishana kwenye stesheni, ujenzi wa railway umbali unaesabika mpka zile kilometa 92 za kupishana sio kama barabara.
Mkuu wangu, twende nao polepole, nyumbu wana tatizo kubwa sana la uelewa. Kwanza huwa hawasomi kilichoandikwa, pili kuelewa kilichomo ndiyo shughuli sasa!
Twende nao mdomdo, tukiwaacha njiani watatusumbua baadae kuwarudia tulikowaacha.
 
Back
Top Bottom