Tanesco ni wizi chini ya viongozi wa CCM kuimaliza zanzibar 50.4 Bilion deni la kubandikiza.

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Wazanzibar wa leo sio wale wa 1964 walipinduliwa.

Kama ni kudaiwa Zanzibar haidaiwi billioni 50.4 na TENESCO , kwani ndio tupo kwenye Muungano huo wanaoutaka wao. Kuibeba Zanzibar na kuiwakilisha kwa Kheri na Shari. wakati wa madeni ya Zanzibar kuna Mikataba ya kibiashara, lakini ukija kwenye ugawaji wa ruzuku na mapato au Misaada inayopatiwa serikali ya Tanganyika kwa koti la Muungano hapa hakuna mikataba . bali kuna wewe KANCHI KADOGO TU utapata 0.5.
Sasa nakuja katika kupigiana hesabu ya madeni Tanganyika inadaiwa na Zanzibar tokea siku waliofanya MUUNGANO FACK 24.4.64. Siku ile ndio

Serikali ya Tanganyika ili ibiya Zanzibar mpaka hivi sasa naandika maoni haya basi serikali ya Tanganyika inaendelea kuidhulumu Zanzibar. Mfano. ABAAZANZIBAR katoa machache na mimi naongezea.

1. Balozi zote za Tanganyika (Tanzania???) wanapata faida ya utoaji Visa na Passport , kama Zanzibar ni Mshirika wa hii Tanzania ni faida gani imepata kwa muda wa miaka 47?

2. East African Community, ilipovunjika muawakilishi wetu alifanyiwa mazonge asihudhurie mkutano uliofanyika pale Nairobi. Mkutano huo ulikua ni wakugawana mapato kwa wakati huo tu Zanzibar ilipatiwa £ 1,32,000 kama sikosei.. Naomba mwenye rikodi aniandikie hapa ili Watanganyika wazione . Hizi pesa ndizo zile zilizokua zinatakiwa kila NCHI ifungue National Bank yake yaani ( Kenya , Uganda, Zanzibar na Tanganyika) . Muwakilishi kutoka Zanzibar hapa alikua ameshatiwa hambaroni na Serikali ya Tanganyika na Muwakilishi wa Tanganyika (nimemsahau jina) alisema pesa za Zanzibar ziingizwe kwenye Account ya Tanzania kwani tumeungana. Na aliikabizi barua ya Muungano FACK.

Kutoka siku hiyo U.Kingdom waliisaidia kila Nchi kufungua Nationala Bank yake na Tannganyika/ Tanzania ilifungua na Zanzibar ndio iliokua na pesa Nyingi kuliko Tanganyika. Jee Magao ya faida Zanzibar ilipewa kiasi gani? Haya sio yaanze kujadiliwa leo kama SAMIA SULUHU ANAVODAI... LAA haya yalikua yajadiliwe tokea 1965, Jee Zanzibar ikipiga hesabu pesa hizi hazitapita ile 50.4 billioni ya TENESCO?

3. Misaada inayopatikana kwa jina la Muungano, hapa kuna pesa, scholarship na pesa za mikopo kutoka Mataifa ya NJE kwani Tanganyika kila siku ni Maskini.Jee Zanzibar inafaidika kiasi gani? Ikiwa ni misaada Zanzibar inagaiwa 4.5 ya misaada lakini ikiwa ni deni Zanzibar hailipi 4.5 ya deni hilo na badala yake hulipa 50% ya Deni. Wakati wanaofaidika ni Tanganyika.

Mimi nawaaambia Serikali ya Tanganyika kama wanataka walipwe deni hili la umeme wangevunja Muungano kwanza au kuwa na Serikali TATU vyenginevo Wazanzibari ni Wataalamu zaidi wakujua haki zao na watazidai. Jee Serikali ya Tanganyika itailipa Zanzibar fidia hiyo?

2008 Kulikua na Mmarekani alitaka kuanzisha umeme wa Juwa na alikuja na Project Proposala yake. Wakati ule Mansoor alikua Waziri wa Umeme kama munavojua ndugu Wazanzibari mtu yoyote anaetaka kuanzisha biashara ni lazima akaombe kibali Tanganyika. Sasa Watanganyika walivojua kwamba huyu Mmarekani anania yakuinyanyua Zanzibar kinishati walimzungusha na alikaa Zanzibar mwaka mzima. Hakukipata kibali cha Project yake ya Solar Energy.

Jee haya sio maonevu na kukandamizwa kiuchumi na Mkoloni Mweusi ? Jee kama Wazanzibari wangeachiwa kuanzisha umeme wa juwa si ingepungua kuitegemea hiyo Tenesco? Munatuchokoza mara hii tutafikishana mbali.
 
Kwa mawazo yako unaona mmeibiwa, na bado ngoja tuvunje muungano kama mnavyoomba halafu tupandishe bei ya nishati hii ndipo mtajua mboga si ugali.
Umeme hu baba wala siyo kuni yakhe, mtulipe watanganyika.
Kama mwaona mwaibiwa fueni umeme wenu mbona umeme waweza fuliwa hata baharini
Mnataka tuwauzie bei ya Pweza. Mmetumia umeme toka mfanye mapinduzi na hamlipi kwa nini? Lipeni yaishe
 
unaonaje mazee
 
zanzibar diaspora ... hamjui maisha halisi ya mzanzibar... hivi lile tifu tifu kipindi kile nililokuwa naliona mzaledo kuhusu pemba ile kesi yao kujitenga na unguja imeishia wapi..?
 
zanzibar diaspora ... hamjui maisha halisi ya mzanzibar... hivi lile tifu tifu kipindi kile nililokuwa naliona mzaledo kuhusu pemba ile kesi yao kujitenga na unguja imeishia wapi..?
ile ikuja baada ya kuona wapemba wametengwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar,sasa imetiwa katika bin,tunachodai ni maslahi ya zanzibar tu,zanzbar diaspora, sovereign state of zanzibar
 
ile ikuja baada ya kuona wapemba wametengwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar,sasa imetiwa katika bin,tunachodai ni maslahi ya zanzibar tu,zanzbar diaspora, sovereign state of zanzibar
Kwanza niweke wazi kuwa muungano ukivunjika mie sitatokwa machozi. Lakini manununguniko yenu waZanzibari yako one sided. Mnaona kuonewa tu mnazifumbia macho faida. Kuna mwanasaikolojia mmoja alisema kuwa watu wakikaa kwenye mazingira ya uonevu kwa muda mrefu hatimaye hiyo hali uingia kwenye akili zao za ndani (subconscious) na kuwafanya waone maonevu kila maahali hata kama hali yenywe imeishabadilika. Naona hili ndilo linawasibu waZanzibari. Hayo mafuta yanayowapa kiwewe mna taarifa za kitaalamu za hali halisi? Niulize swali. Hivi nani alimlazimisha Bakhressa aje kuwekeza bara na si huko visiwani? Kuna watakaosema alisukumwa na kero za muungano. Ukweli ni kwamba mtu mwenye akili na hekima ya kutosha hatakosa kuona faida ya bara kwa Zanzibar. Zanzibar ina watu takribani milioni moja. Hivi ni muwekezaji gani atachagua kuwekeza Zanzibar badala ya soko kubwa la bara lenye watu zaidi ya milioni 40? Tumechoka na kelele bwana. Fanyeni maamuzi magumu tujue moja.
 
Kabla ya mapinduzi mwaka 1964 zanzibar ilikuwa ina uchumi mzuri tu ukitofautisha na nchi zote za africa mashariki,kama utaamini wewe kuna barua waliwahi kuandika waengereza Uk kuomba mkopo zanzibar,na kwa wakati huo zanzibar ilikuwa na population ya watu kama laki 2 mpaka 2.5 ,jiulize kwa miaka hio tulikuwa na kitega uchumi gani cha kufanya uchumi kuwa juu,hata kufikia muengereza kuja kuomba mkopo zanzibar ?

Zanzibar ki jografia ukiangalia imezungukwa na bahari,ina uwezo mkubwa wa kuwa vitega uchumi kuliko hata tanzania bara,musijidanganye na wingi wenu huo watu na ardhi,lakini mukashindwa hata kupewa panadol na serikali bure,lakini ukiangalia zanzibar ina iwezo wa kufanya free port,na tukavutiwa na wawekezaji wengi tu,kwa mfano nchi kama kenya,uganda,burungi,mafia,comorro,na sehemu nyengine za africa mashariki,wanaweza kutumia bandari ya zanzibar kwa kupitishia mizigo yao.

Jengine wawekezaji kama wachina,japan,dubai,tailand,na wengine wanaweza kuja kuweka biashara zao zanzibar ili kuweza kuwauzia wateja wao katika mwambao wa africa mashariki,kama unavyoona dubai,sio lazima sisi zanzibar tuwe na viwanda,kutokana na population yetu,kwa haya yote basi tutajitosheleza kwa ajira.

Jengine kama unakumbuka,zantel ilianzishwa zanzibar ,wakati walipotaka kuleta biashara yao bara waliiipigia vikali isije huko,lakini angalia sasa hivi eti mapato yake ambayo yanakusanywa yapo katika muungano zanzibar kuangukia patupu. Yote hayo ni choyo.

Huyo baharesa unae muona wewe akiondoka leo bara nani atapata hasara ? Na nyinyi wengewe,unajua watu wangapi ambao wamejipatia ajira hapo ? Ukiacha watanganyika,hadi uganda wamepata ajira,kenya,rundwa,acha zako wewe,huyo bakhresa aje leo zanzibar nakuapia katashuka kibiashara zaidi ya kupanda kwa sababu zanzbari ni kituo cha biasahra na yeye ni mfanyaji wa biashara mzoefu,na naaamini wateja wake watakuja zanzibar,na kwanini wasije ? Sisi tunatoka zanzibar tunaenda malasia kununua mchele iweje wao hapo pua na mdogo karibu tu ?

Mkuu naona huna hoja,zanzibar ikitoka leo ndani ya muungano basi tutapiga hatua haraka mno,na Sitta na Mizengo pinada wanaogopa mfumo wa serikali tatu kwa sababu wanajua zanzibar itapiga hatua haraka,kwa maana hiyo wazanzibari watafaidika na uchumi wao,na nyinyi watanga tanga la nyika,mutabakia mukilana wenyewe,kutokana viongozi wenu ni wezi,majambazi,hapo juzi tu jiulize bajeti yenu iliyopitishwa wewe imekugusa vipi ?

Maisha yako unalipia,maji,umeme,maji machafu,matibabu,elimu,public services zote unalipia,jiulize unafaidika vipi wewe ndani ya mfumo huo ? Nyinyi watanga la nyika,muna marasilimali kibao,mbona hamufaidki ? Wanaofaidika ni viongozi wenu majambazi,kila siku ma skendo ya mikataba mibovu.

AAAAAAAAAAMKAA KIJANA.

WAKATI UMEFIKA,SISI WAZANZIBARI,TUNAPIGANIA HAKI YETU,WALA HATUWACHUKII NYINYI,SISI TUKIFANIKIWA TUWAWEZA HATA KUWASAIDIA NYINYI KWA NINI TUSIWASAIDIE ? pigania haki yako na wewe ndani ya serikali ya muungano,moja ni utaifa wako,ambo ni tanganyika,pili bajeti ikuguse na wewe,kwani rasilimali zile za ngoro ngoro ni za watanzania wote sio za wabunge wala kikwete,wala pinda wala 6ta,wala ccm yoyote na zenu wenyewe.

ACHA KIBURI CHAKO WEEWE,MAISHA YAKO HUYAJUI NA HUJUI NINI UNAFANYA WALA UNACHOKIDAI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom