Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,650
- 16,731
Nachat gizani total power Blackout
Pale manyara kuna maji ya moto wenzetu kenya wanatumia kutengeneza thermo hydro power hata kama mradi utakuwa wa miaka 20 tungekuwa na umeme wa uhakika na bei rahisi
sasa hao wanao sema tz itakuwa nchi ya viwanda vitaendeshwaje bila umeme wa uhakika?
Unapotokea mgao, TANESCO imekuwa na uharaka wa kuelezea. Mara husemwa kuna matengenezo kwenye njia za umeme. Mara husemwa kuna hitilafu kwenye mitambo ya sehemu fulani. Mara husemwa kuwa kuna maboresho na kadhalika.
Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchemi Mramba aliuambia umma wa watanzania kuwa mitambo ya umeme wa gesi kutoka Mtwara imewashwa na hivyo umeme kuwa wa kutosha Dar es Salaam na kwingineko. Bado mgao wa umeme unaendelea kwenye jiji la Arusha na hata hapa jijini Dar es Salaam pamoja na kuwashwa kwa mitambo hiyo ya umeme wa gesi.
Nawauliza TANESCO, mgao huu wa umeme unaoendelea nchini Tanzania unatokana na nini tena?
Safi sanaSawa kabisa mimi kazi yangu itakuwa kuulinda Uzi huu ili watu kama lizaboni, zeMalcoporo, Gentamycine, jingalao na wengine kama hao wasiuchafue kwa matusi na kashfa zao.
Nilidhani ni sisi tu mtani kwetu ndio tunaadhibiwa na Tanesco, kumbe ni shida ya nchi nzima? Tumwajibishe nani kwa kadhia hii?