Ukiona umeme hakuna na mijitu inakazania #hapakazitu basi jua kua ni kazi zisizohitaji umeme kama Majungu, Umbea, Uchonganishi, Wizi, Ufitini etc
Yaani hii serikali ya Sisiem inachojua ni kupiga dili tu.............Tanesco wanashidwa kusema tu mashine zote hakuna mpya hata moja ni old painted machine watu washakula hela tanesco hawana kosa lolote wanashindwa wafanyaje coz serikali ndo mzigo. Naamini kabisa serikali ikisimama TAnesco itakuwa vizuri
Jamani watu wa tabata tuna kilio kikubwa mnoo.umeme usipokatwa asubuhi saa kumi na mbili hadi saa moja usiku , basi watakata saa kumi na mbili jioni hadi saa nane usiku . Ni mgao au ni nini? Hili swala la umeme linatuzidishia chuki kwa hii serikali ya ccm. Tukutane oct wandugu....
Natafuta kichinjio changu kiwa tayari kwa kazi ya October 25 Tanesco naona mnaniongezea hasira
Jamani tunapoilaumu tanesco tunakosea kabisa wa kuilaumu ni serikali na asio tanescoTanesco ni kama watabiri wa nyota maana kila siku wanakuja na story mpya.
Mie nieisha choka nao nymbani kwangu nimeweka solar kuondokana na hizi sarakasi za tanesco.
Miaka 50 ya UHURU bado tuanishi kama wanyama wa porini.
Unapotokea mgao, TANESCO imekuwa na uharaka wa kuelezea. Mara husemwa kuna matengenezo kwenye njia za umeme. Mara husemwa kuna hitilafu kwenye mitambo ya sehemu fulani. Mara husemwa kuwa kuna maboresho na kadhalika.
Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchemi Mramba aliuambia umma wa watanzania kuwa mitambo ya umeme wa gesi kutoka Mtwara imewashwa na hivyo umeme kuwa wa kutosha Dar es Salaam na kwingineko. Bado mgao wa umeme unaendelea kwenye jiji la Arusha na hata hapa jijini Dar es Salaam pamoja na kuwashwa kwa mitambo hiyo ya umeme wa gesi.
Nawauliza TANESCO, mgao huu wa umeme unaoendelea nchini Tanzania unatokana na nini tena?
hakuna maji mtera...gesi bado haijanyumbulishwa ili kuzalisha umeme..tanesco kuweni wazi..acheni kuwa watumwa wa wansiasa wasiosoma kama kina Nape na Kinana...mbona hamjiamini? elimu yenu inawasaidia nini?