TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
Unapotokea mgao, TANESCO imekuwa na uharaka wa kuelezea. Mara husemwa kuna matengenezo kwenye njia za umeme. Mara husemwa kuna hitilafu kwenye mitambo ya sehemu fulani. Mara husemwa kuwa kuna maboresho na kadhalika.

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchemi Mramba aliuambia umma wa watanzania kuwa mitambo ya umeme wa gesi kutoka Mtwara imewashwa na hivyo umeme kuwa wa kutosha Dar es Salaam na kwingineko. Bado mgao wa umeme unaendelea kwenye jiji la Arusha na hata hapa jijini Dar es Salaam pamoja na kuwashwa kwa mitambo hiyo ya umeme wa gesi.

Nawauliza TANESCO, mgao huu wa umeme unaoendelea nchini Tanzania unatokana na nini tena?
 
Nawauliza TANESCO, mgao huu wa umeme unaoendelea unatokana na nini tena?
Niko kwenye foleni ya kusubiri majibu ,maana hata huku ughaibuni zenji hatuna umeme sasa!sijui hawa cousin wa TANESCO ZECO kama wanamajibu!
 
Wametoa sababu kwamba mitambo inaendelea kuwashwa tuvumilie mpaka Oct 20, sasa sijui Mtwara imegeuka NASA maana hiyo mitambo inayoendelea tu kuwashwa mpaka Oct 20 itakua sio ya Gesi peke yake kutakua pia na mitambo ya Ku launch rockets
 
Kwa ufupi,nimewauliza baadhi ya wanafanyakazi wa Tanesco kuhusiana na hii issue wakaniambia huko kuwashwa kwa mitambo,mara matengenezo ni sababu tu ya kudanganya wananchi.Shirika lipo ktk hali ngumu kifedha kujiendesha kutokana na CCM kuchota pesa kwa ajili ya kampeni zake zinazoendelea kwa sasa.
 
hakuna maji mtera...gesi bado haijanyumbulishwa ili kuzalisha umeme..tanesco kuweni wazi..acheni kuwa watumwa wa wansiasa wasiosoma kama kina Nape na Kinana...mbona hamjiamini? elimu yenu inawasaidia nini?
 
Unapotokea mgao, TANESCO imekuwa na uharaka wa kuelezea. Mara husemwa kuna matengenezo kwenye njia za umeme. Mara husemwa kuna hitilafu kwenye mitambo ya sehemu fulani. Mara husemwa kuwa kuna maboresho na kadhalika.

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchemi Mramba aliuambia umma wa watanzania kuwa mitambo ya umeme wa gesi kutoka Mtwara imewashwa na hivyo umeme kuwa wa kutosha Dar es Salaam na kwingineko. Bado mgao wa umeme unaendelea kwenye jiji la Arusha na hata hapa jijini Dar es Salaam pamoja na kuwashwa kwa mitambo hiyo ya umeme wa gesi.

Nawauliza TANESCO, mgao huu wa umeme unaoendelea nchini Tanzania unatokana na nini tena?

Jana majira ya 20:00hrs nilianzisha uzi TANESCO SINA HAMU NAO. Katika uzi huo, nilishangaa na kuhoji kwa nini kama Chama tawala cha CCM kikiwa na mikutano ya live ambayo wanalenga umma wa tanzania ufuatilie kupitia runinga na redio umeme unashinda kuanzia asubuhi hadi jioni saa 18:00hrs? Nilihoji

1. Je mitambo inapona ccm wakiwa live na wakiwa offline inakufa tena?
2. Je umeme unakuwa wa kutosha ccm wakiwa live lkn wakiwa na mikutano ya kimya kimya mitambo inakuwa na umeme mdogo hivyo kulazimisha uwepo wa mgao?
3. Tumesikia utetezi kuwa mitambo ya gas iliyowashwa ina nguvu sana hivyo kulazimu kuiwaisha taratibu ili bomba zisipasuke. Je kukiwa na live coverage ya ccm, umeme wa kuwasha tanzania nzima unatoka wapi?
4. Na kwa nini mara baada ya kumaliza mikutano yao ya live coverage, umeme unazimwa hadi usiku wa manane na asubuhi hata fursa ya kusikia magazeti tunanyimwa?

Nasikitika kuwa uzi huo tangu jana modes hawajauruhusu kuwa hewani lkn kupitia uzi wako nilichoandika jana nimekiweka hapa.

Kifupi mie naamini ni janja ya TANESCO na seriakali ili waweze kuiba kiasi kikubwa cha pesa. Itakumbukwa migao ya umeme huambatana na uwashaji wa mitambo ya dharura inayolipwa pesa nyingi sana kwa siku.

Naamini kamati za bunge za 2016, zitakuja na taarifa moja ya ufisadi wa kutisha. tusubiri tu muda utimie
 
Mkuu mbona TANESCO hawajatutangazia mgao wa umeme, pia mitaa ya kwetu umeme upo.
 
Ni lazima tukubaliane TANESCO hawausiani na vyama vya siasa, pia tanesco sio chama cha siasa.
 
Kwa ufupi,nimewauliza baadhi ya wanafanyakazi wa Tanesco kuhusiana na hii issue wakaniambia huko kuwashwa kwa mitambo,mara matengenezo ni sababu tu ya kudanganya wananchi.Shirika lipo ktk hali ngumu kifedha kujiendesha kutokana na CCM kuchota pesa kwa ajili ya kampeni zake zinazoendelea kwa sasa.

Mkuu umewauliza wafanyakazi wapi, shirika linamsemaji wake...... kwa nini usimuulize kupata ukweli.

Sio kila mfanyakazi ni msemaji wa TANESCO.
 
hakuna maji mtera...gesi bado haijanyumbulishwa ili kuzalisha umeme..tanesco kuweni wazi..acheni kuwa watumwa wa wansiasa wasiosoma kama kina Nape na Kinana...mbona hamjiamini? elimu yenu inawasaidia nini?

[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye Mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]
 
Jana usiku huku Mbezi beach walikata....wakaurudisha tena usiku huo huo halafu wakaukata tena na asubuhi hii ndo wameurudisha tena.

Kama kuna yeyote anayeamini kuwa tatizo la umeme wa uhakika limepatiwa ufumbuzi wa kudumu basi mtu huyo atakuwa mjinga kupita maelezo.
 
hakuna maji mtera...gesi bado haijanyumbulishwa ili kuzalisha umeme..tanesco kuweni wazi..acheni kuwa watumwa wa wansiasa wasiosoma kama kina Nape na Kinana...mbona hamjiamini? elimu yenu inawasaidia nini?

[FONT=Calibri,Arial,Helvetica,sans-serif][FONT=Calibri,sans-serif]kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.[/FONT][/FONT]
 
hyo gesi gani inawashwa muda wote huo.ni ushuzi au maana tumechoka sasa

kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi ambayo ilisababisha upungufu wa umeme kwenye Mikoa yote iliuongwa kwenye gridi ya taifa. Baada ya kuanza kuwasha mitambo hiyo Septemba 19, 2015 upungufu huo umeanza kuimarika kwa baadhi ya mikoa. Mitambo yote ya gesi iliyokuwa imezimwa haiwezi kuwashwa mara moja kwa kuwa kitaalam itafyonza gesi haraka na kuleta vacuum kwenye bomba lenyewe. Kumbuka bomba hili ni kubwa la nchi 36 na urefu wa kilometa 487. Hivyo Tanesco tunawasha mtambo mmoja baada ya mwingine ili kumonitor presha ya gesi kwenye bomba. Kazi hii itakamilika mwishoni mwa Oktoba ambapo tutakuwa tumewasha mitambo yote jumla ya megawati 335.

Mkuu Koleba ndiye Tanesco? Ha ha ha
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom