TANESCO Mbeya: Je kuna Electric Surge au Line ya Meta Referral Hospital imezidiwa?

Habari kwa wana JF, ni matumaini yangu muwazima wa afya na mnaendelea vizuri.

Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu. Kwa upande wa Jiji la Mbeya, hii line ya Meta Referral Hospital kuna tatizo limetokea. Mita za umeme zinatoa sauti ya ku 'click' na kwa kuwaka na kuzima (Inaonyesha Units ulizonazo na kutoweka, hii ni kwa energy meters zile za LUKU za kwanza kabisa).

Watu wako kwenye njia panda, wachache wameamua kukaa nje ya nyumba zao kwakuogopa madhara ya umeme. Mpaka sasa Tanesco haijatoa official statement yoyote kwa line hii. Si kwamba ni lazima, ila at least kwa tatizo kama hili wajaribu hata kuwatumia wenyeviti wa mtaa wa maeneo husika kuhusu mambo yanayotokea kama kuna mushkeri kwenye mitambo ya umeme ya eneo husika.

Kwa wale watu ambao hawako nyumbani hali ya huko kwenye majumba yao itakuwaje?, kwa maana kuna walioacha vifaa vyao wazi/viko on.

Juzi juzi na mimi nilikuwa mhanga wa kuunguliwa na Power Supply ya CPU yangu baada ya umeme kuzidi.Sasa shida hiko wapi kama wanaona line ina matatizo si waseme mapema kuliko kuuchuna. By the way kuhusu tatizo la Kuungua kwa power supply siwezi kulaumu sana kwakuwa mimi mwenyewe nilizembea kutokununua Stabilizer.
ngoja niwafate tanesco
 
Hapo mbeya kuna line ya umeme inayotoka chunya hamna siku umeme haujakatika hamna tofauti na makongo juu dar
 
Back
Top Bottom