Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Tanesco kupinga malipo ya Dowans mahakamani | Send to a friend |
Monday, 10 October 2011 20:28 |
Mwandishi Wetu SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), leo litawasilisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ombi la kutaka kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuilipa Dowans Holidings. Uamuzi wa kuilipa Dowans uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kupata baraka za Mahakama Kuu chini ya Jaji Emilian Mushi. Mahakama Kuu iliridhia tuzo ya ICC hivi karibuni ya malipo ya fidia ya fedha kwa Dowans ambayo inaitaka Tanesco kulipa kiasi cha Sh111 bilioni kwa kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo. Awali, Tanesco ilikuwa ikidaiwa Sh94 bilioni lakini baada ya kukata rufaa na kushindwa deni hilo liliongezeka riba ya asilimia 7.5. ICC iliamuru Tanesco kuilipa Dowans Holdings SA(Costa Rica) na Dowans Tanzania kutokana na kukatisha mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya pande hizo mbili mwaka 2008. Mmoja wa kundi la wanasheria wa Serikali anayeshughulikia suala hilo, Dk Eve-Hawa Sinare alisema jana kuwa ombi hilo la kutaka kukata rufaa litafuatana na ombi jingine la rufaa ya kutaka kuzuia uamuzi wa malipo hayo usitekelezwe kwanza kabla ombi hilo kusikilizwa. Dk Sinare ambaye pia ni mmoja mawakili katika kampuni ya Rex Attoneys alisema hutua itakayofuata baada ya ombi hilo ni kuomba nakala halisi za mwenendo wa kesi hiyo, hukumu na tuzo iliyotolewa kwa ajili ya kukata rufaa waliyokusudia katika Mahakama ya Rufani. Alisema kuwa Tanesco walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kwa sababu waliamini kuwa mahakama hiyo haikuangalia mambo muhimu na yenye utata kisheria katika kesi hiyo yenye manufaa ya umma. |
hapa mi naona wabongo ni watu wa stori tu matendo hamna kitu..
Tanesco ni mabazazi hao. Hebu someni kipengele cha 14.3 a-c cha mkataba wao na Dowans walipokubaliana kuwa kama itatokea kukorofishana au kutoelewana basi shauri lao lifikishwe kwenye baraza la usuluhishi la biashara la kimataifa na maamuzi ya baraza hilo yatakuwa ni ya mwisho na hakuna kufikisha mambo hayo mahakamani.
Sasa wanapinga nini? au ndo kuwapiga changa la macho waDanganyika?
Poleni sana.
Hawa mawakili wa Rex Arttoney ni wahujumu uchumi wakubwa na nashangaa kuona Tanesco wanaendelea kuwa nao. Ni wao waliowashauri kuvunja mkataba wakisema hakukuwa na tatizo kwa kuwa kampuni (Dowans) ilikuwa feki na ni hao hao wakaiombea hiyo kampuni feki mkopo benki wakisema ni kampuni safi. Ni hao hao waliopeleka utetezi hafifu ICC ili Tanesco washindwe kesi, leo hii wanasema wanapinga malipo hayo mahakamani. Kweli huu ni mchezo wa kuigiza.Ni wazi huu ni mradi wa watu wakubwa serikalini.
Umenena kuhusu hao magamba wa sheria hapa nchini.