Tanesco kupinga malipo ya Dowans mahakamani

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,427
911,172
Tanesco kupinga malipo ya Dowans mahakamani
Send to a friend
Monday, 10 October 2011 20:28


Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), leo litawasilisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ombi la kutaka kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuilipa Dowans Holidings.

Uamuzi wa kuilipa Dowans uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kupata baraka za Mahakama Kuu chini ya Jaji Emilian Mushi.

Mahakama Kuu iliridhia tuzo ya ICC hivi karibuni ya malipo ya fidia ya fedha kwa Dowans ambayo inaitaka Tanesco kulipa kiasi cha Sh111 bilioni kwa kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo. Awali, Tanesco ilikuwa ikidaiwa Sh94 bilioni lakini baada ya kukata rufaa na kushindwa deni hilo liliongezeka riba ya asilimia 7.5.

ICC iliamuru Tanesco kuilipa Dowans Holdings SA(Costa Rica) na Dowans Tanzania kutokana na kukatisha mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya pande hizo mbili mwaka 2008.

Mmoja wa kundi la wanasheria wa Serikali anayeshughulikia suala hilo, Dk Eve-Hawa Sinare alisema jana kuwa ombi hilo la kutaka kukata rufaa litafuatana na ombi jingine la rufaa ya kutaka kuzuia uamuzi wa malipo hayo usitekelezwe kwanza kabla ombi hilo kusikilizwa.

Dk Sinare ambaye pia ni mmoja mawakili katika kampuni ya Rex Attoneys alisema hutua itakayofuata baada ya ombi hilo ni kuomba nakala halisi za mwenendo wa kesi hiyo, hukumu na tuzo iliyotolewa kwa ajili ya kukata rufaa waliyokusudia katika Mahakama ya Rufani.

Alisema kuwa Tanesco walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kwa sababu waliamini kuwa mahakama hiyo haikuangalia mambo muhimu na yenye utata kisheria katika kesi hiyo yenye manufaa ya umma.

 
[h=4]Comments [/h]


0 #9 Kilasara N. Mamremi 2011-10-11 11:03 Maoni yangu ni kwamba mitambo hii ya Dowans itaifishwe.

Ikumbukwe kwamba mitambo ya Richmond na baadae Dowans iliingizwa nchini na mafisadi: kwanza wakidai mitambo ina uwezo ulio-prove ni feki na pili imetugharimu sana na ku-disrupt uchumi na maendeleo ya nchi yetu.

Haijajulikana wazi wazi rasmi kwamba mmiliki au wamiliki wa Dowans ni nani, na walikuwa na uhusiano wa namna gani na wale viongozi wa Tanzania waliojadiliana nao juu ya kupatikana kwa hii mitambo.

Kutaifishwa kwa mitambo hii itakuwa ni ishara kwamba Tanzania inarudia kuwa nchi ya watu waadilifu, wasiohongeka na walio na uzalendo wa dhati.
Quote









0 #8 Ngosha 2011-10-11 10:54 Jaman watanzania hebu kila mmoja atafakari ni nani katufikisha hapa tulipo! automatically utakuja kuhitimisha kuwa Serikali legelege ya CCM ndo imetufikisha hapa. Mimi naomba tu wazilipe hizo pesa hapo ndipo watawatambua watanzania si wakuchezea!
Quote









0 #7 Gabriel 2011-10-11 10:22 Kila siku tunasoma habari kutoka nchi jirani kama Kenya, Zimbabwe, Rwanda, nk. kwamba kiongozi fulani kapandishwa lupango kujibu mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka yaliyolisababis hia taifa kuingia hasara na hata kuaibika mbele ya umma wa kimataifa. Serikali yetu inatyia aibu kwa unyonge. Ona akina Mahalu; ona akina Mramba, Karamagi, Chenge, Msabaha, Lowassa, Ngeleja na hata Jairo jeuri. Hawa watu wametufikisha mpaka gizani lakini wenye jukumu la kuwawajibisha hawaachi kuvaa suti walizohongwa na kurukia kwenye ndege iliyonunuliwa kifisadi inayotumia shillingi million 10 kwa saa hewani, kwenda kupanda mabembea ughaibuni. Wezyi wanafahamika na Segerea siyo mbali. Kwa nini tusiwahifadhi huko wakati tukifilisi mali yao kuilipa Dowans?
Quote









0 #6 Crucifix 2011-10-11 09:30 Nyinyi Rex Attorneys ni ma[NENO BAYA] na mafisadi tu. Kama ni muziki wa kisheria mlipaswa kuucheza London kwenye mahakama ya kimataifa na sio Tz kwa sababu hapa hakuna kesi bali ni kuridhia yale yaliyoamriwa ICC; na Tanzania ni member wa ICC so hakuna kuleta ubishi. Rex mnaitetea tanesco huku mkipokea pesa za Dowans na kuwawakilisha katika masuala ya mikopo! Wewe Eva Sinare unataka kumdanganya nani?
Quote









0 #5 O.T 2011-10-11 09:13 Hizi ni propaganda na yote haya ni matokeo ya watz wengi kuwa [NENO BAYA]. Mofkhaz can't even do sh**t when a few crazy a**holes r mesin' up out mamaland?
Quote









0 #4 mkurugenzi 2011-10-11 08:52 lazima walipe kwani wameshindwa kesi kusema hatulipi ni kujidanganya kwan mitambo tuliagiza sisi wenyewe na tukaisimamisha sisi wenyewe, lazima tujue kuwa ile ni biashara ya mtu.
Quote









+1 #3 Wilbard 2011-10-11 07:17 Fanyeni mfanyavyo ila tusilipe deni. Mkishindwa na deni likiongezeka ni juu yenu na hao waliowashauri. Nyinyi mlioingia na kuvunja mkataba na washirika wenu (wenye magamba) mtauza nyumba,viwanja n.k ili mlipe
Quote









+1 #2 ibrahim yahya 2011-10-11 07:17 SERIKALI INATAKA KULIPA DOWANS,TANESCO HAITAKI KULIPA.VIJANA JIUNGENI NA CHADEMA KUITOA CCM MADARAKANI.HICHI CHAMA KISIFIKE 2015 HAO NDO TATIZO.
Quote









+1 #1 Mossad 2011-10-11 06:43 C.umamaye zenu Tanesco na Rex attoney, wacenge wakubwa nyie siku zote mlikuwa wapi?
Quote







Refresh comments list
 
ping-pong games in the offing......but one intent is clear Tanesco and her ccm bosses can't wait to pay Dowans billions if not trillions..........knowing they will also pocket plenty of dirty cash..........
 
hapa mi naona wabongo ni watu wa stori tu matendo hamna kitu..

ni kweli kabisa.........................wamezoea danganya toto sana....................
 
Tanesco ni mabazazi hao. Hebu someni kipengele cha 14.3 a-c cha mkataba wao na Dowans walipokubaliana kuwa kama itatokea kukorofishana au kutoelewana basi shauri lao lifikishwe kwenye baraza la usuluhishi la biashara la kimataifa na maamuzi ya baraza hilo yatakuwa ni ya mwisho na hakuna kufikisha mambo hayo mahakamani.

Sasa wanapinga nini? au ndo kuwapiga changa la macho waDanganyika?

Poleni sana.
 
Hapo Uganda M7 kamuweka lupango aliyekuwa swahiba na makamu wake je hapa Tanzania presidaa wetu anaweza kufanya hayo MAAMUZI MAGUMU
 
wakati jaji mushi anahukumu madai ya Tanesco na sirikali alizingatia makubaliano ya Tanesco na Dowans kwamba maamuzi ya icc ni ya mwisho hapatakuwa upande wowote kukata rufaa dhidi ya maamuzi yatakayofikiwa.mimi sidhani kama rex wana jipya zaidi ya kuendeleza ufisadi.watanzania tuungane na wana harakati twende barabarani tudai haki yetu.
 
Tanesco ni mabazazi hao. Hebu someni kipengele cha 14.3 a-c cha mkataba wao na Dowans walipokubaliana kuwa kama itatokea kukorofishana au kutoelewana basi shauri lao lifikishwe kwenye baraza la usuluhishi la biashara la kimataifa na maamuzi ya baraza hilo yatakuwa ni ya mwisho na hakuna kufikisha mambo hayo mahakamani.

Sasa wanapinga nini? au ndo kuwapiga changa la macho waDanganyika?

Poleni sana.

Hawa mawakili wa Rex Arttoney ni wahujumu uchumi wakubwa na nashangaa kuona Tanesco wanaendelea kuwa nao. Ni wao waliowashauri kuvunja mkataba wakisema hakukuwa na tatizo kwa kuwa kampuni (Dowans) ilikuwa feki na ni hao hao wakaiombea hiyo kampuni feki mkopo benki wakisema ni kampuni safi. Ni hao hao waliopeleka utetezi hafifu ICC ili Tanesco washindwe kesi, leo hii wanasema wanapinga malipo hayo mahakamani. Kweli huu ni mchezo wa kuigiza.Ni wazi huu ni mradi wa watu wakubwa serikalini.
 
Hawa mawakili wa Rex Arttoney ni wahujumu uchumi wakubwa na nashangaa kuona Tanesco wanaendelea kuwa nao. Ni wao waliowashauri kuvunja mkataba wakisema hakukuwa na tatizo kwa kuwa kampuni (Dowans) ilikuwa feki na ni hao hao wakaiombea hiyo kampuni feki mkopo benki wakisema ni kampuni safi. Ni hao hao waliopeleka utetezi hafifu ICC ili Tanesco washindwe kesi, leo hii wanasema wanapinga malipo hayo mahakamani. Kweli huu ni mchezo wa kuigiza.Ni wazi huu ni mradi wa watu wakubwa serikalini.

Umenena kuhusu hao magamba wa sheria hapa nchini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom