Naandika hii kwa mara ya mwisho naona umeamua kuamisha magoli na kutoka kwenye swali lenyewe. Swali kuu hapa ni nchi kuwa na kampuni binafsi zenye ushindani wa bila kutegemeana wa kuzalisha umeme mkubwa na kuuza independently na mteja kuwa huru kuchagua. Hili ndo swali la msingi la mleta uzi
Katika quotes zote ulizoleta umeshindwa kuthibitisha hili. Nchi zote ulizotaja, mosi, wanatumia mfumo mmoja wa usambazaji moja, pili wanauza umeme kwa maeneo husika (respective service area), kwa maana nyingine kampuni hizo ndogo ambazo ni privately owned zinazalisha umeme mdogo wa kuuza eneo dogo ambalo amepewa na serikali na mteja wa eneo hilo hana namna nyingine zaidi ya kutumuia umeme wa muuzaji wa hapo.
Na kama kampuni zote zinatumia mfumo mmoja wa usambazaji basi hazipo independent katika usambaji wake hivyo hitilafu ikitokea haijalishi umeme unatoka kwa nani wote mtakosa.
Privately owned kampuni zipo nyingi, hata bongo kampuni za kuzalisha umeme za solar zipo kibao ila sio za kiwango cha kuzalisha umeme wa kuendesha nchi nzima zenyewe na zote huwa zinazalisha kisha kuingiza umeme kwenye grid ya taifa.
Vivyo hivyo kwenye maji, unaweza kuwa na kisima chako au kijiji kikawa na kisima chake ila haliwezi kuja kampuni kuanzisha vyanzo vyake na kujenga mabomba yake tofauti na system iliyopo kwenye nchi husika. Wanachoweza kufanya ni kujenga vyanzo na kuingiza maji kwenye mkondo wa taifa, au kusambaza kwenye eneo lao walilopewa dhamana.
Baada ya kusema hayo, nimemaliza.