TANESCO itafutiwe mshindani wa kibiashara?

Sasa mi naishi Germany
Kama upo huko you should know better. Makampuni ya nishati hayawezi kuwa huria kama yalivyo makampuni ya simu. Hili haliwezekani duniani kote

Kikubwa wanachoweza kufanya ni decentralization, generation afanye huyu, transmission afanye yule na distribution afanye mwingine. Ila wote wanategemeana.

Kampuni moja haliwezi weka mifumo yake tofauti na ile iliyopo nchini. Hata German na Japan ni hivyo, wote wanaingiza umeme kwenye grid ya taifa. Au unapewa eneo maalum la kuhudumia
 
Wewe haupo usa ungekuwepo usingeandika ujinga eti duniani kote hakuna hizo company. Njia ya muongo ni fupi
Basi nipo Ombokoro maana unataka kubisha hata mahala nilipo.
 
Mashirika yote ya seeikali yakipata mshindani yatakufa mapema sana,

Serikali inajua hilo ndio maana hawataki kudhubutu kuruhusu atokee mshindani.

Rejea: shirika la TTCL, Dawasco.
kesho unahitajika ofisini kutoa maelezo

hahahah
 
Nilipata habari kwamba mtumiaji wa umeme anayetumia unit chini ya 70 anapaswa kubadirishiwa tariff. Nikaenda ofisi za TANESCO kwa ajili ya kubadilishiwa. Kwanza mapokezi hayakuwa mazuri kwani walinipotezea muda.

Huduma ya kutolewa ndani ya dakika 15 niliipata kwa zaidi ya saa moja, kujaza fomu tu. Muhudumu ananiambia eti network iko slow. Network ilikuwa inahusika vipi kwenye kujaza fomu iliyoko mezani?

Baada ya kujaza fomu niliambiwa niondoke wao watalishughulikia suala langu. Hadi naandika hapa sijajulishwa lolote na nimeamua kuendelea kutumia utaratibu wa zamani. TANESCO kumbuka kuwa TTCL iko hivi kwa sababu zamani wahudumu wake walijifanya miungu watu.

Baada ya kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma ya mawasiliano hakuna mtu wa kuwabembeleza tena TTCL. Ni kwanini mnashindwa kujifunza kutokana na makosa yalotendwa na taasisi kama ya kwenu?

Leo hii nawapigia simu wanaendelea kunipa kauli za hovyo hovyo! Hakika mmenikera. Eti mtu anatumia line ya huduma kwa wateja lakini anakuwa na kauli chafu

UPDATES:
Tutor B said;

NATAMANI TANESCO WAWE KAMA TTCL

Mwaka jana Nov. 2018 nilienda ofisi za Tanesco wilaya ya Ilemela ili kubadilishiwa matumizi ya umeme kwa sababu natumia chini ya Unit 60 kwa mwezi.

Kwa ujumla huduma zilikuwa mbovu sana kana kwamba wana kisa na mimi. Nilijaza fomu then nikaambiwa nikitaka kuweka umeme tena sitatumiwa token hadi pale nitakaorudi ofisini kwao. Nikakubali na kuondoka.

Hadi naandika hapa nimeishaweka tena umeme na sijaona badiliko lolote.

Udhaifu wao:
Kwanza; Wanafanya kazi kwa kujisikia kwa sababu hawajapata mshindani. Nawashauri wajifunze kwa kile kilichotokea kwa kampuni ya simu pale makampuni ya simu za mkononi yalipoanza kutoa huduma.

Pili; wanauza nguzo wakati nguzo ni mali yao. Iweje wamuuzie mteja nguzo alafu waitumie kwa ajili ya wateja wengine pasipo kumfidia yule alouziwa nguzo?

Sipendi kuandika mengi ila kwa ujumla huduma za Tanesco ni hovyo kabisa kwa sababu hawana mshindani.
 
Haya wamepeleka umeme vijijini - kila mteja akinunua umeme anachangia REA - ni nani alishirikishwa kukubali kukatwa hela hizo? Majuzi nilienda kijijini - hakuna kitu umeme wanafikisha sehemu wanazotaka wao.
 
Hao wana nchi wanakata bila kuambiwa, sasa huo ni ujambazi wa mchana kweupe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unalalamika tu mambo ambayo huyaelewi.

Tanesco hawauzi nguzo, meter wala nyaya. Gharama unazolipia wakati wa kuunganishiwa Service Line ni gharama za huduma (service) na sio materials (nguzo, nyaya, seals, meter n.k).

Unapopewa quotation yako (mkataba wa malipo) ukiusoma mpaka mwisho mambo yote yameainishwa hapo na unaipokea quotation yako na kwenda kulipa bank ina maana umekubaliana na T&Cs.

Shida kubwa inakuja kuwa wabongo wengi hatupendi kusoma na ndio maana huwa tunakubali mikataba ambayo hatuijui na baadae kuja kupata tabu na kunung'unika bure kisa tu hukusoma mkataba wenye maneno chini ya 200.
 
Alafu hawahoji ni kwa nini wanakatwa bila kuambiwa?

Jambo jingine wanapeleka umeme unaoweza kusababisha majanga ya moto wakati jeshi la zima moto haliwezi kuhudumia huko. Nayaona majanga ya moto yakiwakumba hawa wakazi wa vijijini.
 
Mkuu unalalamika tu mambo ambayo huyaelewi.

Tanesco hawauzi nguzo, meter wala nyaya. Gharama unazolipia wakati wa kuunganishiwa Service Line ni gharama za huduma (service) na sio materials (nguzo, nyaya, seals, meter n.k).

Unapopewa quotation yako (mkataba wa malipo) ukiusoma mpaka mwisho mambo yote yameainishwa hapo na unaipokea quotation yako na kwenda kulipa bank ina maana umekubaliana na T&Cs.

Shida kubwa inakuja kuwa wabongo wengi hatupendi kusoma na ndio maana huwa tunakubali mikataba ambayo hatuijui na baadae kuja kupata tabu na kunung'unika bure kisa tu hukusoma mkataba wenye maneno chini ya 200.
Mkuu pamoja na utetezi wako lakini Tanesco inatoa huduma chini ya kiwango huo ni ukweli mchungu!
 
Ndio lakini pamoja na hayo pia kutokuwa na uelewa kwetu sisi raia nako kunachangia kuonekana huduma zipo chini ya kiwango
 
Mkuu unalalamika tu mambo ambayo huyaelewi.

Tanesco hawauzi nguzo, meter wala nyaya. Gharama unazolipia wakati wa kuunganishiwa Service Line ni gharama za huduma (service) na sio materials (nguzo, nyaya, seals, meter n.k).

Unapopewa quotation yako (mkataba wa malipo) ukiusoma mpaka mwisho mambo yote yameainishwa hapo na unaipokea quotation yako na kwenda kulipa bank ina maana umekubaliana na T&Cs.

Shida kubwa inakuja kuwa wabongo wengi hatupendi kusoma na ndio maana huwa tunakubali mikataba ambayo hatuijui na baadae kuja kupata tabu na kunung'unika bure kisa tu hukusoma mkataba wenye maneno chini ya 200.
Kama ni kusoma .. dada mimi nasoma sana na ni mfuatiliaji mzuri sana.
1. Lalamiko langu ni kutobadilishiwa tariff - limeandikwa wapi kwenye mkataba kwamba ni mpaka mtandao uwepo ndo wanakubadilishia? Ina maana tangu Nov. 2018 mtandao haujawahi kuwa sawa ili nihudumiwe?

2. Kwenye mkataba iliandikwa wapi kwamba wateja wa mjini wawachangie wateja wapya wa vijijini kila wanaohitaji huduma ya Luku?

3. Ni kwa nini wasisambaze nguzo pote ili wateja wote wakawa na ghalama moja? Nikihitaji huduma wanakuja kuangalia kama nguzo iko karibu ... ikiwa mbali wanaweka gharama ya nguzo kwenye quotation yao .. lakini wakitaka kuzitumia nguzo hizo kwa ajili ya wateja wengine (majirani) - hawanirudishii chochote - eti nguzo ni mali yao. Mali yao vipi wakati niliilipia.

Tatizo wewe inawezekana unafanya kazi humo ndo maana unawatetea.
 
Back
Top Bottom