DOKEZO TANESCO inakata Tsh 6,000 kila ukinunua umeme mwisho wa mwezi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

kasumbiresa

Member
May 25, 2023
18
4
TANESCO ilisema imeondoa service line lakini Cha kushangaza nimenunua umeme kwa miezi miwili wananikata Tsh. 6000, sijajua shida Nini, Ina maana siku hizi TANESCO haifuati miongozo ya wizara inafuata mambo yake?

Unajua Kuna vitu vingine tunaweza tukasema Magufuli alikuwa Bora upande wa matumizi ya rasilimali zetu ila mama anajisahau kama Rais.
 
Binafsi hali hii ilinitokea, niliweka Elfu 11, nikapewa unit 14, mita yangu ni matumizi makubwa.

Kawaida Elfu 11, kwa mita za matumizi makubwa ni unit 32! Nilifadhaika sana''.
 
52363490eef9e6254098657fd5c2ef7c.jpg
 
TANESCO ilisema imeondoa service line lakini Cha kushangaza nimenunua umeme kwa miezi miwili wananikata Tsh. 6000, sijajua shida Nini, Ina maana siku hizi TANESCO haifuati miongozo ya wizara inafuata mambo yake?

Unajua Kuna vitu vingine tunaweza tukasema Magufuli alikuwa Bora upande wa matumizi ya rasilimali zetu ila mama anajisahau kama Rais.
Halafu ina samehe bilioni 60 Zanzibar, kweli hili shirika ni shirika donor (dona kantre)
 
Bado umeme wenyewe una VAT ni bora watangaze Tanesco kuchangiwa kuliko hali inavyokwenda umeme tuu Nchi masikini unaonekana ni anasa harafu mkikaa majukwaani mnasema tupo Uchumi wa ngapi sijui,hakuna Nchi yenye Uchumi nafuu raia wake wakawa wanaletewa gharama za hovyo hovyo za viwanja kwenye Umeme au Maji huo ni wizi...
 
Tanzania Nchi yangu ukikaaa huku tanesco ukikaaa kule Vodacom ukiacha Salio kwenye cm imepitiwa yote wanakuunganisha na mahuduma usiyoyaitaji
 
Hawa jamaa wanakera sana, Mimi nyumba yangu ilikaa kama mwaka mmoja bila kuwa na mpangaji, mwezi wa tatu nilipata Mpangaji ambaye alilazimika kuweka 15000 ndipo akapewa token, zile token zikaisha mwezi huu wa tano, akaweka 3000 ili anunue umeme ikagoma, ikabidi apige huduma kwa Wateja, wakamwambia eti bado kuna deni la Tsh. 12000 la Mwaka 2021.

Aliponishirikisha nami nikawapigia, nikaona maelezo yao siyaelewi, nikaawauliza mbona kukiwa na deni huwa hatupewi token mpaka deni lilipwe? Kama kulikuwa na deni la nyuma 12000, iweje alipoweka 15000 mwezi wa tatu apewe tokeni ingali deni halijalipwa? Baadae mara waseme niende "TRA" sasa kutoka hapa nilipo hadi hizo Ofisi za "TRA" nauli ni sh. 5000, ikabidi nimwambie tu yule mpangaji aweke tu hiyo pesa tutakatana kwenye Kodi ya nyuma, kiufupi hili suala la kuweka Kodi ya jengo kwenye LUKU linakera sana.
 
Tanzania Nchi yangu ukikaaa huku tanesco ukikaaa kule Vodacom ukiacha Salio kwenye cm imepitiwa yote wanakuunganisha na mahuduma usiyoyaitaji
Hatuna wa kutusemea Mkuu, tumebaki kama Yatima ndani ya Nchi yetu, huku wao wakipongezana kwa kulamba asari.
 
TANESCO ilisema imeondoa service line lakini Cha kushangaza nimenunua umeme kwa miezi miwili wananikata Tsh. 6000, sijajua shida Nini, Ina maana siku hizi TANESCO haifuati miongozo ya wizara inafuata mambo yake?

Unajua Kuna vitu vingine tunaweza tukasema Magufuli alikuwa Bora upande wa matumizi ya rasilimali zetu ila mama anajisahau kama Rais.
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tunaomba namba ya mita kwa ufuatiliaji zaidi.^OK
 
Back
Top Bottom