Darasa: Hivi ndivyo mwananchi anayetumia zaidi ya unit 75 kwa mwezi anavyoumia na gharama za umeme wa TANESCO

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Unaweza kushangaa kuona wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wew ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1

Iko hivi Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4) Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122,

Wakati watumiaji waliowengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 Kama sikosei

Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000
Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000

NAWEZAJE KUA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1)

Kama ni nyumba yakupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima
Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa,Tv,Friji,Pasi n.k

Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304
Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo (Energy Saver) Japo bei yake iko juu ukilinganisha na Taa zenye Wats kubwa Kwa mfano huu huu ukanunua Taa zenye Wats 5 kila moja za nje Nne na taa 8 za ndani zenye Wats 3 kila moja
Jumla ya taa 12 zitakua na Jumla ya Wats 44 tu.

Maana yake utakua umepunguza jumla ya Wats 250 upande wa Taa tu lakini idadi ya Taa imeendelea kua ni ile ile. Mtu mwenye taa moja ya Wats 40 akiwasha nawew ukawa taa zote 12 Matumizi yenu yatakua hayana tofauti kubwa
Mwisho kabisha matumizi yako ya Umeme yakiwa chini ya Unit 75 kwa miezi mitatu mpaka Sita Mfululizo unatakiwa kuandika Barua unaiadress kwa Meneja wa TANESCO wa Ofisi uliyoko Karibu nayo Kuomba kubadilishiwa Kutoka Tarrif 1 kwenda Tarrif 4.

Siku ukitumia Zaidi ya Unit 75 kwa mwezi utarudishwa Tariff 1.

Ahsanteni!

Tafadhali Usisahau kulike na kushare page hii
 
Itabidi nifanye huo utaratibu. Nauziwa units 70.2 kwa Tzs 25,000 na matumizi yangu kwa miezi 6 iliyopita hayazidi hizo units kwa kila mwezi. Pia TANESCO wangeondoa huo urasimu wa kuandika barua, mfumo wa LUKU uko computerized, hizo transitions zingefanyika automatic.
 
Unaweza kushangaa kuona wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wew ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1

Iko hivi Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4) Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122,

Wakati watumiaji waliowengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 Kama sikosei

Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000
Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000

NAWEZAJE KUA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1)

Kama ni nyumba yakupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima
Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa,Tv,Friji,Pasi n.k

Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304
Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo (Energy Saver) Japo bei yake iko juu ukilinganisha na Taa zenye Wats kubwa Kwa mfano huu huu ukanunua Taa zenye Wats 5 kila moja za nje Nne na taa 8 za ndani zenye Wats 3 kila moja
Jumla ya taa 12 zitakua na Jumla ya Wats 44 tu.

Maana yake utakua umepunguza jumla ya Wats 250 upande wa Taa tu lakini idadi ya Taa imeendelea kua ni ile ile. Mtu mwenye taa moja ya Wats 40 akiwasha nawew ukawa taa zote 12 Matumizi yenu yatakua hayana tofauti kubwa
Mwisho kabisha matumizi yako ya Umeme yakiwa chini ya Unit 75 kwa miezi mitatu mpaka Sita Mfululizo unatakiwa kuandika Barua unaiadress kwa Meneja wa TANESCO wa Ofisi uliyoko Karibu nayo Kuomba kubadilishiwa Kutoka Tarrif 1 kwenda Tarrif 4.

Siku ukitumia Zaidi ya Unit 75 kwa mwezi utarudishwa Tariff 1.

Ahsanteni!

Tafadhali Usisahau kulike na kushare page hii
Kuna jambo bado umesahau. Umeme wa Tanesco unakuja low votage. Kama umeme uko low ina maana current huwa kubwa, hivyo mita hukimbia na hapo ndipo tuna pigwa
 
Nchi ya kibolizozo sana hii.ina maana wanatushawishi tuwe na matumizi madogo ya umeme,ilhali umeme ndo kila kitu kwenye dunia ya sasa.nakumbuka tuliambiwa tutaanza kuuza umeme nje kutokana na kuwa na surplus sasa sjui hilo suala limeishia wapi.
 
Umeme bado ni janga la nchi yetu.. Umeme ni ghali mno mnoooooo.. Umeme umekuwa kama anasa katika nchi yetu... Mh. Rais akiwa Kinyerezi Gas Plant akifungua umeme wa Gas 240 MW alisema wazi bila kuficha umeme ni ghali mno mnoooo na akasema upungue bei mara tu watakapofungua Gas plant nyingine za Megawatts nyingi zaidi nadhani mwakani, umeme ni ghali mno mnoo Tanzania.. Hata ukitumia energy savers inasaidia kidogo sana huwezi tumia 75 units kwa mwezi, labda uwe maskini fukara wa kutupa..
 
Kuna jambo bado umesahau. Umeme wa Tanesco unakuja low votage. Kama umeme uko low ina maana current huwa kubwa, hivyo mita hukimbia na hapo ndipo tuna pigwa
Hapo bingwa umeanza kuzama kiumeme zaidi, ingawa wengi ni wajuvi wa mambo humu na pengine wamepiga piga fizikia sana, lakini kukuta mtu anashindwa kuhusianisha hiyo nadharia na hali halisi si jambo la kushangaza. P=VI (ideal)
 
Kuna jambo bado umesahau. Umeme wa Tanesco unakuja low votage. Kama umeme uko low ina maana current huwa kubwa, hivyo mita hukimbia na hapo ndipo tuna pigwa
Mkuu nadhani kuna jambo umekosea kuwaza... For AC current voltage imewekwa costant ni 240v na kinachovary ni current tu... There is no low voltage or variation/flactuation of voltage... Ukitokea voltage iwe ina flactuate jua ndio mambo ya kuunguza vitu ndani...
P=IV where V is constant =240v for Tz.
Power consumption ni current variation....
All equipments are using 240v but they differ in current....
Mfano taa zinatofautian heat and light dispation but voltage ni constant e.t.c
 
Wadogo hao saiv hawapo hebu tuwekee ushahdxa risit za hao wadogo. Mimi sina hata feni na napata unit 28 kwa 10000.
 
wenzio tume shashtuka tumefunga solar panel na 3k inverter umeme wa tanesco ni supportive document
 
Hiyo tariff 4 imewekwa kwa ajili ya watu masikini, ambao umeme wanautumia kwa vitu basic kabisa kama kuwasha taa na kunyoosha nguo mara moja kwa wiki. Na hasa ililenga watu wa vijijini.

Hiyo tarif sio kwa mtu wa kawaida, I mean una taa za ulinzi, friji inawaka muda wote, kunyoosha nguo kila siku, na vitu vya umeme kama tv kuwaka muda wote na mambo kama hayo. Ilikua lengo la serikali kusubsidize watu masikini ili wao pia waweze kupata umeme kwa matumizi yao ya kawaida.

Hizo tarifu ziko kwa mujibu wa sheria ya umeme ya mwaka 2008.

Tusipende kulaum kila kitu, tufuatilie taarifa.
 
Thread Nzuri
Ila Moderator Wanaweza Kuiunganisha Na Nyingine Ambayo Ipo Jukwani Muda Mrefu Sana Na Ina Michango Mingi Sana Ya Members

Pia Kuna Member Anasema Tanesco Ni Wasumbufu Yaani Unakuta Mtu Ana Vigezo Vyote Ya Kuunganisha Kwenye Tarrif D1 (4)
Ukifika Tanesco Na Barua Unaambulia Tabu Nenda Rudi Nenda Rudi
Kuna Jamaa Yangu Kaanza Yombo Tanesco Kapeleka Barua Akaambiwa Ngoja Wafuatilie Meter Yake Kama Imekidhi Vigezo

Wakakuta Ina Vigezo Vyote Tena Alichelewa Kuiomba Hiyo Huduma
Akapewa Tarehe Alipokwenda Tena
Akaambiwa Ngoja Wawasiliane Na Temeke Baadaye Akaambiwa Atulie Tanesco Watakuja Kukagua Meter Nyumbani Kwake Hadi Kesho Kimya
 
Tanesco sasa hivi hawataki kuwaunganisha wateja kwenye hiyo tarrif 4. Wanahofia mapato kushuka zaidi
Mimi nimekidhi vigezo na masharti lakini wamenisumbua hadi nimeamua kuacha kufuatilia
Mkuu
Hii Ni Kweli
Nina Jamaa Yangu Kaambulia Usumbufu
Njoo Kesho Mara Sijui
 
Mkuu nadhani kuna jambo umekosea kuwaza... For AC current voltage imewekwa costant ni 240v na kinachovary ni current tu... There is no low voltage or variation/flactuation of voltage... Ukitokea voltage iwe ina flactuate jua ndio mambo ya kuunguza vitu ndani...
P=IV where V is constant =240v for Tz.
Power consumption ni current variation....
All equipments are using 240v but they differ in current....
Mfano taa zinatofautian heat and light dispation but voltage ni constant e.t.c
Ikitokea umepima voltage kwenye source ukakuta inasoma 180V hiyo utaielezea vipi kama sio low voltage?
 
Kwanini kuwe na kuandika barua kuomba kurudishwa T4 na kurudishwa T1 iwe "automatic" bila maombi ya mteja?
 
[QUOTEno titimunda, post: 26686817, member: 261362"]Nchi ya kibolizozo sana hii.ina maana wanatushawishi tuwe na matumizi madogo ya umeme,ilhali umeme ndo kila kitu kwenye dunia ya sasa.nakumbuka tuliambiwa tutaanza kuuza umeme nje kutokana na kuwa na surplus sasa sjui hilo suala limeishia wapi.[/QUOTE]
Logic ni kwamba yote hayo wao wanataka ila wana changamoto ya nishati ya kutosha.
 
Mbona sio lazima kuandika barua! We tafuta mfanyakazi wa Tanesco mpe 30k anakufanyia hiyo kazi. Mimi kuna jamaa nilimpa 30k akaniambia atanitumia namba niingize kwenye luku meter yangu. Baada ya kama masaa mawili nikapokea sms ina namba kama 20 then ok afu unaingize tena namba nyingine ukibofya ok kitu na box.

Mpaka leo nakula mema ya nchi.
 
Back
Top Bottom