Habari wakuu,
Kwa wiki nzima sasa Tanesco wamekuwa wakileta umeme mdogo kwenye baadhi ya maeneo hapa Dar kiasi kwamba kwa sisi ambao tunatumia fridge guard unakuta haiwezi kuruhusu umeme kuwasha friji kwa sababu umeme ni mdogo na kupelekea vitu vilivyohifadhiwa ndani ya friji kuanza kuharibika. Hivyo hivyo ukiwasha vifaa vingine kama feni unaona havina nguvu kabisa.
Pia kumekuwa na washa, kata nyingi, yaani umeme unakatika na kurudi ghafla.
Tanesco kuweni serious, kama hamuwezi kusambaza umeme unaotosha ni bora kuzima tu kuliko kusambambaza umeme mdogo ambao utapelekea kutuharibia vifaa, ukichukulia kwamba hivi vifaa ni gharama sana.