Jafo: Vingunguti, Tandale na Buguruni pavunjwe pajengwe Maghorofa

Jafo: Vingunguti, Tandale na Buguruni pavunjwe pajengwe Maghorofa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,394
Reaction score
18,878
Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.

Huwa nashindwa kuelewa hawa wanasiasa kama kweli wanajua wanachokifanya. Badala ya kudili na matatizo ya msingi kabisa ya wananchi, wao wanakimbilia kufanya vitu kwa kuwaringishia wageni. Shida ya maji na umeme tu bado inatusumbua taifa zima halafu tunaongelea kupendezesha jiji sijui kwa faida ya nani. Eti huyu naye walikuwa wanampa nafasi ya kuwa rais wa nchi
 
Ana hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etc
 
Hata ukosefu wa mipango miji ni matatizo ya msingi ya nchi yaliyosababishwa na CCM
 
i dont understand, mbunge wa kisarawe anataka magorofa yajengwe dar? kwani huko kisarawe matatizo yameisha hadi aingilie mambo ya mkoa mwingine? kwa nini asijishighulishe zaidi na mambo ya jimboni na mkoani kwake kwanza? ...
 
Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.

Imagine huyu anayetoa hiyo hoja alikuwa waziri!! Anaposhauri serikali ijenge hayo maghorofa angekuwa pia anashauri jinsi serikali itakavyopata hizo pesa za kuwalipa hao wazaramo wenzake na za kujengea hayo maghorofa!!
Samia kajenga yale magøhorofa pale KAWE , je yamependezesha mji au ndio ilikuwa njia ya kutafuta fedha za kuhonga wananchi kwani majengo yale ni sub standard na hayaendani na gharama wanayosema wametumia kuyajenga!! Wizi mtupu.
 
Tukijaaliwa uzima na Allah ndani ya miaka 100 ijayo patajengwa Inshaallah

Mh. Seleman usitie shaka kwa hili
 
Ana hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etc
hilo swali hua najiuliza kila siku shida ipo wapi ya kuamua kwamba ujenzi holela sasa marufuku, maana muda unakwenda na ujenzi holela unaendelea tu kwenye miji mpya inayochipukia, na wakati watu wa mipango watu ardhi wapo
 
Huyo alikuwa Waziri wa TAMISEMI, atuambie wakati ni waziri alifanya nini kutekeleza hayo ambayo leo anataka yafanyike?

CCM wanatulaghai kwamba wakijazana wenyewe bungeni wanaweza kuikosoa na kuishauri serikali ila ni utapeli mtupu.
 
Buguruni HAPO vingunguti, huwa pananisikitisha SANA, KWA NINI hao WATU wasilipwe pashushwe ghorofa za KUFA MTU mambo mengine tuweke siasa pembeni hiyo njia ni potential SANA kuelekea airport, taifa, kariakoo, hapapaswi kiwa hivyo, pavunjwe pajengwe kisasa Niko na WEWE jafo, ASANTE kunwakilisha kaka
 
Mada imetawaliwa na chuki za kisiasa. Njia mojawapo ya kuondoa malazi holela ni hio. Kubomoa vinanda vibovu viluvyokaa bila mpangilio na kujenga makazi ya jumuia huku kila aliekuwa na nyumba hapo anapewa nyumba moja.
factos
 
Maghorofa yajengwe alafu unalipwa na froor ya chin mnapewa
 
Back
Top Bottom