TAMKO LA UVCCM na Mwelekeo wa Kisiasa Nchini

Eh yani wanataka watajwe wamiliki wa richmönd? Richmond si haipo. Yani wanaacha kuöngelea kuwataja wamilik wa dowans, i dont trust them!
 
Ila wanajamvi tuwe makini sana na hawa jamaa, bado siamini kama kweli wapo kwa ajili ya ukombozi wa kweli.... Nahisi baada ya kuona vijana wamechoshwa na mizengwe ya chama chao sasa wanatumia janja hiyo kuteka akili zao.... tuwe makini sana, tusijejikuta tumetegeka kwa mitego ya kipuuzi na baadae kuja kujilaumu :amen:
Nakubaliana na wewe 100%, hii ni janja ya nyani, siwaamini CCM na matawi yao hata siku moja, SIDANGANYIKI!
 
kwa hiyo unasema UVCCM wala CCM hawastahili kusema serikali isiilipe DOWANS? nani anayestahili sasa?
Umekazania CCM wamesema wasiilipe Dowans wakati Dowans ni JK ambaye ni mwenyekiti wa CCM unaakili kweli, ni sawa na kutuambia CCM imesema isiilipe CCM kama huo si unafiki ni nini, kama wamedhamilia kweli watuambie nani mmiliki wa Dowans na si kuja na matamko ya kinafiki.
 
Nimesikia na kuona toka taarifa ya habari tbc1. Vijana wa ccm wamechachamaa. Madai yao ya kuwekwa bayana suala la DOWANS, Bodi ya mikopo na nidhamu ya serikali ni ya msingi sana. Swali ni kuwa huu ujasiri asili yake wapi? May be the last straw of jk to salvage the cupsized ship. Tungoje tuone
 
Quinine na yeye!!!!
Achana na mimi hujui siasa zinavyokwenda ukirushiwa madongo unakimbilia kulia lia kwa kina Invisible kuwa unatukanwa tuache sisi tuliozoea kurushiwa madongo, mtu akininyea mbovu mimi namharishia kichwani haendi mtu kwa mods.
 
hata mie nimeona, inaomekana movie ndo inaanza nini...leta popcorn/bisi
 
janja yao wamesoma mbowe anapeleka hoja bungeni wanajaribu kuzuga ili wengine wasiendelee kujipanga kuwashughulikia , mbowe we mbele kwa mbele mpk kieleweke
 
Wakuu mnaweza msiamini kile ninachokipost hapa sasa hivi, lakini ukweli kwa mara ya kwanza leo UVCCM Taifa wametoa tamko zito lililosomwa na katibu mkuu wa taifa ndugu Shigela wameonesha wazi kuchoshwa na ccm na leo ndio wametaja kazi za uvccm ni nini, wamempa angalizo kali JK kwamba hawawezi tena kuvumilia kuangalia nchi inavyozidi kuangamia, na wamesisitiza kimya chao kilikuwa kina maana ya NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK. kwahiyo wamesisitiza hawajakurupuka.
Najitahidi kulipata hilo tamko niliweke hapa jamvini maana ndio limetoka kusomwa jioni hii.

My take: sasa naona ukombozi wa kuirudisha nchi yetu mikononi mwetu upo karibu kuliko vile nilivyotarajia.

Nijuavyo mimi UVCCM inandeshwa kwa remoti na RIZ 1 kweli na yeye kausishwa ,au ndo tunapigwa changa la macho...?
 
Hata km siipendi ccm, huo ni utovu wa nidhamu. Mtoto huwezi kumkoromea mkubwa hadharani. Kwa nini wasiyaongee kwenye vikao vyao
 
Umoja wa vijana Wa CCM Taifa,Leo wametoa tamko kwa vyombo vya habari kupitia kamati kuu ya Utendaji wa UVCCM
-WANAITAKA SERIKALI ISIILIPE DOWANS kwasababu mmiliki halali wa Richmond iliyoiuzia mitambo Dowans hajulikani,Na kamati ya Bunge ilitoataalifa kwa uma kuwa Richmond ni kampuni hewa,Vilevile kesi ya Dowans imeendesha kisiri mno bila wananchi kujulishwa,iweje leo wajulishwe kulipa?
-WAME ITAKA SERIKALI KUIPINDUA Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwasababu imekuwa haitoi fedha za wanafunzi kwa wakati,kitu kinachopelekea migomo ya kila siku.
-Mwisho Wamewataka MAWAZIRI WA SERIKALI(CCM) waache kurumbana hadharani kwani hii inaleta sura mbaya kwa jamii na inaonyesha hawana vikao vya pamoja kuhusu mambo ya serikali.

Source.Taarifa ya Habari leo usiku,(TBC,ITV)
 
Achana na mimi hujui siasa zinavyokwenda ukirushiwa madongo unakimbilia kulia lia kwa kina Invisible kuwa unatukanwa tuache sisi tuliozoea kurushiwa madongo, mtu akininyea mbovu mimi namharishia kichwani haendi mtu kwa mods.

Hahahahaahahah
 
Nijuavyo mimi UVCCM inandeshwa kwa remoti na RIZ 1 kweli na yeye kausishwa ,au ndo tunapigwa changa la macho...?

mkuu... amini usiamini hali ni mbaya sana sisiem sasa hivi... imeshindwa kujitawala kabisa.., kinachojiri kwa haya ya sisiem ni ukweli kwamba hali ya kifedha ni ngumu sana ndani ya chama... wana madeni makubwa sana ya uchaguzi... chama kina genge kubwa la mamba wanaofugwa na wanaosubiri kulishwa bure... makada wote wa sisiem si wafanya biashara...wala hawana shughuli wana tegemea pesa za chama... hali ni mbaya sisiem hina biashara...vitega uchumi vya chama vimekosa hadhi ya kiuchumi... watu hawapangishi majengo ya sisiem kwa sbabu ya kashfa nyingi za ndani ya chama... kikubwa ni kwmba mianya mingi ya wizi na ufisadi serikalini inadhibitiwa sasa na watanzania wapenda nchi... chama cha mapinduzi kimekuwa ni adui mkubwa wa wafanyakazi wa serikali, wakiwemo wa vyombo vya dola.... unategemea nini..? wakati umefika... matumbo yana njaa... walozoea kula bure sasa wana haha... hawa vijana kuongea hivi ni kutafuta kula ya bure iendelee ndani ya chama cha kijani
 
Let me assure you guys, hata kama yatatolewa matamko yote duniani hakuna hata mtu mmoja atazuia mabadiliko makuu ya kisiasa na uongozi nchi hii. Too bad and too late for any who is not pure in heart to catch the flight! Watu watatafuta mchawi kila kona na kudhania wengine vibaya....mchawi ni Mungu wa wanyonge walio wengi TZ wakiweza kumkamata ndo watasimamisha haya mageuzi. I wrote my prophesy during easter greetings in JF 2008 and repeated with a vision in 2009. Watu wakaendelea kuoa na kuolewa, kula na kunywa kama kawaida. Sasa mvua inanyesha milango ya safina imefungwa ndo wana kurupuka. sorry bad timing!
 
Hawa vijana hawana lolote zaidi ya uhuni. Wanafanyiana unafiki,yaani pale ni one mistake inakula kwako.ni vita ya ulaji na madaraka. Sioni jipya ndani mle. Mathalani tamka lao la leo ni ukosefu nidham kwa Baba zao. Haiingii akili na haikuwa kutokea katika ccm tangu nilipoijua,jumuiya mojawapo ikawa na sura tofauti na maamuzi ya chama. Kwa ufupi ninaamini mfadhili wa uvccm mmojawapo ni RA na mwenyekiti wa bodi ya udhamini ni EL, leo wajitutumue kukemea DOWANS? Uhuni huo.
 
Back
Top Bottom