Tishio la Waasira na Tuhuma za UVCCM dhidi ya CHADEMA: BAVICHA Yatoa Tamko Kali...

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Wadau hili ni Tamko la Bavicha kujibu tishio la waziri wa mahusiano na uratibu Steven Wassira kukifuta chama cha Chadema na Tuhuma za katibu mkuu wa uvccm martin shigela.

TAARIFA KWA UMMA
UTANGULIZI:Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) linapinga tamko lililotolewa na UVCCM kupitia Katibu Mkuu wake Martin Shigela kwenye vyombo vya habari tarehe 28 na 29 Agosti 2012 za kuhusisha mauaji yaliyotokea Morogoro tarehe 27 Agosti 2012 ya kijana Ally Hassan Singano (Zona).BAVICHA inakemea pia kauli zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) tarehe 31 Agosti 2012 za kuhusisha CHADEMA na siasa za umwagaji damu na inawataka vijana kujiandaa kwa hatua zaidi iwapo Serikali itaifuta CHADEMA.Aidha, BAVICHA imepokea taarifa kutoka Morogoro kuwa baadhi ya vijana wake wameandikiwa barua na serikali ngazi ya mkoa kuwa wanaitwa kuhojiwa na tume ya kuchunguza mauaji na inatoa agizo kwa vijana wote wa CHADEMA kutokwenda kuhojiwa na tume hiyo iliyoundwa na mkuu wa mkoa ambaye ni sehemu ya viongozi wanaotuhimiwa kushawishi polisi kukiuka makubiliano na kusababisha mauaji.

KAULI ZA UVCCM NI MWENDELEZO WA MADAI YA UONGO YA MUKAMA NA CCM NA NI KUWEWESEKA BAADA YA DR SLAA ‘KUANIKA' MIPANGO YAO HARAMU YA KUTUMA VIJANA WAKE WENYE SILAHA KUVURUGA MAANDAMANO NA MIKUTANO YA CHADEMA

BAVICHA inatambua kwamba propaganda chafu hizo za UVCCM ambazo pia zimedai kuwa vijana wa CHADEMA waliingiza silaha kwa wingi Igunga ni mwendelezo wa siasa chafua ambazo zilifanywa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama katika uchaguzi huo kwa kudai kuwa CHADEMA iliingiza magaidi na makomandoo kutoka nje ya nchi, uongo ambao alishindwa kuuthibitisha mahakamani na hivyo kuchangia katika mahakama kubatilisha ushindi wao haramu katika uchaguzi huo.BAVICHA inafahamu kwamba UVCCM imetoa kauli hiyo kutokana na ‘kuweweseka' kuwa kabla ya matukio ya tarehe 27 Agosti 2012 Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa alianika mipango ya vijana wa UVCCM waliofundishwa kambini kupewa silaha kwa ajili ya kuvuruga mikutano ya CHADEMA.Katika kukanusha taarifa hizo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akajikuta anatoa taarifa za mpango uliokuwepo wa kukodi magari ya vijana kwenda kufanya vurugu kwenye mikutano ya CHADEMA bila kujijua kwa kusingizia kuwa CHADEMA ndiyo inayopanga kusafirisha vijana kwenda kufanya vurugu kwenye mikutano yake yenyewe.BAVICHA inatambua kwamba kwamba wakati wa uchaguzi wa Igunga ambao UVCCM imeurejea katika kauli yake vijana wa chama hicho ndio ambao walipelekwa kwenye kambi za mafunzo ya mikakati haramu ikiwemo mauaji zilifanyika Iramba mkoani Singida na Uyui mkoani Tabora na taarifa hizi hazikuwa siri kwa kuwa zilitolewa hadharani na vijana walioamua kujivua ‘magamba' na kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu walichokuwa wakifundishwa katika kambi hizo. BAVICHA inatambua kuwa baada ya mipango haramu ya CCM na UVCCM juu ya operesheni za CHADEMA kufichuliwa, CCM na Serikali katika Mkoa wa Morogoro hawakuwa na mkakati mbadala zaidi ya kulitumia Jeshi la Polisi kuvuruga maandamano na mikutano ya CHADEMA kwa kukiuka makubaliano ambayo yalifikiwa awali katika ya CHADEMA na Jeshi la Polisi.BAVICHA inasisitiza kwamba katika matukio ya Morogoro hata baada ya polisi kuanza kuwashambulia vijana wa CHADEMA wasiokuwa na silaha yoyote, BAVICHA ilihakikisha kwamba vijana wanakuwa watulivu na wanatimiza lengo la kuelekea katika eneo la mkutano kutoka kwenye eneo la Msamvu ambalo walianza kukusanyika kwa ajili ya mapokezi.

POST MORTEM IMETHIBITISHA AMEUWAWA NA FLYING OBJECT, POLISI NI WATUHUMIWA HAWAPASWI KUJICHUNGUZA NA VIJANA WASIENDE KUTOA USHIRIKIANO KWA TUME YA MKUU WA MKUU WA MKOA

BAVICHA inawakumbusha vijana kote nchini kuzingatia kuwa vijana mashuhuda waliokuwa eneo la tukio waliohojiwa walieleza kuwa Ally Hassan Singano (Zona) alianguka baada ya kufyatuliwa kwa bunduki ya askari polisi iliyoelekezwa kwake. Pamoja na mashuhuda kutofautiana aina ya bunduki iliyotumika baadhi wakieleza ni ya risasi ya moto na wengine wakieleza kuwa ni ya kufyatulia mabovu ya machozi, utofauti huu hauondoi ukweli kuwa askari wa Jeshi la Polisi waliokuwepo eneo la tukio ndio watuhumiwa wakuu.Aidha, maelezo yaliyotolewa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile tarehe 29 Agosti 2012 kuhusu ripoti ya uchunguzi wa mwili kitabibu (post postmortem) pamoja kutolewa huku vielelezo kamili vikifichwa yamethibitisha haja ya uchunguzi huru kufanyika.BAVICHA inafahamu kwamba katika maelezo hayo polisi pamoja na kudai kuwa Ally Hassan Singano (Zona) imekiri kuwa sababu ya kifo chake ni kupigwa na kitu kizito kilichoruka (hard flying object), maelezo ambayo yanapaswa kuwarejesha vijana na wadau wote wa haki za binadamu kwenye ukweli ulisomwa na mashuhuda kwamba kama sio risasi basi alipigwa na bomu la machozi kutoka kwa askari polisi.Kutokana na ripoti ya uchunguzi huo kuonyesha utata na Jeshi la Polisi kuendelea kuwa watuhumiwa wakuu wa kusababisha mauaji, BAVICHA linaunga mkono kauli iliyotolewa na CHADEMA ya kutaka kufanyike uchunguzi huru kwa kutumia Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) sura namba 24 ya Sheria ya Tanzania ambayo imeelekezwa kuundwe kwa chombo cha kimahakama cha uchunguzi wa vifo (Corona's Court) kwa vifo vyenye utata au vilivyotokea kwenye mazingira ya vurugu.Hivyo, kufuatia taarifa ambazo BAVICHA imezipokea kuwa pamoja na timu ya polisi inayoendelea na uchunguzi mkuu wa mkoa naye ameunda tume yake ambayo tayari imeshaanza kuwaita baadhi ya viongozi na vijana wa CHADEMA kwa ajili ya kuwahoji, BAVICHA inatoa agizo kwa wanachama wake mkoani Morogoro kutokwenda kuhojiwa na tume hiyo ya mkuu wa mkoa ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama iliyolisimamia jeshi la polisi na kusababisha vurugu na mauaji.

KAULI ZA WASSIRA ZINAMFANYA KUWA WAZIRI WA ‘UHASAMA NA UHARIBIFU', VIJANA WA CHADEMA TUTAENDELEA KUDAI HAKI NA KUPAMBANA NA MAFISADI KWA NJIA ZA AMANI ZA KIDEMOKRASIA, BAVICHA INAWATAKA VIJANA WAJIANDAE KWA HATUA ZAIDI IWAPO SERIKALI ITAIFUTA CHADEMA

BAVICHA imezichukulia kwa uzito kauli za Waziri Wassira za kuitaka CHADEMA ‘kuendesha siasa bila kumwaga damu' na kudai kuwa CHADEMA imekuwa ikiendesha siasa za ‘kuvunja hali ya amani na utulivu nchini' na kudai kwamba Serikali iko tayari kuifuta CHADEMA.BAVICHA inamtaka Waziri Wassira kuelewa kwamba vijana wa CHADEMA wataendelea kusimamia amani katika nchi kwa kuunganisha nguvu katika kupambana kwa njia za kidemokrasia na mafisadi na kufuatia kauli hiyo ya Wassira, BAVICHA inatoa maelekezo kwa vijana wote wa CHADEMA nchini kujiandaa kuchukua hatua zitakazoelekezwa iwapo Serikali inayoongozwa na CCM ‘itaigusa' CHADEMA kufuatia madai ya uongo yanayoendelea kutolewa.Ikumbukwe kwamba miezi michache iliyopita alinukuliwa akidai kuwa CHADEMA itasambaratishwa ndani ya mwaka mmoja, hivyo serikali inapaswa kueleza iwapo kauli zake hizo anazozitoa jimboni ni msimamo wa CCM na serikali au ni zake binafsi.Kauli za kiserikali zinazotolewa na Waziri Wassira jimboni kwake kila anaposhikwa hasira anapofanya mikutano na kubaini vijana hawamkubali yeye na CCM kwa kuunga mkono vuguvugu la mabadiliko zinathibitisha kwamba anafaa kuwa Waziri wa ‘uhasama na uharibifu' badala ya ‘mahusiano na uratibu. BAVICHA ilitarajia kwamba Waziri Wassira ambaye ndiye mwenye wajibu wa kumshauri Rais kuhusu masuala ya siasa na mahusiano na pia anahusika na masuala ya usalama wa taifa angemshauri Rais kumtaka Waziri wa Sheria na Katiba kuwezesha sheria hiyo kutumika na chombo huru cha uchunguzi kuundwa badala yake ameendelea kufanya propaganda chafu za kuhusisha CHADEMA na umwagaji damu unaofanywa na vyombo vya dola vya serikali inayoongozwa na CCM.

Imetolewa leo tarehe
01/09/2012 na:
John Heche
Mwenyekiti Taifa-BAVICHA
 
Wadau hili ni Tamko la Bavicha kujibu tishio la waziri wa mahusiano na uratibu Steven Wassira kukifuta chama cha Chadema na Tuhuma za katibu mkuu wa uvccm martin shigela.

TAARIFA KWA UMMA
UTANGULIZI:Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) linapinga tamko lililotolewa na UVCCM kupitia Katibu Mkuu wake Martin Shigela kwenye vyombo vya habari tarehe 28 na 29 Agosti 2012 za kuhusisha mauaji yaliyotokea Morogoro tarehe 27 Agosti 2012 ya kijana Ally Hassan Singano (Zona).BAVICHA inakemea pia kauli zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) tarehe 31 Agosti 2012 za kuhusisha CHADEMA na siasa za umwagaji damu na inawataka vijana kujiandaa kwa hatua zaidi iwapo Serikali itaifuta CHADEMA.Aidha, BAVICHA imepokea taarifa kutoka Morogoro kuwa baadhi ya vijana wake wameandikiwa barua na serikali ngazi ya mkoa kuwa wanaitwa kuhojiwa na tume ya kuchunguza mauaji na inatoa agizo kwa vijana wote wa CHADEMA kutokwenda kuhojiwa na tume hiyo iliyoundwa na mkuu wa mkoa ambaye ni sehemu ya viongozi wanaotuhimiwa kushawishi polisi kukiuka makubiliano na kusababisha mauaji. KAULI ZA UVCCM NI MWENDELEZO WA MADAI YA UONGO YA MUKAMA NA CCM NA NI KUWEWESEKA BAADA YA DR SLAA ‘KUANIKA’ MIPANGO YAO HARAMU YA KUTUMA VIJANA WAKE WENYE SILAHA KUVURUGA MAANDAMANO NA MIKUTANO YA CHADEMABAVICHA inatambua kwamba propaganda chafu hizo za UVCCM ambazo pia zimedai kuwa vijana wa CHADEMA waliingiza silaha kwa wingi Igunga ni mwendelezo wa siasa chafua ambazo zilifanywa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama katika uchaguzi huo kwa kudai kuwa CHADEMA iliingiza magaidi na makomandoo kutoka nje ya nchi, uongo ambao alishindwa kuuthibitisha mahakamani na hivyo kuchangia katika mahakama kubatilisha ushindi wao haramu katika uchaguzi huo.BAVICHA inafahamu kwamba UVCCM imetoa kauli hiyo kutokana na ‘kuweweseka’ kuwa kabla ya matukio ya tarehe 27 Agosti 2012 Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa alianika mipango ya vijana wa UVCCM waliofundishwa kambini kupewa silaha kwa ajili ya kuvuruga mikutano ya CHADEMA.Katika kukanusha taarifa hizo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akajikuta anatoa taarifa za mpango uliokuwepo wa kukodi magari ya vijana kwenda kufanya vurugu kwenye mikutano ya CHADEMA bila kujijua kwa kusingizia kuwa CHADEMA ndiyo inayopanga kusafirisha vijana kwenda kufanya vurugu kwenye mikutano yake yenyewe.BAVICHA inatambua kwamba kwamba wakati wa uchaguzi wa Igunga ambao UVCCM imeurejea katika kauli yake vijana wa chama hicho ndio ambao walipelekwa kwenye kambi za mafunzo ya mikakati haramu ikiwemo mauaji zilifanyika Iramba mkoani Singida na Uyui mkoani Tabora na taarifa hizi hazikuwa siri kwa kuwa zilitolewa hadharani na vijana walioamua kujivua ‘magamba’ na kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu walichokuwa wakifundishwa katika kambi hizo. BAVICHA inatambua kuwa baada ya mipango haramu ya CCM na UVCCM juu ya operesheni za CHADEMA kufichuliwa, CCM na Serikali katika Mkoa wa Morogoro hawakuwa na mkakati mbadala zaidi ya kulitumia Jeshi la Polisi kuvuruga maandamano na mikutano ya CHADEMA kwa kukiuka makubaliano ambayo yalifikiwa awali katika ya CHADEMA na Jeshi la Polisi.BAVICHA inasisitiza kwamba katika matukio ya Morogoro hata baada ya polisi kuanza kuwashambulia vijana wa CHADEMA wasiokuwa na silaha yoyote, BAVICHA ilihakikisha kwamba vijana wanakuwa watulivu na wanatimiza lengo la kuelekea katika eneo la mkutano kutoka kwenye eneo la Msamvu ambalo walianza kukusanyika kwa ajili ya mapokezi.POST MORTEM IMETHIBITISHA AMEUWAWA NA FLYING OBJECT, POLISI NI WATUHUMIWA HAWAPASWI KUJICHUNGUZA NA VIJANA WASIENDE KUTOA USHIRIKIANO KWA TUME YA MKUU WA MKUU WA MKOABAVICHA inawakumbusha vijana kote nchini kuzingatia kuwa vijana mashuhuda waliokuwa eneo la tukio waliohojiwa walieleza kuwa Ally Hassan Singano (Zona) alianguka baada ya kufyatuliwa kwa bunduki ya askari polisi iliyoelekezwa kwake. Pamoja na mashuhuda kutofautiana aina ya bunduki iliyotumika baadhi wakieleza ni ya risasi ya moto na wengine wakieleza kuwa ni ya kufyatulia mabovu ya machozi, utofauti huu hauondoi ukweli kuwa askari wa Jeshi la Polisi waliokuwepo eneo la tukio ndio watuhumiwa wakuu.Aidha, maelezo yaliyotolewa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile tarehe 29 Agosti 2012 kuhusu ripoti ya uchunguzi wa mwili kitabibu (post postmortem) pamoja kutolewa huku vielelezo kamili vikifichwa yamethibitisha haja ya uchunguzi huru kufanyika.BAVICHA inafahamu kwamba katika maelezo hayo polisi pamoja na kudai kuwa Ally Hassan Singano (Zona) imekiri kuwa sababu ya kifo chake ni kupigwa na kitu kizito kilichoruka (hard flying object), maelezo ambayo yanapaswa kuwarejesha vijana na wadau wote wa haki za binadamu kwenye ukweli ulisomwa na mashuhuda kwamba kama sio risasi basi alipigwa na bomu la machozi kutoka kwa askari polisi.Kutokana na ripoti ya uchunguzi huo kuonyesha utata na Jeshi la Polisi kuendelea kuwa watuhumiwa wakuu wa kusababisha mauaji, BAVICHA linaunga mkono kauli iliyotolewa na CHADEMA ya kutaka kufanyike uchunguzi huru kwa kutumia Sheria ya Uchunguzi wa Vifo (Inquest Act) sura namba 24 ya Sheria ya Tanzania ambayo imeelekezwa kuundwe kwa chombo cha kimahakama cha uchunguzi wa vifo (Corona’s Court) kwa vifo vyenye utata au vilivyotokea kwenye mazingira ya vurugu.Hivyo, kufuatia taarifa ambazo BAVICHA imezipokea kuwa pamoja na timu ya polisi inayoendelea na uchunguzi mkuu wa mkoa naye ameunda tume yake ambayo tayari imeshaanza kuwaita baadhi ya viongozi na vijana wa CHADEMA kwa ajili ya kuwahoji, BAVICHA inatoa agizo kwa wanachama wake mkoani Morogoro kutokwenda kuhojiwa na tume hiyo ya mkuu wa mkoa ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama iliyolisimamia jeshi la polisi na kusababisha vurugu na mauaji.KAULI ZA WASSIRA ZINAMFANYA KUWA WAZIRI WA ‘UHASAMA NA UHARIBIFU’, VIJANA WA CHADEMA TUTAENDELEA KUDAI HAKI NA KUPAMBANA NA MAFISADI KWA NJIA ZA AMANI ZA KIDEMOKRASIA, BAVICHA INAWATAKA VIJANA WAJIANDAE KWA HATUA ZAIDI IWAPO SERIKALI ITAIFUTA CHADEMABAVICHA imezichukulia kwa uzito kauli za Waziri Wassira za kuitaka CHADEMA ‘kuendesha siasa bila kumwaga damu’ na kudai kuwa CHADEMA imekuwa ikiendesha siasa za ‘kuvunja hali ya amani na utulivu nchini’ na kudai kwamba Serikali iko tayari kuifuta CHADEMA.BAVICHA inamtaka Waziri Wassira kuelewa kwamba vijana wa CHADEMA wataendelea kusimamia amani katika nchi kwa kuunganisha nguvu katika kupambana kwa njia za kidemokrasia na mafisadi na kufuatia kauli hiyo ya Wassira, BAVICHA inatoa maelekezo kwa vijana wote wa CHADEMA nchini kujiandaa kuchukua hatua zitakazoelekezwa iwapo Serikali inayoongozwa na CCM ‘itaigusa’ CHADEMA kufuatia madai ya uongo yanayoendelea kutolewa.Ikumbukwe kwamba miezi michache iliyopita alinukuliwa akidai kuwa CHADEMA itasambaratishwa ndani ya mwaka mmoja, hivyo serikali inapaswa kueleza iwapo kauli zake hizo anazozitoa jimboni ni msimamo wa CCM na serikali au ni zake binafsi.Kauli za kiserikali zinazotolewa na Waziri Wassira jimboni kwake kila anaposhikwa hasira anapofanya mikutano na kubaini vijana hawamkubali yeye na CCM kwa kuunga mkono vuguvugu la mabadiliko zinathibitisha kwamba anafaa kuwa Waziri wa ‘uhasama na uharibifu’ badala ya ‘mahusiano na uratibu. BAVICHA ilitarajia kwamba Waziri Wassira ambaye ndiye mwenye wajibu wa kumshauri Rais kuhusu masuala ya siasa na mahusiano na pia anahusika na masuala ya usalama wa taifa angemshauri Rais kumtaka Waziri wa Sheria na Katiba kuwezesha sheria hiyo kutumika na chombo huru cha uchunguzi kuundwa badala yake ameendelea kufanya propaganda chafu za kuhusisha CHADEMA na umwagaji damu unaofanywa na vyombo vya dola vya serikali inayoongozwa na CCM.Imetolewa leo tarehe 01/09/2012 na:
John Heche
Mwenyekiti Taifa-BAVICHA
Hongera kamanda Heche hii imetulia sana piga huyo gamba Wasira huyu mzee amezeeka vibaya, anaogopa kustaafu.
 
Wassira anaogopa mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea nchini.
 
Mzee wa usingizi huyo, msishangae alikuwa ndotoni'

Huyu mzee na vijana wake wanajua wanachokifanya na si kwa nia nzuri kabisa. Jamani kwa nini siasa za Tanzania zinakuwa hivi? Maranyingi nimemsikiliza Mzee huyu na anaonekana kutokuwa tayari kwa mabadiriko, the same applied to M/kiti wa vijana ccm. Where do they want to lead us to...ee Mungu tusaidie na hawa watu.
 
Pindi unapoona kiongozi wa serikali au wa chama tawala anatoa tuhuma dhidi ya UPINZANI, amefilisika kisiasa. Chama tawala hakitakiwi kulalamika, bali ni kutekeleza na kufanyia kazi malalamiko. Serikali haina mipaka ktk kufanya kazi zake, Kama CDM wameingiza silaha, Serikali ilikuwa wapi?
 
Back
Top Bottom