Tamko la serikali dhidi ya kampuni zitakazo sababisha ajali...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
.....Serikali imetoa tamko leo asubuhi dhidi ya kampuni zote za usafirishaji wa majini na nchi kavu zitakazo sababisha ajali......akitoa tamko hilo kwa niaba ya serikali waziri Omari Nundu amesema kuanzia leo SUMATRA imepewa agizo kuzifungia au kuzinyang'anya leseni za biashara kampuni zote zitakazo sababisha ajali...

Waziri akaendelea kusema kuwa kuanzia sasa serikalia haitakua na huruma na kampuni yoyote itakayo sababisha ajali...na kwa maelezo yake,endepo kampuni itasababisha ajali itakuwa ni automatic ban.....

My opinions:
Kama hili litatekelezwa ipasavyo litapunguza ajali kwa kiasi kikubwa sana.....
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,470
9,013
anajua mtu akifikia uwezo wa kumiliki chombo cha usafiri anakuwa anamiliki makampuni (majina ya kampuni) mangapi!? Waziri na watawala wasijifanye kuelewa mambo maanaa ukweli ni kuwa wananchi wanaelewa zaidi yao!
 

Komeo

JF-Expert Member
May 3, 2011
2,497
1,169
Hiyo SUMATRA iliyopewa agizo hilo inafanya kazi hadi Zenji? Maana siku za nyuma walifukuzwa kule na ofisi zao kufungwa. Kwasasa wana operate huku bara tu.
 

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,461
Nchi ya kukurupuka utaijua tu. Huwezi kusema kama kasuku eti kampuni itakayosababisha ajali automatic ban. Kuna ajali zisizozuilika na kuna ajali za uzembe wa wazi. Kabla ya kutoa tamko ni lazima watoe safety standards ili atakayezikiuka na kusababisha ajali afungiwe.

Kwanza hajasema watakaotoa leseni kwa vyombo vibovu, Traffic watakao ruhusu magari yasiyofaa kubeba abiria, watakao beba abiria kwenye malori kama kwenye kampeni watakaojaza abiria wafanyweje tusingojee tufe au tuuwawe ndio awafungiwe mtu.

Usalama barabarani, majini na angani ni everyday duty sio tamko. Wizara na mamlaka husika zisikimbie wajibu zake. Wenzetu wapo makini sana kwenye kuzia ajali kwa kuangalia maeneo yote ubara wa vyombo, watumiaji, waendeshaji na utunzwaji wa vyombo husika. Kuna mabasi mengi yasiyofaa kwa abiria. Traffic hawafanyi kazi zao za usalama barabarani, meli nyingi na boat ni mbovu. Ndege zetu nyingi chakavu na hazina viwango. Viwanja vyetu havina zimamoto, barabara zetu hazifai sasa tuanze wapi????

wizara isije na lugha za jumla za kupanic waje na kauli na utendaji wenye kichwa na miguu, haya matamko ya zimamoto yametuchosha na tunakufa kila siku.
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,406
62,432
Hebu waache upuuzi wao hukoo tena wakae kimya waache kupayuka kama wajinga....hebu wasiache nikapata unnecessary Ban bure mie, yaani "kuanzia leo" ina maanisha nini? Uzembe, ujinga, ubedhui, kujisahau, na mengine mabaya kwani mara ngapi maneno hayo yalitolewa na hakuna kilichofanyika? au tuanze kuyakumbusha hapa? Washen......wakubwa hawa, hivi jamaa wanapatikana wapi? ningeweza kuwa-face ningesema haya kwa amcho makavu tena mchana kweupe kuwa wasitufanye wajinga kiasi hiki, pumbavu kabisa.
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,502
7,827
matamko kama hayo ni yakupuuzia tu, yameshatolewa mangapi na yanayopingana? watengeneze miundombinu yenye ufanisi na sio kutoa matamko, hata mke wangu nyumbani anatoa matamko.
 

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
6,711
12,417
Matamko hayasaidii kama hakuna sheria kali ambazo pia zitasimamiwa ipasavyo,
vinginevyo kila mara tutaendelea kuunda tume ambazo hata hivyo zikileta mapendekezo
hakuna anayeyafanyia kazi: mfano Baada ya ajali ya MV Bukoba ambayo iliwaachia makundi
ya watu simanzi, mateso, ukiwa, ufukara na kila aina ya dhiki, serikali yetu hii wakati huo
ikiongozwa na Benjamini Mkapa, kwa kutumia kodi zetu hizi hizi, iliunda Tume kuchunguza
jambo hilo ikiongozwa na Jaji Robert Kisanga.
Kabla ya ajali ya juzi ya MV Spice Islander, mtu angeliweza kutabiri kwamba yaliyoibuliwa
na Tume ya Jaji Kisanga, hayajafanyiwa kazi, yametupwa kwenye makabati na hivyo ajali
kama ya MV Bukoba inaweza kutokea muda wowote nchini mwetu na mahala popote.
Tume na matamko ya serikali ni hila za kuwaridhisha tu wananchi baada ya kutokea jambo
kubwa lililowashitua kwa staili ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite...
 

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,166
Mark my words in capital letters "HAYATATENDEKA"

Ni staili yetu tunaongea ajali inapotokea na baada ya kuwazika marehemu tunarudi kulekule kwenye uzembe na ubabaishaji. Haibkubaliki kuwa kampuni ifutiwe leseni baada ya kusababisha ajali, na sio kwa kuhatarisha maisha ya watu.

Ingekuwa ni kweli baada ya kutokea kwa jali ya MV Bukoba kusingetokea ajli kubwa kama hiii.

Pamoja na danganya toto ya kusema ziwekwe speed governors kwenye magari, still bado yanaua na yanaendelea kuua. so, same old story, nakubaliana na Li Flower "HAYATATENDEKA"
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Hiki kitu tumeandika sana hapa Jamvini. I hope serikali itasimamia kauli zake maana haiingii akilini kwa magari ya kampuni moja (kwa mfano) kupata ajali zaidi ya 4 ndani ya miezi 6. Summry, Abood, Hood yamekuwa kama yanashindana kwa kupata ajali.

Huko nyuma serikali iliwahi kutoa statement kwamba mabasi makubwa hataruhusiwa kuchanganya bodi na engine (fuso vs bus). Lakini nadhani kuna 'lobbying' ilifanyika hivyo nothing happened. Ni matumaini yangu kwamba kama taifa hatutakumbwa na mkasa kama huu wa kuzika watu kwa mamia kwa sababu uzembe.
 

Shapu

JF-Expert Member
Jan 17, 2008
2,105
782
Sidhani kama huko serikalini kwenu kuna watu wenye akili timamu. Wanatakiwa wafanye root cause analysis na katika kila area waweke ation plan. sasa hawa wanakuja na hii solusion ambayo haina kichwa wala miguu...stupid.
 

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,316
.....Serikali imetoa tamko leo asubuhi dhidi ya kampuni zote za usafirishaji wa majini na nchi kavu zitakazo sababisha ajali......akitoa tamko hilo kwa niaba ya serikali waziri Omari Nundu amesema kuanzia leo SUMATRA imepewa agizo kuzifungia au kuzinyang'anya leseni za biashara kampuni zote zitakazo sababisha ajali...

Waziri akaendelea kusema kuwa kuanzia sasa serikalia haitakua na huruma na kampuni yoyote itakayo sababisha ajali...na kwa maelezo yake,endepo kampuni itasababisha ajali itakuwa ni automatic ban.....

My opinions:
Kama hili litatekelezwa ipasavyo litapunguza ajali kwa kiasi kikubwa sana.....

Nafikiri kuna mapungufu makubwa sana katika tamko lake.Alitakiwa awe muwazi zaidi kwa kusema atakaye sababisha ajali kwa uzembe au kwa kutofata sheria ndio wanatakiwa kufungiwa.

Kwani Hakuna hata siku moja mtu mwenye akili timamu akaamka asubuhi na kusema leo ngoja nikaendeshe gari au chombo chochote kile na nikasababishe ajali. Kila mtu anaomba salama akiwa anaendesha chombo.

Tunaamini hakuna kampuni inayokusudia kusababisha ajali na kupoteza maisha ya watu. Kwani kitendo hicho kibiashara kinapunguza wateja na kuisababishia kampuni kuyumba na hatimaye kufa kiuchumi.

Nafikiri Serikali a JMT inawapasa kusimamia vizuri sheria za usalama wa vyombo vyote sio tu vya majini pia vya nchi kavu na abiria. Sheria lazima ziwekwe wazi kuwajuza watumiaji na wamiliki. Hakika kutoa elimu ni muhimu sana kabla abiria kuanza safari na hata wanapofika kama inavyofanyika katika Ndege.

Lakini vile vile ni muhimu kuvikagua vombo vyote kuhakikisha uzima na usalama wake kabla kuanza safari zake za majini au nchi kavu.

Kunatakiwa uadilifu mkubwa kwa watendaji wa mamlaka za Serikali katika kusimamia sheria.

Kila la kheir
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,406
62,432
Hahahhaaaaa Osie baba hata shemeji hua anatoa matamko? kuwa leo "usile tundi" hahahaaaa imekaa vizuri kakaaa, kwa hio hawa jamaa wamezidiwa akili hata na shemeji eeehh??
matamko kama hayo ni yakupuuzia tu, yameshatolewa mangapi na yanayopingana? watengeneze miundombinu yenye ufanisi na sio kutoa matamko, hata mke wangu nyumbani anatoa matamko.
 

Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
Hii serikali iache kufikiri kwa kutumia masaburi na lusekelo, badala ya kutuambia hadi sasa imeshawachukulia hatua watumishi wangapi ili iwe fundisho, wao wanakuja na matamko! Haya ndio matatizo ya serikali ya kulindana. Na huyu makamu wa kwanza wa rais wa znz naye amelizka na matamko haya!
 

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,435
Huyu waziri na hiyo serikali yao waanakurupuka tu,hawajui wanachoongea.Haya ndio madhara ya kuwa na serikali yenye hulka ya kufuata upepo na kukuruupukia maamuzi ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina.
Kama serikali ipo makini na inachokiongea ingewawajibisha maafisa wa serikali waliochangia kutokea kwa ajali ile .Hawa wanataka kutuambia kuwa siku zote ajali zinapotokea ni uzembe wa wamiliki,wakati si kweli.Mbona hajazungumzia ikibainika kuwa waliochangia/sabaisha ajali kutokea ni wasimamizi kwa maana ya maafisa wa serikali!?
Kwanza wanatupumbaza hawa sana kwa ujinga wao sasa wanataka kila mmoja atembee na kusadiki juu ya maneno yao ili hali inafahamika wazi kuwa wavunjaji wa sheria wakubwa kwenye hivi vyombo vya usafirishaji ni wao.Hii ni kutokana na kwamba wamiliki wengi wa vyombo vya usafiri ndio hao wenye dhamana ya kuvisimamia vyombo hivi(kwa maana ya mawaziri,makamanda wa polisi nk) ama wanaomiliki ni maswaiba wao wakubwa wanaowachangia kwenye kampeni zao za kisiasa .Nawasilisha
 

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,840
628
kama chenge aliua watu wawili akalipa laki saba
kwani wenye makampuni yao watashindwa nini kulipa hata wakiua mia.

tatizo ni kutosimamia na kupindisha pindisha sheria
 

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,786
1,633
tamko! tamko! MATAMKO MANGAPI YAMESHATAMKWA NA AJALI MBAYA NA ZINATOKEA KILA KUKICHA, juzi kati hapo morogoro c kulitokea ajali mbaya zaid ya 3 kukatamkwa matamko?? TUNATAKA HATUA ZA KISHERIA NA C MATAMKO YA KIJINGAJINGA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom