Serikali yaingilia kati taarifa ya unyanyasaji wa wafanyakazi Kampuni ya Pepsi, Waziri asema anaenda kiwandani hapo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa juu ya uwepo wa unyanyasaji wa wafanyakazi katika Kampuni ya SBC Tanzania (Kiwanda cha Pepsi), hatimaye Serikali imetoa tamko juu ya kinachoendelea kiwandani hapo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira & Wenye Ulemavu) ametoa tamkoa hilo leo Machi 27, 2022 na kuelezea kuwa ana ripoti ya kinachoendelea na kuongeza kuwa atafika kiwandani hapo yeye mwenyewe katika kiwanda hicho Tawi la Dar es Salaam, kesho Jumatatu Machi 28, 2022.


HILI HAPA TAMKO RASMI LA NAIBU WAZIRI…

Nimeona jambo katika Mitandao yetu, naomba kwa ufupi kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepusha Upotoshaji wa makusudi kuwa Serikali haijalitilia nguvu.

Suala la SBC LTD nalitambua na hatua za kisheria zinaendelea, awali nilishamuagiza Kamishina Brigedia General Francis Mbindi (Kipindi kilichopita) alienda na kulishughulikia vizuri mara ya kwanza alichukua hatua na kutoa Maagizo na Maelekezo ya Utekelezaji Sheria za Kazi pamoja na hayo alifuta Vibali vya Wafanyakazi wa kigeni waliokiuka Sheria.

Yapo yaliyotekelezwa na tulipobaini ambayo hayakutekelezwa alirudi mara ya pili na kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria za Kazi na kwakuwa maswala ya kazi sio jinai sio sahihi kwa waliotaka kuona watu wakiburuzwa bali kuna taratibu za kufuata kwa mujibu wa Sheria tofauti na Jinai.

Juzi nikiwa katika Kikao cha High Level Policy Conference Youth as Researchers on Covid -19 kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Nililazimika kukutana na Kamishina wa Kazi Bi.Suzan na timu ya Wataalamu ambao wameendelea kulifanyia Kazi vizuri na nikaagiza yafuatayo.

Mosi: nimewaagiza kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Ikiwa ni Kufanya uchunguzi wa kina juu ya yanayolalamikiwa na pili kufanya ukaguzi tena kwa mapya yatakayojitokeza na kuchukua hatua.

Naomba kutoa Rai pia kwa Wafanyakazi wasisubiri shida zikithiri kwenye maeneo yao ya Kazi, watupe taarifa mapema pamoja na kwamba pia tuna taarifa ya madai mengine siyo ya kweli wapo Wafanyakazi waliofanya makosa ya kinidhamu na kuvunja Sheria za Kazi ambao wanataka kujificha katika haya na kuzusha yasiyo kweli kutafta huruma kwa jamii.

Serikali ya Mhe. Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassani haitapendelea Mtu wala kumuonea Mtu wala kampuni, HAKI itachakatwa kwa mujibu wa Sheria na ataipata anaestahili.

Jumatatu nitapokea taarifa, hatua na Mapendekezo ya Uchunguzi na nitafika hapo mwenyewe kwa niaba ya Mhe. Waziri na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa UAMUZI, MAELEKEZO kisheria kulingana na taarifa tafiti zitakazopatikana na tutaujulisha Umma.

Nawasihi Sana Ndugu zangu tuwe na Utulivu pande zote, tutalimaza salama na kwa mujibu wa Sheria HAKI ITATENDEKA.

Patrobas Katambi,
NW OWM Kazi, Vijana na Ajira,
27.03.2022.



=====================

Pia soma...
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Welldone na hii inapendeza mno unapoona serikali yako inafanyia kazi malalamiko kama haya ambayo yanaweza kuwa sehemu mbili,

Ninategemea serikali yangu itakuja na uamuzi sahihi na kuutekeleza, sio vema tukarudi nyuma kama ilivyofanyika nyuma na maagizo yake hayakutekelezwa,kudos to Minister
 
Naomba kutoa Rai pia kwa Wafanyakazi wasisubiri shida zikithiri kwenye maeneo yao ya Kazi, watupe taarifa mapema pamoja na kwamba pia tuna taarifa ya madai mengine siyo ya kweli wapo Wafanyakazi waliofanya makosa ya kinidhamu na kuvunja Sheria za Kazi ambao wanataka kujificha katika haya na kuzusha yasiyo kweli kutafta huruma kwa jamii.
Wakisema mapema mnawaambia wachochezi, wakisubiri mnawaambia haya,
 
Huyo Brigedia aliona Jitendra Shekawat ana haki ya kukaa nchini tangu 2012 Hadi leo?

Kwani vibali kihalali vinatolewaje?
Tangu 2012 ni kazi gani hiyo ambayo mzawa hawezi kuifanya.

Jitendra ni manager strategic planning, tangu 2012 Hadi leo hatuja train mzawa planner.

Foti unae wakingia kifua wahindi unasemaje?
 
Huyo Brigedia aliona Jitendra Shekawat ana haki ya kukaa nchini tangu 2012 Hadi leo?
Kwani vibali kihalali vinatolewaje?
Tangu 2012 ni kazi gani hiyo ambayo mzawa hawezi kuifanya.
Jitendra ni manager strategic planning, tangu 2012 Hadi leo hatuja train mzawa planner.
Foti unae wakingia kifua wahindi unasemaje?
Kama ni kweli huyo brigedia kafanya hivyo hapo kachemka.

Kibali cha kazi ni miaka 2 una renwal tena 2 jumla miaka 4 hapo wazawa tayari wanakuwa washaelewa hiyo kazi

Na ndo maana serikali inataka epart mmoja aambatane na watu kumi ili hata mmoja kati hao kumi waweze kujua hiyo kazi pindi muda wake unapoisha yy aishie wazawa waendelee
 
Nchi yetu ina sheria zake za immigrations, sasa inapotokea sheria hizi zinachezewa, heshima ya nchi inakwisha,

Inapotokea passport zetu zinatumiwa bila halali na watu ambao sio watanzania huu ni ufisadi wa hali ya juu, ni muhimu hizi permits ziwe verified ninaanza kuwa na wasiwasi hii permit ni ya mchongo,

Immigrations department yetu inatuvua nguo pamoja na walinda mipaka yetu (jwtz),nchi imegeuka short cut ya humans trafficking
 
kama ni kweli huyo brigedia kafanya hivyo hapo kachemka kibali cha kazi ni miaka 2 una renwal tena 2 jumla miaka 4 hapo wazawa tayari wanakuwa washaelewa hiyo kazi na ndo maana serikali inataka epart mmoja aambatane na watu kumi ili hata mmoja kati hao kumi waweze kujua hiyo kazi pindi muda wake unapoisha yy aishie wazawa waendelee
Jitendra ana zaidi ya miaka kumi.

Kila baada ya miaka miwili Foti anapeleka bahasha uhamiaji na idara ya kazi vibali vinatolewa ili tunyanyasike sisi
 
Welldone na hii inapendeza mno unapoona serikali yako inafanyia kazi malalamiko kama haya ambayo yanaweza kuwa sehemu mbili, ninategemea serikali yangu itakuja na uamuzi sahihi na kuutekeleza, sio vema tukarudi nyuma kama ilivyofanyika nyuma na maagizo yake hayakutekelezwa,kudos to Minister
Akifika pale atapewa bahasha nono na mambo yanaisha,

Angalia issue ya mto Mara kila anayekanyaga anarudi na bahasha nono
 
Siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa juu ya uwepo wa unyanyasaji wa wafanyakazi katika Kampuni ya SBC Tanzania (Kiwanda cha Pepsi), hatimaye Serikali imetoa tamko juu ya kinachoendelea kiwandani hapo.
pia wakitoka hapo wapitie na viwanda vingine haki nyingi sana za msingi zinaminywa ila wahusika hawashughulikiwi,

Na wakianza kushughulikiwa kwa kufuata taratibu zilizopo yataanza maneno kuwa tunakimbiza wawekezaji ilhali ni vitu ambavyo vipo katika maandishi hivyo utekelezaji muhimu uwepo.
 
Mlioko kwenye mkutano na waziri tujuzeni yanayoendelea.

Mtaendelea kumkumbatia Jiten ?

Ziad anasemaje kuhusu Jiten?
 
Back
Top Bottom