Tamko la mbunge Ubungo kuhusu bomoa bomoa ya Magufuli

""NAMUUNGA MKONO FREEMAN AIKAELI MBOWE AGOMBEE URAISI 2015""

Mkuu hiyo sijakubaliana nayo, itatuangusha. Au unaonaje?[/QUOTE]

Zitto kabwe katangaza kugombea Urais 2015 na Mnyika katangaza kumuunga mkono Mbowe kugombea Urais 2015, mmmmh patamu hapo kumbe mpasuko hauko CCM peke yake.!!!!!!!!!
 
UNAPOTEA NDUGU HUU NI MSIMAMO WA SON OF PEASANT (SoP) SIO MSIMAMO WA MNYIKA,MIMI NDIE NILIEPOST HII THREAD HAPA NA SIO MNYIKA ELEWA VIZURI.

NA HUU NI MSIMAMO WANGU KWA SASA ILA UNAWEZA BADILIKA NIKIAMUA BAADAE

ILA KWA SASA NAMUUNGA MKONO FREEMAN AIKAELI MBOWE AGOMBEE URAISI 2015
 
Kumbe umaarufu wa akina Zitto na Mnyika unabeba na mamlaka nyingine za chama bila kufuata kanuni na taratibu.
 
New York (Manhattan) hakuingiliki kutokana na foleni ndio maan wengi wanatumia subway kufika mjini na wakiwa humo taxi. Ili kupunguza kadhia hiyo, ndiyo maana walitaka kujenga tunnel chini ya mto Hudson itakayowaunganisha na New Jersey ili kuongeza treni zinazosafiri kati ya miji hiyo miwili. Los Angeles pamoja na flyovers kibao bado kuna kitu kinaitwa road rage. Ole wako mpigie honi jamaa aliye kwenye foleni. London wameweka congestion fees katika kujaribu kukwepa hilo. Paris walikuwa wajanja wakajenga La Defense ili kupunguza haja ya watu kuingia paris na magari yao. Copenhagen wanapunguza parking mjini na wamejenda mji mpya wa Orestad kupungizia mzigo mji mkongwe. Na kadhalika na kadhalika.
Na bado kuna foleni?

Sisi tunatakiwa tujenge overpass kwenye makutano ya barabara kwa kuanzia. Dar-es-Salaam msongamano upo kwenye makutano machache sana ambapo hakuna taa au kuna polisi au kuna vi bottleneck vidogo vidogo kama vituo vya daladala.

Bagamoyo Rd. (Millenium Tower mpaka Morroco) kuna foleni kwa sababu ya mataa ya Bamaga na Morroco

Morogoro Road (Kimara mpaka Urafiki) kuna foleni kwa sababu ya mataa ya Mandela pale sheli (vituo vya mafuta bongo vinaitwa sheli, kiwe cha BP kiwe cha Total, ni Shell!).

Posta kuna foleni kwa sababu ya bottleneck ya kituo cha daladala

Bagamoyo Rd. kuna foleni Tegeta kwa sababu ya kituo cha daladala kiko barabarani (Wanapaita Kwa Ndevu).

Chang'ombe Rd. kuanzia Veta Mpaka TRA Temeke kuna foleni kwa sababu ya mataa ya Nyerere Road tu.

Tabata mpaka Buguruni mpaka Nyerere Road foleni inasababishwa na mataa ya Tazara, basi!

Magomeni mpaka Fire mpaka Umoja wa Vijana kuna foleni kwa sababu ya mataa ya Usalama/Mapipa na mataa ya Lumumba.

Hapa Mnazi Mmoja kuna ka foleni ka kufa mtu kanakoanzia Clock Tower mpaka Karume kwa sababu pale Anatoglu hakuna taa, hakuna polisi. Mkokoteni mmoja ukiziba njia panageuka parking lot.

Foleni ya Kariakoo Msimbazi ni kwa sababu ya taa za Nyerere Rd/Kamata. Basi!

Sasa hizi sehemu zenye bottleneck ndio tunasema tuweke overpass kwanza. Badala ya kungoja hiyo mipango ya kujenga miji mingine, unafikiri itaanza leo hiyo?
 
Kwa hiyo, Mkuu, solution pekee unayoiona ni overpass? Tatizo si taa bali wingi wa magari. Kwa nini tusitafute njia mbadala za kupunguza wingi wa hayo magari? Kama dala dala ni tatizo kwa nini tusifanye hima na huo mradi wa mabasi yaendayo kasi? Miji mingi zina dedicated lanes kwa ajili ya mabasi. Ukitekelezwa vyema utapunguza sana msongamano wa magari kuliko hizo fly-overs ambazo tunazipigia debe. Angalia hapa uone wenzetu walivyofanikiwa Curitiba, Brazil Curitiba - Wikipedia, the free encyclopedia

Miji ya Bogota na Medellin yamefanikiwa sana kwenye hili. Mipango ya kuendeleza CBD nyingine ni ya muda mrefu lakini sidhani kama itagharimu kama hiyo inayopendekezwa sasa. Serikali inatakiwa i-identify sehemu, itayarishe master plan na iwekeze kwenye services. Hii ikiambatana na sheria ngumu za uendelezaji katikati ya jiji, italazimisha wawekezaji kukimbilia huko. Mfano mzuri ni La Defense karibu na Paris. Tukumbuke kuwa hata hizo fly-overs haziwezi kuangaliwa in isolation, ni lazioma ziwe sehemu ya mpango mji kamambe. Hauwezi kuangalia tatizo sheli bila kujiuliza linaanzia wapi. Foleni hazisababishwi na kukosekana taa au polisi peke yake bali wingi wa magari kupita uwezo wa barabara kumudu.

Amandla....
.
 
Swali langu kwanini ubungo,Je kuanzia Airport mpaka kwenye mabomu,Je DAR ndo mkoa unaoitaji barabara za lami tu.????
 
JOHN JOHN MNYIKA
MBUNGE UBUNGO

Tamko langu la awali kuhusu kuwekwa X katika majengo ya pembeni ya Barabara ya Morogoro

Katika kipindi cha wiki moja mfululizo kuanzia tarehe 11 mpaka 17 Februari 2011 nikiwa bungeni Dodoma nimekuwa nikipokea simu na sms toka kwa wananchi wakilalamikia hatua ya wafanyakazi wa wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam (TANROADS) kupita katika nyumba zao zilizopembezoni mwa barabara ya Morogoro bila wakazi kupewa notisi na kuweka alama za “X” ama “BOMOA TNRD”.

Aidha nimesoma kwenye baadhi ya vyombo vya habari (mf. NIPASHE Toleo na. 056929 la tarehe 18 Februari 2011 Uk 1 na 8) habari yenye kichwa “bomoa bomoa nyingine kukumba wakazi wa Ubungo/Dar”

Habari hiyo imemnukuu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, James Nyabakari akiwataka watu wote waliojenga kwenye hifadhi ya Barabara kubomoa wenyewe na kwamba serikali haitawalipa kwa kuwa ni wavamizi na kwamba watakaolipwa ni wale tu ambao serikali itahitaji maeneo yao.

Taarifa zinazoelezwa ni kwamba alama hizo zimewekwa mita 90 pande zote mbili za barabara kuanzia maeneo ya Ubungo mpaka Kimara, na kwamba hali hiyo itawagusa pia wananchi wa Mbezi mpaka Kiluvya katika hatua za baadaye.

Nikiwa mwakilishi wa wananchi wa maeneo husika nimeshangazwa na hatua kubwa kama hizi za kiserikali kuchukuliwa bila kufanyika kwa mikutano ya umma ama walau kutoa taarifa ya kuelimisha umma kuhusu mipango husika inayotarajiwa kufanyika. Aidha nimeshangazwa zaidi na hatua kama hizo kuchukuliwa bila walau wawakilishi wa wananchi kama wenyeviti wa mitaa, madiwani na wabunge kuelezwa kwa kina mipango inayokusudiwa kufanyika na athari zake kwa wananchi wa maeneo husika. Utendaji kazi wa namna hii ni kinyume na misingi ya utawala bora inayotaka uwazi na pia ni chanzo cha migogoro isiyo ya lazima katika jamii.

Nachukua fursa hii kutoa mwito kwa serikali ngazi ya wizara ya ujenzi, mkoa na wilaya kuhakikisha kwamba mikutano na wananchi inafanyika ama walau matangazo kwa umma yanatolewa kuhusu suala husika.

Aidha mamlaka husika za kiserikali zitoe maelezo ya wazi kuhusu wananchi wanaostahili fidia na kutoa notisi ya muda wa kutosha kwa wakazi wenye majengo yanayostahili kubomolewa ili kupitisha barabara ya mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka (DART) na mipango mingine.

Katika kufanya hivyo Serikali izingatie kuwa wapo wakazi wengi wenye kustahili kulipwa fidia kutokana na historia ya Barabara hiyo ya Morogoro kuliko ambavyo suala hili linavyotazamwa kijuujuu.

Ikumbukwe kwamba Mwaka 1932, wakati wa mkoloni, ilitungwa sheria ya barabara nchini, sheria hii inatambua na kuelezea uwapo wa barabara za umma nchini. Kiambatanisho cha sheria hii kinaitaja barabara itokayo Morogoro mpaka Iringa, maarufu kama barabara ya Morogoro kama barabara ya umma, pamoja na mambo mengine, sheria hii inampa waziri mwenye dhamana na barabara uwezo wa kuamua juu ya upana muafaka wa barabara za umma kwa kutoa tangazo kwenye gazeti la serikali.

Mnamo mwaka 1967, waziri mwenye dhamana ya barabara nchini alitoa notisi namba 161 kwenye gazeti la serikali, kupitia tangazo hilo upana wa barabara uliongezwa kutoka futi 33 za mwaka 1932 na kufikia futi 75, hii ni kutoka katikati.

Sheria hii ya mwaka 1967 ndio umekuwa msingi wa 'bomoa bomoa' na 'chukua chukua' inayotekelezwa na serikali chini ya mwavuli wa kile kinachojuulikana kama upanuzi wa barabara ya Morogoro. Hata hivyo ni vyema ikumbukwe kuwa tangazo hilo la serikali halikueleza juu ya maeneo yanayo milikiwa na watu binafsi.

Hivyo mamlaka husika zirejee kwamba utekelezaji wa sheria hauzingatii kikamilifu wakazi ambao wameyamiliki maeneo hayo kabla ya mwaka 1967 ambao kimsingi sheria hii imewakuta,hivyo wanahaki ya kulipwa fidia. Pamoja na ukweli kuwa katika miaka hiyo majengo yalikuwa bado hayajatamalaki lakini sehemu kubwa ya ardhi ilikuwa ni ama mashamba ya watu au maeneo ya ufugaji ambayo kwa muda wote huo yamekuwa yakirithishwa au kuuzwa vizazi hadi vizazi mpaka kufikia hatua ya sasa ya kuendelezwa. Kwa serikali inayofuata sheria zinazojali haki, watu hawa wanastahili fidia kwa kuwa sheria hii iliwakuta.

Ikumbukwe pia kwamba baada ya Barabara ya Morogoro kukamilika miaka ya mwanzoni mwa sabini, serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilianzisha kote nchini vijiji vya ujamaa na kuhamishia watu katika vijiji hivyo. Maeneo ya kati ya Ubungo na Kiluvya yalikuwa sehemu ya vijiji hivyo na watu wakahamishiwa katika maeneo hayo kwa ajili ya makazi. Dar es salaam ilitangazwa kama eneo la mjini mwaka 1985 bila ya wananchi wa maeneo husika kushirikishwa kwa ukamilifu.

Hivyo ni muhimu kwa mamlaka husika kurejea ukweli kwamba Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 kifungu cha 15 kinatambua haki za watu walioishi katika vijiji kati ya tarehe 1 Januari 1970 na tarehe 31 Disemba mwaka 1977; hivyo kimsingi haki za wananchi wa eneo kati ya Ubungo na Kiluvya walioanza makazi yao katika kipindi husika zinapaswa kuthaminiwa na kulindwa.

Mamlaka husika zikumbuke kwamba mwaka 2001 bila kuzingatia sheria hiyo ya ardhi Wizara ya husika iliingilia makazi ya wananchi na kuongeza ukubwa wa eneo la hifadhi ya barabara kuwa mita 120 kila upande wa Barabara ya Morogoro.

Izingatiwe pia kwamba mwaka 2009 Waziri wa Miundombinu wa wakati huo Dr Shukuru Kawambwa alitoa kanuni kupitia gazeti la serikali namba 21 na 23 la Januari 2009 zilizopunguza eneo hilo kutoka mita 120 mpaka mita 60 kwa pande zote mbili za barabara katika maeneo mengi, mchakato huu nao ulifanyika kimya kimya bila wananchi kupewa taarifa za wazi na za kina.

Katika kanuni hizo maeneo mengi ya barabara ya Morogoro nchi nzima yametengwa kuwa mita kati ya 30 na 60 kwa pande zote mbili isipokuwa ya kutoka Ubungo mpaka Kiluvya ambayo yametengwa kwa kiwango kikubwa zaidi bila kuzingatia kwamba baadhi ya maeneo hayo yalishatolewa kihalali kwa wananchi kupitia sheria nyingine kama maeneo ya makazi kama nilivyoeleza awali. Hivyo, katika mazingira hayo, ikiwa serikali ina mpango wa kuongeza ukubwa wa barabara ziada ya eneo ambalo tayari lilishatolewa kwa wananchi na wajibu wa serikali kuhakikisha wananchi hao wanapata fidia stahili.

Baada ya sheria zingine kuwapa haki ya kuanzisha vijiji na baadaye miji Serikali iliwapa uhalali zaidi wa kuwa na makazi rasmi katika maeneo hayo kwa kuwapelekea huduma za msingi ambazo kisheria hutolewa maeneo halali yanayo tambulika kisheria. Serikali imewawekea miundo mbinu ya umeme, maji, simu na wengine wamepewa mpaka hati miliki na wizara ya ardhi. Iweje wizara ya ujenzi imwambie mtu kuwa ardhi anayo imiliki si halali wakati amesha milikishwa ardhi hiyohiyo na wizara ya ardhi? Au wizara ya ujenzi na ile ya ardhi ziko chini ya serikali mbili tofauti?

Kimsingi mimi kama mwakilishi wa wananchi wa eneo husika, naunga mkono suala la miradi ya maendeleo katika maeneo yetu; hata hivyo miradi hiyo lazima izingatie vile vile haki na stahili za wananchi wanaoondolewa kupisha miradi husika. Na ni muhimu kwa mchakato mzima kuwa shirikishi na taarifa sahihi kutolewa kwa wakati. Hivyo, pamoja na mikutano na taarifa ambazo nahimiza mamlaka husika kuzitoa na mimi kwa upande wangu nitatembelea maeneo yanayogusudiwa kubomolewa na nitafanya mikutano na wananchi kuhusu suala husika pindi nikirejea Dar es salaam. Aidha, natoa rai kwa wananchi wote wa maeneo husika ambao wanaamini kwamba haki zao zinavunjwa waweze kuunganisha nguvu ya umma katika kuhimiza uwajibikaji na kufuatilia stahili zao kama sehemu ya kutimiza wajibu wao wa kiraia kwa maendeleo ya kaya zao na taifa kwa ujumla.

Imetolewa safarini toka Dodoma tarehe 20 Februari 2011:

John Mnyika (Mb)
Jimbo la Ubungo

Kwa mara ya kwanza nimeona Mbunge Mnyika umenena mambo mazito. Sasa tunangoja ufuatiliaji wako na utekelezaji wa ahadi zako ndani ya tamko lako.
 
Kwa mara ya kwanza nimeona Mbunge Mnyika umenena mambo mazito. Sasa tunangoja ufuatiliaji wako na utekelezaji wa ahadi zako ndani ya tamko lako.

heeee mara ya kwanza?? aisee wewe ni Mlibya nini??huwezi kuwa Mtanzania wewe.
 
Mhh kaka hii kauli NAMUUNGA MKONO FREEMAN AIKAELI MBOWE AGOMBEE URAISI 2015" Imekaaje??? Mshaanza kapeni za urais 2015??? Mi ninahofu kauli hii itawagawa mapema saana na mtaanza kugombana kabla hata 2015 kufika. Ushauli wangu: IFUTE KAULI MBIU HII

Aliyepost sio Mnyika......
 
Mkuu hiyo sijakubaliana nayo, itatuangusha. Au unaonaje?

Zitto kabwe katangaza kugombea Urais 2015 na Mnyika katangaza kumuunga mkono Mbowe kugombea Urais 2015, mmmmh patamu hapo kumbe mpasuko hauko CCM peke yake.!!!!!!!!![/QUOTE]

Angalia kwa makini, aliyepost ni son of peasant na sio Mnyika
 
Mnyika anatafuta sifa za kitoto na kijinga. Kuna mtu leo hapa kamuomba atafute suluhisho la foleni ya barabara ya Morogoro sasa itaondokaje kama barabara hazitapanuliwa. Na, je, kama mtu kajenga katika road researve watu wake kujadiliana wakati wananchi na uchumi wa nchi unaharibika kutokana na wakazi wengi kukaa katika foleni. Tatizo la vijana hawa wa upinzani ni kudhani kupinga kila jambo ndio kupata kura ama kulalamika kila wakati ndio kujiona kuwa karibu na wananchi. My take kwa Mnyika: Kugombea ni jambo moja na kushinda na kuongoza ni jingine. Huu si wakati wa kampeni hivyo kama uliwadanganya wananchi ili wakupe kura haya matamko yako hayatasaidia lolote. Ni wakati uwaendee tena na kuwapa ukweli kuwa utawala wa sheria ni mihimu na barabara pia ni muhimu kwa ajili yao na nchi. Wasitazame maslahi yao na kushindwa kutambua njia hupitwa na wote. Tena walio na haki ya kulipwa siamini kama wataachwa maana utaratibu wa malipo umekuwa ukifanyika na inaposhindikana huwezi kumbomolea nyumba mtu bila kufuata sheria, hivyo wanaweza kwenda mahakamani na mahakama kuamua vinginevyo

Sheria ya barabara na Kanuni zake zilivyopitishwa kupitia Tangazo la Serikali Na 161 la tarehe 5/5/1967, Ibara ya 2 inatamka wazi wazi kuwa “hifadhi la barabara kuu zote nchini (Trunk road) ni Futi 75 au Mita 22.86 tu.Katika Sheria ya Barabara namba 13 ya 2007, na Kanuni zake zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali Na 21 la Tar 23 Januari 2009, eneo hilo liliongezwa kufikia Mita 60 kwa maana ya mita 30 kila upande.

Ibara ya 27 ya Kanuni za Sheria ya barabara zilizopitishwa kwa tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009, inatamka kuwa upana wa njia ya barabara (lane) katika barabara zote kuu hapa nchini (Trunk roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25. Hivyo hifadhi ya barabara ya Mita 60, lina uwezo wa kuzalisha jumla ya njia za barabara (lanes) 18, yaani (lanes) 9 za kuelekea upande mmoja na 9 kuelekea upande mwingine.

Kwa kuwa Serikalli ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya "Operesheni Vijiji" ndio iliwahamishia wanachi katika maneo hayo na kuwagawia ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara, yaani nje ya Mita Futi 75 wakati huo aua sasa Miata 60. Itakumbukwa kuwa wakati wa operesheni vijiji wananchi walikuwa wakibomolewa na kuchomewa makazi yao yaliyokuwa maporini katika mashambayao na kulazimishwa kuhamia vijijni. Ambapo baadaye Serikali ilifikia hatua ya kuwamilikisha kwa kuwapatia hati miliki

Sio haki hata kidogo kwa wananchi hao kubomolewa kwa kuwa upanuzi wa barabara ya Morogoro unaweza kufanyika bila ya kuwabughudhi wananchi waliopo katika eneo lisilohusika na upanuzi wa barabara (nje ya Mita 60) katika eneo la Ubungo hadi Kiruvia.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2008, wafadhili wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) waliamua kuwalipia fidia wanachi waishio katika road reserve kati ya Kimara hadi Magomeni kutokana na ukweli kuwa waliwekwa hapo na Serikali. fidia hizo wzilizwahusu haid wapangaji Na kwa wale waliokuwa wakitumia majengo hayo kwa shughuli za kuingiza vipato walilipwa fidia ya upotevu wa mapato kwa muji bu wa sheria za fidia za Tanzania.
 
huu ndio ujinga unaoturudisha nyuma. Mtu kajenga kwenye eneo si lake unaongea nae nini? Wacha wabomolewe barabara zijengwe. Tumepata waziri chapa kazi tusiingize siasa mwache awajibike. Mnyika unaanza vibaya! Statement yako upuuzi mtupu.

Miaka ya 1970 wakati wa opersheni vijiji, wananchi walikuwa wakibomolewa na kuchomewa nyumba zao zilizokuwa katika mashamba yao na kuhamishiwa katika vijiji vya ujamaa vilivyoanishwa. Kati ya Ubungo hadi Kiruvia vilianzishwa vijiji pia. Wanavijiji walikuwa wakigawiwa ardhi kwa kuacha hifadhi ya Futi 75 vkama inavyosisitizwa na Ibara 2 ya Sheria ya barabara tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05 Februariu 1967.

Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 kinatamka kuwa “Ugawaji wa ardhi uliofanywa au kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya tarehe 01 Januari 1970 na tarehe 31 Desemba 1977, kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila ya kuzingatia sheria yeyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu wa kisheria kwa kundi la waliogawiwa ardhi hiyo na pia sheria hiyo kufuta haki na wajibu wowote aliokuwa nao mtu chini ya sheria yoyote ambayo inawezekana ilikuwapo kabla ya ugawaji wa ardhi hiyo kufanyika”.
Kifungu cha 16 cha sheria hiyo kinatamka “kwa madhumuni ya kuepusha mashaka na ili kuwezesha kuwapo kwa usalama wa miliki ya ardhi na hivyo kuchangia maendeleo ya ardhi ya kijiji masharti ya kifungu cha 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na Halmshauri ya Kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya tarehe 01 Januari 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika sheria hii kwamba badala ya tarehe ya zilizotajwa katika Kifungu cha 15, kumewekwa tarehe kati ya tarehe 01 Januari 1978 na tarehe ya sheria hii kuanza kutumika”.

Kwa mujibu wa vifungu hivyo hapo juu wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji vilivyokuwepo kati ya Ubungo hadi Kiruvia wana haki ya kumiliki ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara, yaani iliyoko nje ya Futi 75 kama inavyoelezwa na Ibara ya 2 ya Sheria ya barabara tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05 Februariu 1967.
 
Weeh Mh.Mnyika sasa unaanza kuchemka, nakukumbusha tu kama hujawahi kuambiwa, barabara kutoka Mbezi mwisho kupitia Madale(kwa Mrh.Mzee Rashid Kawawa) mpaka Bagamoyo road ilitakiwa iwe kiwango cha lami, na barabara hii inaunganisha segerea mpaka JKN international airport.

Tangu mwanzoni wa 2000, serikali ilishatoa notisi na kuonyesha mipaka ya barabara lkn kinyume chake wananchi walianza kujenga kwa kasi wakisubiri hizo hizo fidia unazosema, mpaka leo kesi iko court na barabara haipitiki, kwa ushauri tuu nikiwa mkazi wa maeneo hayo, hao unaowatetea hawataki hata kutoa sumuni kulima barabara ikiharibika utasikia ni ya Tanroads, sasa bila hatua kama za Dr. Magufuli hatutaenda bwana John, sitaki kuamini kama umeanza kucheza mchezo wa Mr. Nice Guy, kama ni hivyo Ubungo sio mahala pako kaka!

Mujuni2 hao wanachi wa Mbezi wengi wao waliahamishiwa hapo wakati wa operesheni vijiji, hichi kilikuwa ni Kijiji cha Ujamaa hadi mwaka 1985 vijiji vyote 52 vilipowekwa chini ya Mipango Miji, Tatizo ni kuwa wakati nchi nzima Rooad Resetrve ni Mita 60 katika hali ya kutaka kuwakomoa watu wanaoishi kati ya Ubungo hadi Kiruvia Road \Reserve imewekwa Mita 120 kalai Upande wa barabara.
Ibara ya 27 ya Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009 inatamka kuwa upana wa njia ya barabara (lane) katika barabara zote kuu hapa nchini (Trunk roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25. Hivyo hifadhi ya barabara ya Mita 60, lina uwezo wa kuzalisha jumla ya njia za barabara (lanes) 18, yaani (lanes) 9 za kuelekea upande mmoja na 9 kuelekea upande mwingine.

Je ni kwanini Ubungo hadi Kiruvia kuwe na upana tofauti? Ilihali hao wananchi waliwekwa hapo na Serikali yenyewe kupitia operesheni vijiji?
Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 kinatamka kuwa “Ugawaji wa ardhi uliofanywa au kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya tarehe 01 Januari 1970 na tarehe 31 Desemba 1977, kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila ya kuzingatia sheria yeyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu wa kisheria kwa kundi la waliogawiwa ardhi hiyo na pia sheria hiyo kufuta haki na wajibu wowote aliokuwa nao mtu chini ya sheria yoyote ambayo inawezekana ilikuwapo kabla ya ugawaji wa ardhi hiyo kufanyika”.
Kifungu cha 16 cha sheria hiyo kinatamka “kwa madhumuni ya kuepusha mashaka na ili kuwezesha kuwapo kwa usalama wa miliki ya ardhi na hivyo kuchangia maendeleo ya ardhi ya kijiji masharti ya kifungu cha 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na Halmshauri ya Kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya tarehe 01 Januari 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika sheria hii kwamba badala ya tarehe ya zilizotajwa katika Kifungu cha 15, kumewekwa tarehe kati ya tarehe 01 Januari 1978 na tarehe ya sheria hii kuanza kutumika”.
SULUHISHO LA MGOGORO HUU LITAPATIKANA ENDAPO YAFUTAYO YATAFANYIKA:-
a) Kwa kuwa sera ya “Operesheni Vijiji” ni sera ya TANU na baadaye CCM, na ni moja ya sera nzuri sana ambazo Tanzania imewahi kuwa nazo zilizochangia kujenga mshikamano, umoja, utulivu na amani ya Tanzania na watanzania kwa ujumla. Vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 ni lazima viheshimiwe na wananchi waliokuwepo katika vijiji vya ujamaa kabla ya maeneo kati ya Ubungo hadi Kiruvia kuingizwa katika Sheria ya Mipango Miji wana haki ya kumiliki ardhi waliyogawiwa na kuwa nayo kihalali.
b) Kwa kuwa mwaka 2001, wakati Wizara ya Ujenzi inatoa amri kwa mkandarasi wake kuingia Futi 400 au Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi pande zote mbali za barabara, Wizara ya Ujenzi haikuwa imeshirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zingeweza kuisaidia kuwatambua akina nani walikuwepo katika vijiji na akina nani hawakuwepo. Wizara ya Ujenzi haina budi kupunguza matumizi ya nguvu na kauli za kibabe katika masuala yanayowahusu wananchi na badala yake ishirkishe ngazi zilizotajwa katika utekelezaji wa mipango yake, ikiwemo utatuzi wa migogoro ya ardhi inayohusu hifadhi za barabara. Katika hili Wizara ya Ujenzi iwe tayari kupokea ushauri wa wadau wengine. Kwani sote tunajenga nyumba moja (Tanzania) kwanini tugombee fito!
c) Kwa kuwa Sheria ya barabara na Kanuni zake zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967 na Sheria ya barabar nbamba 13 ya 2007 na Kanuni zake zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali No 21 la Tar 23 Januairi 2009 vyote vinatambua kuwa eneo la upana wa Mita 60 linatosha kwa maendeelo ya barabara kuu hapa nchini. Ili kumaliza mgogoro huu upana huo ndio uwe hifadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia kama ilivyo kwa nchi nzima. Ni kuwakose haki wananchi wa maeno haya kuwawekea hifadhi kubwa zaidi kuloko maeneo mengine yaliyopita barabara kuu.
d) Kwa kuwa wananchi waliokuwa wanavijiji wa vijiji vilivyoanzishwa kando kando ya barabara ya Morogoro kati ya eneo la Ubungo hadi Kiruvia wana haki ya kumiliki ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara (iliyoko nje ya Futi 75) kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyoonyesha kwa kuwamilikisha kwa kuwapatia hati miliki baadhi yao. Wizara ya Ujenzi ifanyie Kanuni zake marekebisho ili eneo la hiufadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia iwe Mita 60 kama ilivyo maeno mengine zinakopita barabara kuu (Trunk Roads) na imwagize wakala wake TANROAD kurekebisha mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara kuendana na marekebisho hayo.
e) Kwa kuwa wananchi waliokuwa wanavijiji wa vijiji vilivyoanzishwa kando kando ya barabara ya Morogoro kati ya eneo la Ubungo hadi Kiruvia wana haki ya kumiliki ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara (iliyoko nje ya Futi 75) kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyoonyesha kwa kuwamilikisha kwa kuwapatia hati miliki baadhi yao. Endapo Wizara ya Ujenzi inalitaka eneo hilo iwe tayari kuwalipa fidia wananchi hawa kwa maendelezo waliyoyafanya katik ardhi hiyo.

Mujuni2 hao wanachi wa Mbezi wengi wao waliahamishiwa hapo wakati wa operesheni vijiji, hichi kilikuwa ni Kijiji cha Ujamaa hadi mwaka 1985 vijiji vyote 52 vilipowekwa chini ya Mipango Miji, Tatizo ni kuwa wakati nchi nzima Rooad Resetrve ni Mita 60 katika hali ya kutaka kuwakomoa watu wanaoishi kati ya Ubungo hadi Kiruvia Road \Reserve imewekwa Mita 120 kalai Upande wa barabara.
Ibara ya 27 ya Kanuni za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009 inatamka kuwa upana wa njia ya barabara (lane) katika barabara zote kuu hapa nchini (Trunk roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25. Hivyo hifadhi ya barabara ya Mita 60, lina uwezo wa kuzalisha jumla ya njia za barabara (lanes) 18, yaani (lanes) 9 za kuelekea upande mmoja na 9 kuelekea upande mwingine.

SULUHISHO LA MGOGORO HUU LITAPATIKANA ENDAPO YAFUTAYO YATAFANYIKA:-
a) Kwa kuwa sera ya “Operesheni Vijiji” ni sera ya TANU na baadaye CCM, na ni moja ya sera nzuri sana ambazo Tanzania imewahi kuwa nazo zilizochangia kujenga mshikamano, umoja, utulivu na amani ya Tanzania na watanzania kwa ujumla. Vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 ni lazima viheshimiwe na wananchi waliokuwepo katika vijiji vya ujamaa kabla ya maeneo kati ya Ubungo hadi Kiruvia kuingizwa katika Sheria ya Mipango Miji wana haki ya kumiliki ardhi waliyogawiwa na kuwa nayo kihalali.
b) Kwa kuwa mwaka 2001, wakati Wizara ya Ujenzi inatoa amri kwa mkandarasi wake kuingia Futi 400 au Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi pande zote mbali za barabara, Wizara ya Ujenzi haikuwa imeshirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zingeweza kuisaidia kuwatambua akina nani walikuwepo katika vijiji na akina nani hawakuwepo. Wizara ya Ujenzi haina budi kupunguza matumizi ya nguvu na kauli za kibabe katika masuala yanayowahusu wananchi na badala yake ishirkishe ngazi zilizotajwa katika utekelezaji wa mipango yake, ikiwemo utatuzi wa migogoro ya ardhi inayohusu hifadhi za barabara. Katika hili Wizara ya Ujenzi iwe tayari kupokea ushauri wa wadau wengine. Kwani sote tunajenga nyumba moja (Tanzania) kwanini tugombee fito!
c) Kwa kuwa Sheria ya barabara na Kanuni zake zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967 na Sheria ya barabar nbamba 13 ya 2007 na Kanuni zake zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali No 21 la Tar 23 Januairi 2009 vyote vinatambua kuwa eneo la upana wa Mita 60 linatosha kwa maendeelo ya barabara kuu hapa nchini. Ili kumaliza mgogoro huu upana huo ndio uwe hifadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia kama ilivyo kwa nchi nzima. Ni kuwakose haki wananchi wa maeno haya kuwawekea hifadhi kubwa zaidi kuloko maeneo mengine yaliyopita barabara kuu.
d) Kwa kuwa wananchi waliokuwa wanavijiji wa vijiji vilivyoanzishwa kando kando ya barabara ya Morogoro kati ya eneo la Ubungo hadi Kiruvia wana haki ya kumiliki ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara (iliyoko nje ya Futi 75) kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyoonyesha kwa kuwamilikisha kwa kuwapatia hati miliki baadhi yao. Wizara ya Ujenzi ifanyie Kanuni zake marekebisho ili eneo la hiufadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia iwe Mita 60 kama ilivyo maeno mengine zinakopita barabara kuu (Trunk Roads) na imwagize wakala wake TANROAD kurekebisha mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara kuendana na marekebisho hayo.
e) Kwa kuwa wananchi waliokuwa wanavijiji wa vijiji vilivyoanzishwa kando kando ya barabara ya Morogoro kati ya eneo la Ubungo hadi Kiruvia wana haki ya kumiliki ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara (iliyoko nje ya Futi 75) kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyoonyesha kwa kuwamilikisha kwa kuwapatia hati miliki baadhi yao. Endapo Wizara ya Ujenzi inalitaka eneo hilo iwe tayari kuwalipa fidia wananchi hawa kwa maendelezo waliyoyafanya katik ardhi hiyo.

Dear Jatropha

Sijui kama haya maelezo yako mazuri yanamfikia Mh. Magufuli. Lakini hata hivyo huu ni mwanzo mzuri. Kwakuwa Mh Mnyika ni mwana JF basi auchukue huu ushauri wako na kuufanyia kazi.

BTW, hivi Mh. Mwakyembe ni member wa JF, hata kama sio member lakini kama kuna mtu anaweza kumfikishia huu ushauri wako anaweza kufanya hivyoo, maana Mh. Mwakyembe itakuwa rahisi yeye kuelewa mantinki ya hoja yako kuliko Mh. Magufuli. (No disrepect to Magufuli lkn kwasababu Mwakyembe ni lawyer na hii hoja imekaa kisheria zaidi).

Kama inashindikana basi ndg. Jatropa unaweza kutumia mtandao wa bunge kumfikishia mwakyembe mapendekezo yako TOVUTI www.parliament.gotz

Haki hupiganiwa haitolewi kwenye kisahani cha dhahabu
 
Mnyika anatafuta sifa za kitoto na kijinga. Kuna mtu leo hapa kamuomba atafute suluhisho la foleni ya barabara ya Morogoro sasa itaondokaje kama barabara hazitapanuliwa. Na, je, kama mtu kajenga katika road researve watu wake kujadiliana wakati wananchi na uchumi wa nchi unaharibika kutokana na wakazi wengi kukaa katika foleni. Tatizo la vijana hawa wa upinzani ni kudhani kupinga kila jambo ndio kupata kura ama kulalamika kila wakati ndio kujiona kuwa karibu na wananchi. My take kwa Mnyika: Kugombea ni jambo moja na kushinda na kuongoza ni jingine. Huu si wakati wa kampeni hivyo kama uliwadanganya wananchi ili wakupe kura haya matamko yako hayatasaidia lolote. Ni wakati uwaendee tena na kuwapa ukweli kuwa utawala wa sheria ni mihimu na barabara pia ni muhimu kwa ajili yao na nchi. Wasitazame maslahi yao na kushindwa kutambua njia hupitwa na wote. Tena walio na haki ya kulipwa siamini kama wataachwa maana utaratibu wa malipo umekuwa ukifanyika na inaposhindikana huwezi kumbomolea nyumba mtu bila kufuata sheria, hivyo wanaweza kwenda mahakamani na mahakama kuamua vinginevyo[/QUOTE

Ndugu yangu naomba ufahamu huyu ndie mwakilishi wetu sisi watu wa jimbo la ubungo,Vilevile sisi sote ni watanzania tunayo haki ya kuhoji jambo lolote liwe baya au zuri ilimradi tu tusivunje sheria za nchi.Sasa basi selekari inapo hamua kufanya jambo fulani kama upanuzi wa barabara inapaswa kutufahamisha vizuri sisi ambao tunatazamiwa kupata hasara au faida kutokana na huu mradi,ndio maana sisi ambao nyumba zetu zimewekwa alama kwa ajiri ya upanuzi huo imebidi tumtume mbunge wetu afuatilie swala hili kwa kina ili tuweze kujua nini kitafuata sio tunaishi kwa hofu ndani ya nchi yetu.Naomba uelewe sisi tunahitaji maelezo na wala sio kuzuia upanuzi wa barabara.
Alafu naomba ufahamu mbunge sisi ndio mabosi wake,sisi ndio tumemchagua na sisi ndio tunae mtuma kwa hiyo tamko lake si kwa ajiri ya maslai yake bali ni kwa maslai ya sisi waathirika,na yeye akituletea maelezo ambayo ayana manufaa kwetu tutamuajibisha.
 
Tumekuelewa mh. Mnyika, lkn please please tunaomba ufute kauli mbiu yako hapo chini ya thread maana haina kujenga bali utagawa wanachama tu kwa sasa.

Kwa sasa ni muhimu kushughulikia matatizo ya nchi na muda wa kampeni bado, hii italeta hisia tofauti miongoni mwetu....
 
Dear Jatropha

Sijui kama haya maelezo yako mazuri yanamfikia Mh. Magufuli. Lakini hata hivyo huu ni mwanzo mzuri. Kwakuwa Mh Mnyika ni mwana JF basi auchukue huu ushauri wako na kuufanyia kazi.

BTW, hivi Mh. Mwakyembe ni member wa JF, hata kama sio member lakini kama kuna mtu anaweza kumfikishia huu ushauri wako anaweza kufanya hivyoo, maana Mh. Mwakyembe itakuwa rahisi yeye kuelewa mantinki ya hoja yako kuliko Mh. Magufuli. (No disrepect to Magufuli lkn kwasababu Mwakyembe ni lawyer na hii hoja imekaa kisheria zaidi).

Kama inashindikana basi ndg. Jatropa unaweza kutumia mtandao wa bunge kumfikishia mwakyembe mapendekezo yako TOVUTI www.parliament.gotz

Haki hupiganiwa haitolewi kwenye kisahani cha dhahabu

Ndugu Bobuk,
Mhe John Magufuli ni mtu fedhuli na kiburi sana, anafahamu kabisa kuwa Serikali za Mitaa kwa maana ya Halmashauri za Miji na Wilaya ni wakala wa Serikali Kuu, hata Waziri wq Ardhi Mhe Anna Tibaijuka alikiri hivyo hivi karibuni. Mwaka 2001, Magufuli alipotoa agizo kwa mkandarasi aliyewekwa na wizara kuvamia ardhi na makazi wa wanachi Mita 120 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro pande zote mbili za barabara na kupanda mawe na mabango yanaoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara hakushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa. Kwani alifahamu kuwa akishirikisha ngazi hizo zitampa ukweli kuwa wananchi hao wana haki ya kuwa katika ardhi isiyohusika na upanuzi wa barabara, yaani nje ya Futi 75 kama inavyoonyeshwa na Ibara ya 2 ya Sheria ya barabara Kanuni zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 5 Februari 1967. Mkandarasi huyo alifanya kazi hiyo kima kimya.

Kanuni za utawala bora na wa sheria unataka watumishi wote wa Serikali Kuu kupiga ripoti katika Ofisi za Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa na kuweka sahihi katika vitabu vya wageni kabla ya kuingia katika maeneo ya Kata na Mitaa husika. Mbona watumishi wa TANROAD, tena wakiwa chini ya Magufuli pekee, hawafanyi hivyo?.

Kwanini watumishi hao hao wa TANROAD wakiwa chini ya mawaziri wengine wanzingatia kanuni hizi za utawala bora? Kama sio Mhe John Magufuli kutumia ubabe na undava undava dhidi ya wananchi?.

Kitendo cha Mameya na Wakurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kukaa kimya 2001, na kuachia Magufuli avuruge "Mater Plan ya Jiji la Dar es Salaam ya 1979" ambayo ilionyesha wazi kuwa hifadhi ya barabara ya Morogoro kati ya Ubungo hadi Kiruvia ni Futi 75 kama inavyoonyeshwa na Ibara ya 2 ya Sheria ta barabara Kanuni zilizopitishwa kupitia Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 5 Februari 1967. Ndio kimemtia Magufuli kiburi cha kuvuruga vyanzo vya mapato vya Jiji na Manispaa zake 201 ikiwemo Mabango ya Matangazo. Inashangaza sana kuona Mameya na Wakurugenzi wa Jiji na Manispaa zake wakikaa kimya na kuruhusu Mgambo wa Jiji kuendelea kufukuzana na Mama Ntilie na Wamachinga na kuwaachaia wahuni kutoka TANROAD (wasio piga ripoti katika Serikali za mitaa za maeneo husika) wakichafua Mabango yaliyowekwa kwa kuingia mikataba na Jiji na Manispaa. Ilitakiwa wahuni hao kutoka TANROAD wakamatwe na kufikishwa mahakama za Jiji na kuhukumiwa kwenda jela mara moja.

Aidha Jiji linatakiwa kucondemn jengo bovu zilizopo ofisi za Wizara ya Miundo Mbinu na kuhakikisha Mhe John Magufuli anahamia Dodoma kwa kukosa adabu kwa wenjeji wake ambao ni Halmashauri ya Jiji na Manispaa husika, Vivyo hivyo kwa TANROAD.

Mbunge wa Ubungo Mhe Johna Mnyika anatakiwa kutambua kuwa Mhe John magufuli anatumia OMBWE la uongozi lililopo kutoka ngazi ya Taifa, Jiji ahdi Manispaa kufanikisha mikakati yake ya kujipatia umaarufu kutoka kwa watanzania wasio na kumbukumbu kuwa mradi wa mabasi yaendayo kasi ulilipa fidia kwa wakazi waliokuwa wakiishi katika eneo linalodaiwa kuwa ni hifadhi ya barabara kutoka Kimara hadi Magomeni 2008. Magufuli anatumia tatizo la foleni na jina la mradi huo kujitafutia umaarufu kwa kutaka kuwabomolea wananchi maskini nyumba zao ambazo nyingi ziko nje ya eneo linalohusika na upanuzi wa barabara yaani kuwa nje ya Futi 75 na Mita 60 kama sheria za barabara zinavyoelekeza. Mbunge wetu anatakiwa kuacha mtindo wa kutoa matamko kama alivyokuwa akifanya wakati akiwa kiongozi wa chama kidogo cha siasa CHADEMA; hivi sasa ni mbunge wa Jimbo lenye wapiga kura wengi zaidi kuliko Jimbo lolote hivyo anatakiwa kuziba OMBWE la uongozi lililopo kwa kuwataka wananchi wasiwaruhusu watumishi wa TANROAD kuingia ndani ya ardhi na makazi yao kwa zaidi ya Mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande,kwani eneo zaidi ya Mita 30 lina mgogoro kati ya wananchi wanaoishi hapo na Mhe John Magufuli (binafsi) kwani wananchi wamekuwa wakiishi katiak eno hilo kwa kugawiwa kihalali na utawala wa hayati Mwalimu Nyerere tokea Mhe Magufuli akiwa anasoma shule ya Msingi huko kwao Chato.

Asante mwanawane kwa kujibu hoja za wanawatanzania. Good start mh. I can see responsiveness in you big up. Kidumu chama cha chadema. Umngu ibariki Tanzania
 
Tatizo si taa bali wingi wa magari....Foleni hazisababishwi na kukosekana taa au polisi peke yake bali wingi wa magari kupita uwezo wa barabara kumudu..
Sasa kwa nini huo wingi wa magari unaonekana kwenye makutano tu?

Halafu, ni kuwa impractical kutufananisha na France. Too utopian. Tanzania yetu hii mmejaa mafundi mchundo ambao hata kujenga kibarabara hamuwezi (asingekuwepo Mchina hapa, ushamuona Mchina anajenga barabara Paris? Kama umepita/umeishi hiyo miji ya Magharibi na Latin America, tuambie, ushaona Mchina kavaa helmet Copenhagen huko?), ndo tutaweza kujenga hiyo mipango miji ya La Defense na Brazil, please!

Ndo maana, kwa kuanzia, napendekeza kinachowezekana. Small-minded you may call it, but it is the practical model you can be afford technically and fiscally.
 
Back
Top Bottom