Tamko la mbunge Ubungo kuhusu bomoa bomoa ya Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la mbunge Ubungo kuhusu bomoa bomoa ya Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Feb 22, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  JOHN JOHN MNYIKA
  MBUNGE UBUNGO

  Tamko langu la awali kuhusu kuwekwa X katika majengo ya pembeni ya Barabara ya Morogoro

  Katika kipindi cha wiki moja mfululizo kuanzia tarehe 11 mpaka 17 Februari 2011 nikiwa bungeni Dodoma nimekuwa nikipokea simu na sms toka kwa wananchi wakilalamikia hatua ya wafanyakazi wa wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam (TANROADS) kupita katika nyumba zao zilizopembezoni mwa barabara ya Morogoro bila wakazi kupewa notisi na kuweka alama za "X" ama "BOMOA TNRD".

  Aidha nimesoma kwenye baadhi ya vyombo vya habari (mf. NIPASHE Toleo na. 056929 la tarehe 18 Februari 2011 Uk 1 na 8) habari yenye kichwa "bomoa bomoa nyingine kukumba wakazi wa Ubungo/Dar"

  Habari hiyo imemnukuu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, James Nyabakari akiwataka watu wote waliojenga kwenye hifadhi ya Barabara kubomoa wenyewe na kwamba serikali haitawalipa kwa kuwa ni wavamizi na kwamba watakaolipwa ni wale tu ambao serikali itahitaji maeneo yao.

  Taarifa zinazoelezwa ni kwamba alama hizo zimewekwa mita 90 pande zote mbili za barabara kuanzia maeneo ya Ubungo mpaka Kimara, na kwamba hali hiyo itawagusa pia wananchi wa Mbezi mpaka Kiluvya katika hatua za baadaye.

  Nikiwa mwakilishi wa wananchi wa maeneo husika nimeshangazwa na hatua kubwa kama hizi za kiserikali kuchukuliwa bila kufanyika kwa mikutano ya umma ama walau kutoa taarifa ya kuelimisha umma kuhusu mipango husika inayotarajiwa kufanyika. Aidha nimeshangazwa zaidi na hatua kama hizo kuchukuliwa bila walau wawakilishi wa wananchi kama wenyeviti wa mitaa, madiwani na wabunge kuelezwa kwa kina mipango inayokusudiwa kufanyika na athari zake kwa wananchi wa maeneo husika. Utendaji kazi wa namna hii ni kinyume na misingi ya utawala bora inayotaka uwazi na pia ni chanzo cha migogoro isiyo ya lazima katika jamii.

  Nachukua fursa hii kutoa mwito kwa serikali ngazi ya wizara ya ujenzi, mkoa na wilaya kuhakikisha kwamba mikutano na wananchi inafanyika ama walau matangazo kwa umma yanatolewa kuhusu suala husika.

  Aidha mamlaka husika za kiserikali zitoe maelezo ya wazi kuhusu wananchi wanaostahili fidia na kutoa notisi ya muda wa kutosha kwa wakazi wenye majengo yanayostahili kubomolewa ili kupitisha barabara ya mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka (DART) na mipango mingine.

  Katika kufanya hivyo Serikali izingatie kuwa wapo wakazi wengi wenye kustahili kulipwa fidia kutokana na historia ya Barabara hiyo ya Morogoro kuliko ambavyo suala hili linavyotazamwa kijuujuu.

  Ikumbukwe kwamba Mwaka 1932, wakati wa mkoloni, ilitungwa sheria ya barabara nchini, sheria hii inatambua na kuelezea uwapo wa barabara za umma nchini. Kiambatanisho cha sheria hii kinaitaja barabara itokayo Morogoro mpaka Iringa, maarufu kama barabara ya Morogoro kama barabara ya umma, pamoja na mambo mengine, sheria hii inampa waziri mwenye dhamana na barabara uwezo wa kuamua juu ya upana muafaka wa barabara za umma kwa kutoa tangazo kwenye gazeti la serikali.

  Mnamo mwaka 1967, waziri mwenye dhamana ya barabara nchini alitoa notisi namba 161 kwenye gazeti la serikali, kupitia tangazo hilo upana wa barabara uliongezwa kutoka futi 33 za mwaka 1932 na kufikia futi 75, hii ni kutoka katikati.

  Sheria hii ya mwaka 1967 ndio umekuwa msingi wa 'bomoa bomoa' na 'chukua chukua' inayotekelezwa na serikali chini ya mwavuli wa kile kinachojuulikana kama upanuzi wa barabara ya Morogoro. Hata hivyo ni vyema ikumbukwe kuwa tangazo hilo la serikali halikueleza juu ya maeneo yanayo milikiwa na watu binafsi.

  Hivyo mamlaka husika zirejee kwamba utekelezaji wa sheria hauzingatii kikamilifu wakazi ambao wameyamiliki maeneo hayo kabla ya mwaka 1967 ambao kimsingi sheria hii imewakuta,hivyo wanahaki ya kulipwa fidia. Pamoja na ukweli kuwa katika miaka hiyo majengo yalikuwa bado hayajatamalaki lakini sehemu kubwa ya ardhi ilikuwa ni ama mashamba ya watu au maeneo ya ufugaji ambayo kwa muda wote huo yamekuwa yakirithishwa au kuuzwa vizazi hadi vizazi mpaka kufikia hatua ya sasa ya kuendelezwa. Kwa serikali inayofuata sheria zinazojali haki, watu hawa wanastahili fidia kwa kuwa sheria hii iliwakuta.

  Ikumbukwe pia kwamba baada ya Barabara ya Morogoro kukamilika miaka ya mwanzoni mwa sabini, serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ilianzisha kote nchini vijiji vya ujamaa na kuhamishia watu katika vijiji hivyo. Maeneo ya kati ya Ubungo na Kiluvya yalikuwa sehemu ya vijiji hivyo na watu wakahamishiwa katika maeneo hayo kwa ajili ya makazi. Dar es salaam ilitangazwa kama eneo la mjini mwaka 1985 bila ya wananchi wa maeneo husika kushirikishwa kwa ukamilifu.

  Hivyo ni muhimu kwa mamlaka husika kurejea ukweli kwamba Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 kifungu cha 15 kinatambua haki za watu walioishi katika vijiji kati ya tarehe 1 Januari 1970 na tarehe 31 Disemba mwaka 1977; hivyo kimsingi haki za wananchi wa eneo kati ya Ubungo na Kiluvya walioanza makazi yao katika kipindi husika zinapaswa kuthaminiwa na kulindwa.

  Mamlaka husika zikumbuke kwamba mwaka 2001 bila kuzingatia sheria hiyo ya ardhi Wizara ya husika iliingilia makazi ya wananchi na kuongeza ukubwa wa eneo la hifadhi ya barabara kuwa mita 120 kila upande wa Barabara ya Morogoro.

  Izingatiwe pia kwamba mwaka 2009 Waziri wa Miundombinu wa wakati huo Dr Shukuru Kawambwa alitoa kanuni kupitia gazeti la serikali namba 21 na 23 la Januari 2009 zilizopunguza eneo hilo kutoka mita 120 mpaka mita 60 kwa pande zote mbili za barabara katika maeneo mengi, mchakato huu nao ulifanyika kimya kimya bila wananchi kupewa taarifa za wazi na za kina.

  Katika kanuni hizo maeneo mengi ya barabara ya Morogoro nchi nzima yametengwa kuwa mita kati ya 30 na 60 kwa pande zote mbili isipokuwa ya kutoka Ubungo mpaka Kiluvya ambayo yametengwa kwa kiwango kikubwa zaidi bila kuzingatia kwamba baadhi ya maeneo hayo yalishatolewa kihalali kwa wananchi kupitia sheria nyingine kama maeneo ya makazi kama nilivyoeleza awali. Hivyo, katika mazingira hayo, ikiwa serikali ina mpango wa kuongeza ukubwa wa barabara ziada ya eneo ambalo tayari lilishatolewa kwa wananchi na wajibu wa serikali kuhakikisha wananchi hao wanapata fidia stahili.

  Baada ya sheria zingine kuwapa haki ya kuanzisha vijiji na baadaye miji Serikali iliwapa uhalali zaidi wa kuwa na makazi rasmi katika maeneo hayo kwa kuwapelekea huduma za msingi ambazo kisheria hutolewa maeneo halali yanayo tambulika kisheria. Serikali imewawekea miundo mbinu ya umeme, maji, simu na wengine wamepewa mpaka hati miliki na wizara ya ardhi. Iweje wizara ya ujenzi imwambie mtu kuwa ardhi anayo imiliki si halali wakati amesha milikishwa ardhi hiyohiyo na wizara ya ardhi? Au wizara ya ujenzi na ile ya ardhi ziko chini ya serikali mbili tofauti?

  Kimsingi mimi kama mwakilishi wa wananchi wa eneo husika, naunga mkono suala la miradi ya maendeleo katika maeneo yetu; hata hivyo miradi hiyo lazima izingatie vile vile haki na stahili za wananchi wanaoondolewa kupisha miradi husika. Na ni muhimu kwa mchakato mzima kuwa shirikishi na taarifa sahihi kutolewa kwa wakati. Hivyo, pamoja na mikutano na taarifa ambazo nahimiza mamlaka husika kuzitoa na mimi kwa upande wangu nitatembelea maeneo yanayogusudiwa kubomolewa na nitafanya mikutano na wananchi kuhusu suala husika pindi nikirejea Dar es salaam. Aidha, natoa rai kwa wananchi wote wa maeneo husika ambao wanaamini kwamba haki zao zinavunjwa waweze kuunganisha nguvu ya umma katika kuhimiza uwajibikaji na kufuatilia stahili zao kama sehemu ya kutimiza wajibu wao wa kiraia kwa maendeleo ya kaya zao na taifa kwa ujumla.

  Imetolewa safarini toka Dodoma tarehe 20 Februari 2011:

  John Mnyika (Mb)
  Jimbo la Ubungo
   
 2. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mhh kaka hii kauli NAMUUNGA MKONO FREEMAN AIKAELI MBOWE AGOMBEE URAISI 2015" Imekaaje??? Mshaanza kapeni za urais 2015??? Mi ninahofu kauli hii itawagawa mapema saana na mtaanza kugombana kabla hata 2015 kufika. Ushauli wangu: IFUTE KAULI MBIU HII
   
 3. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ""NAMUUNGA MKONO FREEMAN AIKAELI MBOWE AGOMBEE URAISI 2015""
  Nilivutiwa na heading ya thread yako ila nlipoona kauli kama hiyo apo juu... nikajisikia na uvivu wa kuisoma, naona umetumwa na chichiemu
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Babayah67 Itawagawa kina nani?? Yaani maoni ya Mtoto wa Mkulima (SoP) yatagawa CDM..

  Je, nikikwambia NAMUUNGA MKONO LOWASA AGOMBEE URAIS 2015 utasemaje??

  Tukirejea kwenye Maelezo ya Mh. Mnyika nadhani ni vema akaomba kukutana na Mh. Magufuli (waziri husika) wakazungumza na kupata maelezo ya kwenda kwa wananchi.
  We are getting tired na haya matamko ambayo hayana majibu ya matatizo ya wananchi.
  Matamko siku zote yana-serve matakwa ya kisiasa zaidi kuliko kupata ufumbuzi wa jambo husika.

  Mh Mnyika najua utakuwa Dar Es Salaam kwa sasa, tunaomba ulichokiandika ukifanyie kazi ili wananchi walio katika kadhia hii wapate amani kuliko ilivyo sasa.
   
 5. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Aise me ni mkazi wa chuo kikuu kwaiyo wewe nu mbunge wangu ingawa sikupiga kula (sbb jina langu halikuepo kwenye orodha)!

  Me nna ushauri mdg kwako na chama chako,naomba muache kutoa haya matamko ambayo sisi kama wananchi hatuoni maana yake. Kila mtu anajua selikali ya ccm ni kiziwi kwaiyo haya matamko yatatoka na hayata tatua hayo matatizo kbs. Wewe shaidi yangu nyinyi kama chadema mmeshatoa matamko mangap?na mangapi yameleta utofauti au selikali imeyafanyia kazi?

  Kwa maono yangu me nayaona haya matamko kama tume zinazoundwa na selikali ambazo hazileti utofauti wowote. Nashauri mje na njia mpya za kuwashinikiza jawa watu wawe wanasikia kilio chetu. Too bad siwezi kushauri tufuate mfumo au njia gani ila hilo halinizuii kusema kua haya matamko yenu yamenichosha kwakwel.

  Asante sana
   
 6. i

  iwensato Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni haki kulipa wenye nyumba ambazo tayari zilikwishalipwa lakini zikauzwa kwa wengine wasiojua?
   
 7. o

  oyoyoo Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyika anatafuta sifa za kitoto na kijinga. Kuna mtu leo hapa kamuomba atafute suluhisho la foleni ya barabara ya Morogoro sasa itaondokaje kama barabara hazitapanuliwa. Na, je, kama mtu kajenga katika road researve watu wake kujadiliana wakati wananchi na uchumi wa nchi unaharibika kutokana na wakazi wengi kukaa katika foleni. Tatizo la vijana hawa wa upinzani ni kudhani kupinga kila jambo ndio kupata kura ama kulalamika kila wakati ndio kujiona kuwa karibu na wananchi. My take kwa Mnyika: Kugombea ni jambo moja na kushinda na kuongoza ni jingine. Huu si wakati wa kampeni hivyo kama uliwadanganya wananchi ili wakupe kura haya matamko yako hayatasaidia lolote. Ni wakati uwaendee tena na kuwapa ukweli kuwa utawala wa sheria ni mihimu na barabara pia ni muhimu kwa ajili yao na nchi. Wasitazame maslahi yao na kushindwa kutambua njia hupitwa na wote. Tena walio na haki ya kulipwa siamini kama wataachwa maana utaratibu wa malipo umekuwa ukifanyika na inaposhindikana huwezi kumbomolea nyumba mtu bila kufuata sheria, hivyo wanaweza kwenda mahakamani na mahakama kuamua vinginevyo
   
 8. M

  Mundu JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mimi sioni tatizo la Mnyika na hilo tamko lake. kwanza kwa mujibu wa maelezo hayo, ni eye opener kwa watu wengi humu ndani. Pia ameeleea kipi kitafuata baada ya yeye kurudi Darisalama. Labda lisomwe tena vizuri hilo tamko!

  Serikali ya kipuuzi ya CCM, kama kweli inaona mbali, ile barabara ingepanuliwa kwa kiasi cha kutosha wakati wanapanua barabara ya Ubungo Mlandizi. Macho yao ni madogo kama goroli, na hivyo walishindwa kuona mbali. Hata miaka kumi haijafika, barabara eti imezidiwa na magari.

  Ni wizi tu na 10% zinawasumbua, ndio mara fikra na mawazo yao wanafanya nusunusu.

  Kila mtu (waziri) anakuja na vision yake...akiondoka, hakuna linalokuwa endelevu! Where is the council, (town) master plan? Where is the country roadmap ambayo hata akija shetani, ataifuata na kuisimamia??

  Eti watu wanashauri, wananchi waende mahakamani? mahakama gani hiyo ipo kwa ajili ya wananchi hapa nchini? watu wameuwawa waziwazi hapa na mapolisi na hakuna askari yeyote aliyechapwa hata kiboko. hakuna kitu ni ubatili mtupu wa kiserikali hiki.
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hivi umesoma vizuri tamko la Mnyika au umekurupuka tu na kuanza kuandika!!! Soma mwisho wa tamko lake. Amesema hapingi suala lolote linalolenga kuleta maendeleo kwa nchi ila sheria zilizopo ziheshimiwe na wadau/wahusika wanapashwa kuelimishwa badala ya kutumia ubabe wa kupita na kuweka X. Amejitolea vile vile kupita na kuyaona maeneo husika. Sasa hicho unachokiita ni sifa za kitoto ni kipi hapa?

  Kama huko kazini, naomba unisamehe!!!!

  Tiba
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa ualewa wangu tamko ni msimamo, sasa hutakia atoe msimamo wake...CDM/Mnyika aendelea kutoa matamko hata kama yatafika 1000 ndani ya mwaka mmoja poa.....halafu tubaki sisi wananchi kuchukua hatua
   
 11. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mendelo hayawezi kutokea katika makaburi ya wengine. Kujenga barabara ya kupunguza foleni isiwe kaburi kwa wenye maeneo karibu na barabara. Alichosema Mnyika ni sahihi kabisa.
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi aliyewaambia kuwa kupanua barabara ndiyo suluhisho pekee la foleni barabarani? Ingekuwa hivyo basi Marekani na sehemu nyingine zilizoendelea zisingekuwa na foleni. Inajulikana wazi kila unapopanua barabara ndivyo magari yanavyozidi kuongezeka. Bila kuangalia mfumo mzima wa jiji letu ( kuwa na central business district moja, kutokuwa na njia mbadala za kusafirisha wananchi n.k.) hatutatatua tatizo hili hata tujenge flyovers ngapi!

  Mheshimiwa mbunge anafanya alichoagizwa nacho ni kutetea watu wa jimbo lake wasinyimwe haki yao. Tofauti na tulivyozoea anafanya hivyo kwa uwazi mkubwa. Badala ya kumbeza ilitakiwa tumuunge mkono na kumhimiza afanye zaidi.

  Amandla........
   
 13. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  huu ndio ujinga unaoturudisha nyuma. Mtu kajenga kwenye eneo si lake unaongea nae nini? Wacha wabomolewe barabara zijengwe. Tumepata waziri chapa kazi tusiingize siasa mwache awajibike. Mnyika unaanza vibaya! Statement yako upuuzi mtupu.
   
 14. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa wewe umeandika nini hapa tofauti na Mnyika. Issue hapa ni kufuata taratibu za kisheria tu. Na taratibu za kisheria zina mlolongo wake, sio tu kusoma sheria inasemaje halafu unafanya maamuzi. Lazima watu wachambue evidences zote kabla ya kufanya maamuzi.
   
 15. N

  Nanu JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani hapingi, bali anasema kama serikali kupitia waziri husika ilipanua barabara na tayari watu walikuwa wameshagawiwa basi kwa wale ambao wako nje ya mita 60 yaani kati ya mita 60-120 walipwe fidia kama hawajalipwa. kama wamelipwa ni heri.
   
 16. Marunda

  Marunda Senior Member

  #16
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani ndugu unaulimbukeni wa uelewa wa sheria. Highway kutoka Ubungo hadi mbezi road reserve kutoka centre ya barabara ni 70m each side. Lakini TANROADS wanaweka alama za X upto 90m.

  Nani wakuwasemea hawa wananchi kama si mwakilishi wao kama mnyika. Hata kama kuna mabadiliko ya sheria kwa nini wasielimishwe kabla ya kufanya hivyo?

  Usipende kulaumu kabla ya kujua sababu.
   
 17. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280

  Kweli wewe oyooyoo! Wewe ndo wale wanaodhani kua DART na upanuzi wa daladala ndo suluhisho la foleni Dar! Pole ndugu!

  Amandlah.
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hata na mimi hiyo kauri sijaipenda kabisa. Unless ni makubaliano ya ndani kwa ndani. So far Rais wetu ni Dr. Slaa, sasa kama CDM wanataka kumtosa baada ya kazi yake kubwa haitapendeza. Hiyo kampeni nafikiri Kijana kachemka na ikiwezekana aifute haraka kwani watu bado wana uchungu wa kuibiwa kura last year yeye kishakuja na mgombea mwingine!!
   
 19. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ""NAMUUNGA MKONO FREEMAN AIKAELI MBOWE AGOMBEE URAISI 2015"" [/QUOTE]

  Mkuu hiyo sijakubaliana nayo, itatuangusha. Au unaonaje?
   
 20. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Uandishi huu sio wa mwanafunzi wa chuo Kikuu!
   
Loading...