Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,852
Sasa kwa nini huo wingi wa magari unaonekana kwenye makutano tu?
Halafu, ni kuwa impractical kutufananisha na France. Too utopian. Tanzania yetu hii mmejaa mafundi mchundo ambao hata kujenga kibarabara hamuwezi (asingekuwepo Mchina hapa, ushamuona Mchina anajenga barabara Paris? Kama umepita/umeishi hiyo miji ya Magharibi na Latin America, tuambie, ushaona Mchina kavaa helmet Copenhagen huko?), ndo tutaweza kujenga hiyo mipango miji ya La Defense na Brazil, please!
Ndo maana, kwa kuanzia, napendekeza kinachowezekana. Small-minded you may call it, but it is the practical model you can be afford technically and fiscally.
Mkuu, neno "peke yake" unalielewa lakini? Taa, makutano n.k. zote zinachangia kuleta foleni lakini si main cause. Sababu kubwa ni watu wengi kuelekea upande mmoja kwa wakati mmoja. Hii inasababishwa na watu wanakoishi na wanakoenda kujitafutia riziki, starehe, manunuzi ya kawaida n.k. Haya yote yanatokana na jinsi mji ulivyopangwa na si taa au sheli.
Kumbe tatizo lako ni mafundi mchundo? Kwa vile haujaona mswahili amevaa helmeti basi unataka kututosa wote? Hivi unadhani hizo unazoita overpass atajenga nani? Mbona siku hizi karibu kila kitu kinatengenezwa uchina, basi ina maana kuwa hao wa nchi za magharibi wamekuwa hamnacho? Hivi kama unataka kujipima afya, utajifananisha na mgonjwa? Mifano niliyokutolea inahusu mipango miji, na kinachotakiwa ni ubunifu tu ili kuhakikisha utatumia fedha kiduchu ulizokuwa nazo kwa ufanisi zaidi.
Unachopendekeza ni utopian, based kwenye picha za fly-over za nchi za magharibi bila kujua adha zake. Na ni kweli small minded kwa maana ni mfano wa jinsi tunavyopenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Kama vile kumkata mtu mguu kwa vile ana kidonda bila kuchunguza chanzo cha kidonda.
Kwa vile inaelekea uko hapa kubishana na si kujadiliana basi naona heri nikuachie forum.
Nilikuwepo.
Amandla......